Nduta: watu 10 wanaomba hifadhi wazuiliwa jela

Nduta: watu 10 wanaomba hifadhi wazuiliwa jela

Watu kumi wenye asili ya Burundi wanaomba hifadhi ya ukimbizi hivi karibuni walikamatwa na polisi ya Tanzania. Watu hao waliokuwa katika hifadhi ndani ya kambi ya Nduta walikuwa walirudi nchini na kurejea uhamishoni. Wanadai kuwa walinyanyaswa wakiwa katika maeneo yao ya asili na kuamuru kurudi nchini Tanzania.Wanahofia kufukuzwa . HABARI SOS Médias Burundi

Waomba hifadhi hao ni wanaume sita, akimama wawili na watoto wawili.

” waliwasili katika kambi ya Nduta wiki iliyopita na hawakujielekeza moja kwa moja kwenye kituo cha mapokezi. Walipenda kulala kwa marafiki zao sababu wanaifahamu vizuri kambi hiyo ambako waliishi kwa miaka mitano kabla ya kurudi nchini mwanzoni mwa mwaka huu”, alifahamisha mkimbizi aliyekuwa eneo la tukio.

Walikamatwa na polisi na kuzuiliwa jela baada ya taarifa zao kutolewa kwa polisi na wenzao.

” Walituhumiwa kukaa pasina kibali. Wanakabiliwa na hatari ya kufukuzwa sababu Tanzania haitowi tena hifadhi ya ukimbizi”, analalamika mkimbizi wa burundi katika kambi ya Nduta.

Hata hivyo, wadau wanahakikisha kuwa walibaguliwa na kunyanyaswa na wakaazi wa vijiji vyao vya asili katika mikoa ya Makamba na Ruyigi (kusini-mashariki) kwa tuhma za kuharibu sura ya nchi na kujiorodhesha katika makundi ya waasi”. Wanaomba kupokelewa kama wakimbizi wapya nchini Tanzania.

Raia wenzake wanaelewa madai yao.

” Iwapo mtu amerudi katika huu umasikini na kuacha nchi yake, kwa vyovyote vile angetakiwa kupokelewa sababu ni ushahidi kuwa ananyanyaswa, hata na sisi tuna mpango wa kutoka ndani ya kambi lakini tunakosa mahala pa kwenda” , wanasema.

Warundi hao waliwasili Tanzania kwa wakati mbaya sababu wiki iliyopita, viongozi wa nchi hiyo walifahamisha kuwa wako na mpango wa kufukuza wakimbizi wa zamani waliorudi ukimbizini.

Kwa jumla zaidi ya warundi 1048 wanalengwa na hatua hiyo. Ni wakimbizi wa zamani waliorudi uhamishoni katika kipindi cha miaka miwili iliyopita baada ya kurejea nchini Burundi. Wahusika wanaomba serikali ya Tanzania kusimamisha hatua yake na kuzidi kuwa sababu zilizowapelekea kutoroka nchi bado ziko pale pale.
Kambi ya Nduta ina wakimbizi wa Burundi zaidi ya elfu 76.

Previous Kirundo: Imbonerakure auwawa na wenzake
Next Gitega: the price of food products goes up to double, residents are worried