Mkutano wa Nairobi: wawakilishi wa jamii ya Banyamulenge waajiondoa katika mazungumzo

Mkutano wa Nairobi: wawakilishi wa jamii ya Banyamulenge waajiondoa katika mazungumzo

Wawakilishi wa jamii ya Banyamulenge walisusia mazungumzo ya Nairobi tangu alhamisi. Hoja, ni shambulio lililosababisha vifo vya watu saba wajumbe wa jamii hiyo mkoa wa kivu-kusini (Mashariki mwa RDC) tarehe 30 novemba. HABARI SOS Médias Burundi

Kulingana na tangazo la siku ya alhamisi, wawakilishi wa jamii ya Banyamulenge wanasema ni hali ambayo hawawezi kuvumilia na kukubali.

Wanalaani shambulio hilo la kundi la Mai Mai kwa ushirikiano na waasi kutoka Burundi wa Red Tabara katika milima mirefu ya Minembwe mkoa wa Kivu kusini mashariki mwa DRC.

” Watu saba waliuwawa katika shambulio hilo na 10 wengine kujeruhiwa” kulingana na tangazo la wawakilishi wa jamii hiyo.

Wanaomba serikali ya Kongo na mpatanishi wa EAC ” kulaani shambulio hilo la 30 novemba na mashambulizi mengine yanayofanyika katika wilaya ya Mwenga, Uvira, Itongwe na Fizi tangu april 2017 na ambayo malengo yake ni kutokomeza kabila “

Mazungumzo hayo hata hivyo yalicheleweshwa kwa masaa mengi siku ya alhamisi. Ujumbe kutoka serikali ya Kongo walipata wasi wasi kuwa siri za mjadala wawo zinavuja kuelekea nchi jirani kupitia vifaa vilivyowekwa ndani ya mitambo ya kutafsiri lugha, walihakikishia SOS Media Burundi washiriki katika vikao hivyo.

” Tunaomba yafukuzwe makundi ya silaha yaliyosababisha mauwaji hayo na adhabu zichukuliwe dhidi yao sawa na yale yaliokubaliwa na pande zote zinazoshiriki mazungumzo hayo na kutanzagwa rasmi na mjumbe maluum wa rais katika mazungumzo hayo” alifafanua Enock Ruberangabo, mmoja wa wawakilishi wa jamii ya Banyamulenge mjini Nairobi.

Kwa mjibu wake, “Haina maana yoyote kuendelea na mazungumzo wakati mashambulizi yakiendelea uwanjani, kinyume na walichoafikiana.”

Previous North Kivu: the M23 accused of murdering civilians demands an independent investigation
Next Kivu-kaskazini: jeshi la Kongo na mashirika ya kiraia yanatuhumu kundi la M23 kuwauwa raia wa kawaida, wanaomba uchunguzi huru ufanyike