Kirundo: Imbonerakure auwawa na wenzake
Mwanaume wa miaka 41 aliuwawa asubuhi ya siku ya alhamisi eneo la Rwimbogo kijiji cha Rushubuje tarafa ya Ntega (Mkoa wa Kirundo kaskazini mwa Burundi). Muhanga huyo aliyekuwa Imbonerakure (Kijana mjumbe wa tawi la vijana wa chama tawala cha CNDD-FDD) alipigwa vikali na wenzake kwa tuhma za kuvunja Siri kuhusu makosa yanayofanywa na kundi. HABARI SOS Médias Burundi
Habiyambere (miaka 41) alikamatwa na kundi la Imbonerakure usiku wa jumatano majira ya saa nne za usiku.
Vijana hao Imbonerakure ambao kiongozi wao ni Nzobarinda alikuwa akiwashambulia mwanaume na mwaname mmoja waliokuwa wakiongea baada ya kwenda kwenye kilabu cha pombe.
“Habiyambere alikuwa amekuja kumtafuta mkubwa wa Imbonerakure katika eneo la Rwimbogo kwa jina la Nzobarinda ambaye walikuwa wakiendesha wizi kwa pamoja”, vyanzo vya ndani vinasema.
Alimuuliza wapi alikuwa anakwenda nyakati hizo za saa nne na akajibu kuwa anakwenda kwake Nzobarinda.
Kwa mjibu wa vyanzo vyetu, Nzobarinda alikuwa na chuki dhidi yake sababu alikuwa akituhumu kuvunja siri, yeye na Imbonerakure wengine wanafanya wizi usiku wakiwa na mkuu wa Imbonerakure.
Nzobarinda aliamuru Imbonerakure wengine kumpa ” adhabu”
” Hata atakata pumzi yake ya mwisho. Nitajihusisha na ya kufuatia” alihakikisha Nzobarinda.
walimpiga muhanga na kumuacha eneo hilo akiwa mahtuti.
” Hatuelewi namna aliweza kufika kwake. Majira ya saa nane za usiku alhamisi, tulimupeleka kwenye kituo cha afya akiwa katika hali mbaya. Alikuwa akitapika na kukojoa damu. Alifariki majira ya saa kumi na moja za asubuhi kwenye kituo hicho cha afya” alithibitisha mjumbe wa familia yake.
Familia ya muhanga inaomba sheria ifanye kazi.
” Waliohusika wanajulikana. Hadi sasa vyombo vya sheria bado kuwajibika na kuwakamata watuhumiwa.
Watuhumiwa wanasema kuwa muhanga alifumaniwa akijaribu kutoboa nyuma ili aweze kuingia na kuiba ndani.
Shirika la ndani la haki za binadamu linaomba waliofanya mauwaji hayo wakamatwe mara moja. Yanaomba pia kiongozi wa tarafa ya Ntega , Pierre Claver Mbanzabugabo kuacha ukimya wake sababu tarafa hiyo imekuwa uwanja wa mauwaji.
Viongozi wa tarafa hawajasema lolote kuhusiana na madai hayo.
About author
You might also like
Nairobi conclave: the Congolese government speaks of a last chance for armed groups
The Congolese government’s special envoy to the Nairobi talks warns the rebel movements that will not respect the Nairobi agreements. They will be completely eradicated by the regional force, warned
Goma-Gavana mwanajeshi kwa wananchi: askali jeshi wa kikosi cha EAC sio maadui zetu
Gavana wa kijeshi wa mkoa wa kivu kaskazini aliwaomba wananchi wakaazi wa mkoa huo kuacha kushambulia kwa maneno askali waliotumwa mashariki mwa DRC chini ya kikosi cha kikanda cha jumuiya
Goma: nearly 80 people killed in less than a month
According to the local civil society, at least 80 people have been killed in the city of Goma, capital of the province of North Kivu in the east of the