Nyanza-Lac: mpasuko kati ya wajumbe wa kamati ya kushughulikia migogoro kwenye baraza la tarafa

Nyanza-Lac: mpasuko kati ya wajumbe wa kamati ya kushughulikia migogoro kwenye baraza la tarafa

Inaripotiwa hali ya kutoelewana kati ya wajumbe wa kamati ya mkoa yenye jukumu la kusuhulisha migogoro kati ya wajumbe wa baraza la tarafa la Nyanza-Lac na ofisi ya baraza hilo. Upande mmoja unataka wajumbe wa zamani, wanaotuhumiwa na upande mwingine matumizi mabaya ya fuko la tarafa wabaki kwenye nafasi hiyo. HABARI SOS Médias Burundi

Kamati hiyo iliundwa na gavana wa mkoa wa Makamba (kusini mwa Burundi) François Ngozirazana tangu mwanzoni kabisa wa mzozo wa uongozi katika tarafa ya Nyanza-Lac wiki kadhaa zilizopita.

Kamati hiyo inaundwa na wawakilishi wa uongozi wa mkoa, korti kuu ya mkoa wa Makamba, idara ya ujasusi katika mkoa wa Makamba pamoja na ofisi ya chama tawala cha CNDD-FDD ngazi ya mkoa.

Kwa mjibu wa vyanzo, tume hiyo haikuleta matokeo mazuri kutokana na hali ya kutoelewana iliojitokeza wakati wa uchunguzi.

Pande moja ya wajumbe wa kamati ilitaka kumuunga mkono mkuu wa tarafa ya Marie Goreth Irankunda na wajumbe wa ofisi ya baraza la tarafa na kusimamisha baadhi ya wajumbe wa baraza la tarafa wenye ushawishi mkubwa.

Waliolengwa ni pamoja ni mkuu wa zamani wa tarafa hiyo Jean Claude Nduwimana na mke wa mshahuri wa gavana Évelyne Havyarimana.

Nduwimana tayari anazuiliwa katika gereza la polisi tarafani Nyanza-Lac.

Mpasuko mkubwa ulianza pale ambapo ilitolewa waranti ya kukamatwa kwa Évelyne Havyarimana mjumbe wa baraza hilo na mwanamke peke mfuasi wa chama cha chama cha CNDD-FDD.

Alilengwa sababu kundi la wale wanaounga mkono Marie Goreth Irankunda wanaamini kuwa iwapo mkuu wa tarafa wa sasa atafukuzwa, Évelyne Havyarimana atachuwa nafasi ya kuu wa tarafa ya Nyanza-Lac.

Baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo walipinga kukamatwa kwake. Badala yake, waliomba bila mafanikio uchunguzi ufanyike kuhusu tuhuma dhidi ya ofisi ya baraza la tarafa. Baada ya kushuhudi hali hiyo, walikataa kusaini ripoti ya kikao hicho.

Tangu mwanzoni mwa wiki hiyo, kamati ya uchunguzi inayoundwa na washahuri wa mwendeshamashtaka mkuu wa mahakama ya rufaa mkoani Makamba ilianza uchunguzi kuhusu makosa yanayotuhumiwa ofisi ya baraza la tarafa.

Kulingana na chanzo, tayari makosa mengi kuhusu matumizi mabaya ya fuko la tarafa yamegundulika.

Baadhi ya wajumbe wa baraza la tarafa wanasema wako tayari kuweka wazi makosa yote ya ofisi hiyo.

Tarahe 2 disemba, wajumbe wa baraza la tarafa la Nyanza-Lac walimufukuza mkuu wa tarafa na ofisi yake wakimtuhumu kutowajibika, matumizi mabaya ya pesa na ubadilifu wa mali ya umma. Marie Goreth Irankunda na ofisi yake wanan’gangana kutoka.

Previous Gitega: two unsolved murders in the districts of Gishubi and Mutaho
Next Uganda: mahakama ya ICC inathibitisha kifungo cha miaka 25 dhidi ya raia wa Uganda Dominic Ongwen