Kivu-kaskazini: jeshi la Kongo na mashirika ya kiraia yanatuhumu kundi la M23 kuwauwa raia wa kawaida, wanaomba uchunguzi huru ufanyike

Kivu-kaskazini: jeshi la Kongo na mashirika ya kiraia yanatuhumu kundi la M23 kuwauwa raia wa kawaida, wanaomba uchunguzi huru ufanyike

Ma mia ya raia wa kawaida waliuwawa na watu wenye silaha wanaofanana na waasi wa kundi la machi 23 (M23) wiki hii katika kijiji cha Kisharu, eneo la Binza na Kishishe kijiji cha Bambu katika wilaya ya Rutshuru, kivu-kaskazini, mashariki mwa DRC, kwa mjibu wa mashirika ya kiraia na angalau raia wengine kuuwawa na M23, kwa mjibu wa jeshi la Kongo. Kundi hilo la waasi linakanusha madai hayo. Linasema ni kampeni inayolenga kuchafuza sura yetu na kutuharibia uhusiano na wananchi. Waasi wa M23 wanaomba uchunguzi ufanyike. HABARI SOS Médias Burundi

Visa hivyo vilifanyika katika kipindi cha siku nne kati ya jumapili na jumatano, kwa mjibu wa madai hayo.

Waasi wa M23 waliingiza kwa nguvu angalau vijana 15 katika wapiganaji wao kwenye vijiji vya Kako, Bambo na Tongo, kwa mjibu wa vyanzo vya ndani.

Habari hiyo zinathibitishwa na mbunge wa wilaya ya Rutshuru ( mkoa wa Kivu-kaskazini) anayelaani hali hiyo.

Mashirika ya kiraia ya ndani yanafahamisha kuwa kati ya waliofariki ni pamoja na akinamama, vijana na watoto na miili yake bado haijazikwa.

Katika tangazo hilo, FARDC (jeshi la jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo) siku ya alhamisi linatuhumu kundi la M23 kuwauwa angalau raia wa kawaida 50. Mashirika ya kiraia ya ndani yanahakikisha kuwa idadi ya waathiriwa iliongezeka baada ya kugundulika miili mingine siku ya alhamisi eneo la Bwito.

Jeshi la Kongo lilituhumu tena M23 na Rwanda kuwa nyuma ya mauwaji ya Kisheshe. Rwanda imekuwa ikikanusha mara kwa mara madai hayo kwamba Rwanda inawaunga mkono waasi.

Msemaji wa katibu mkuu wa UN, Stéphane Dujarric alifamisha kuwa ” Monusco ( ujumbe wa umoja wa mataifa) alipata habari kuwa kuna mapigano kati ya kundi la M23 na waasi wa Mai Mai eneo hilo.

Kundi la M23 lilitoa tangazo tarehe mosi disemba ambamo linapinga ” kuwauwa raia wa kawaida”. Linapinga madai hayo yanayolenga kuchafua sura ya kundi hilo na kuharibu uhusiano na wananchi katika eneo chini ya udhibiti wao”.

Wanaomba uchunguzi huru ufanyike.

” Kundi letu linatupilia mbali madai hayo dhidi yake ambayo hayana msingi na kulaani uchonganishi na wananchi kwa lengo la kuanzisha vurugu ambazo zitakakiwa sana na serikali ya Kinshasa na washirika wake”, yanasomeka ndani ya tangazo hilo.

M23 inatahadharisha kuhusu ” mauwaji ya halaiki yanayoendelea eneo la Masisi”. Yanasisitiza juu kuwepo mjadala wa moja kwa moja na serikali ya Kongo.

Previous Mkutano wa Nairobi: wawakilishi wa jamii ya Banyamulenge waajiondoa katika mazungumzo
Next Cibitoke: nine bodies of Rwandan rebels found in Kibira