Minembwe: mwanajeshi mmoja na mchungaji waliuwawa kwa siku mbili

Minembwe: mwanajeshi mmoja na mchungaji waliuwawa kwa siku mbili

Mwanajeshi wa FARDC ( jeshi la jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo) aliuwawa jumatano hii asubuhi eneo la Minembwe. Ni katika wilaya ya Fizi mashariki mwa Kongo . Katika eneo hilo, mchungaji mmoja aliuwawa jumatatu, mauwaji yalidaiwa kufanywa na askali wa FARDC. HABARI SOS Médias Burundi

Mwanajeshi aliyeuwawa ni wa brigedia ya 12 ambayo inapiga kambi eneo la Minembwe. Kulingana na vyanzo vya kijeshi, watu wenye silaha waliopiga risasi wanadaiwa kuwa wapiganaji wa kundi la Twirwaneho linaloundwa na jamii ya Banyamulenge.

” Walimuuwa wakati akielekea kuchota maji katika mto wa Runandu”, wanasema askali wenzake.

Kifo cha mwanajeshi huyo kilisababisha taharuki katika kanda hiyo inayokaliwa na rai a wa Kongo wa jamii ya Banyamulenge, wanaofananishwa na makabila mengi na raia wa Rwanda.

” Wake wa askali jeshi walifanya mandamano. Wanasema kuwa wanataka kuwafukuza raia wa Rwanda watoke kwenye ardhi ya Kongo. Walipiga mawe kwenye maduka yanayomilikiwa na Banyamulenge kwenye kituo cha Madegu”, wanasema mashahidi.

Kisa hicho kilitokea baada ya mauwaji ya mchungaji mmoja wa jamii ya Banyamulenge ijumatatu.

Muzima Rugamba alikuwa katika kundi la watu wakati alipouwawa.

” Watu wengi walikuwa ndani ya nyumba kwenye kituo cha Madegu. Walikuwa wamejificha mvua. Wanajeshi walikuja na kuchukuliwa kila kitu walichokuwa nacho, simu za mkononi na pesa …..Kabla ya kwenda, walimupiga risasi mchungaji Muzima na kufariki papo hapo”, wanasema mashahidi.

Jeshi la Kongo lilifahamisha kuwa uchunguzi ulianzishwa kuhusu kesi hiyo. Kwa mjibu wa vyanzo vyetu, askali jeshi watatu waliouwa mtu huyo wa Mungu wanahudumu katika brigedia ya 12.

” Watuhumiwa walikamatwa” vyanzo vyetu katika taasisi za usalama vinasema.

Takriban raia 20 waliuwawa eneo la Minembwe tangu mwaka wa 2020, kumi kati yao wakiwa waliuwawa na wanajeshi kwa mjibu wa mashirika ya kiraia ya ndani.

Kisa kilichosababisha hasira nyingi ni kile cha kijana mwanafunzi aliyeuwawa kwa mapanga na askali jeshi mwanzoni mwa oktoba iliyopita.

Katika ukanda huo, ng’ombe laki tatu waliporwa na makundi ya silaha pamoja na FARDC tangu 2017 kwa mjibu wa viongozi wa wafugaji katika ukanda huo.

Msemaji wa kundi la silaha la Twirwaneho hakupatikana ili kujieleza kuhusu madai hayo.

Previous Nyanza-Lac: two people seriously injured following a land dispute
Next Bubanza: explosion of school dropouts due to hunger