Uganda: mahakama ya ICC inathibitisha kifungo cha miaka 25 dhidi ya raia wa Uganda Dominic Ongwen
Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC alhamisi hii iliidhinisha adhadu ya kifungo cha miaka 25 jela kwa kosa la uhalifu wa kivita na dhidi ya binadamu wa Dominic Ongwen zamani kiongozi wa kivita. Kwanza alikuwa mtoto jeshini na badaye akageuka mmoja kati ya makamanda wa kundi la waasi la wapiganaji wa Mungu la LRA katika miaka ya 2000. Chumba cha rufaa cha mahakama hiyo ya kimataifa kilitoa maamuzi yake na kuidhinisha uamzi wa korti hiyo kuhusu hatma yake na adhabu zake. Katika maamuzi yake, chumba cha awali cha mahakama hiyo kilitangaza kuwa Dominic Ongwen alipatikana na makosa 61 ya uhalifu wa kivita na dhidi ya binadamu aliyotenda kaskazini mwa Uganda kati ya tarehe mosi julai 2002 na 31 disemba 2005 na alikuwa amekatiwa adhabu ya kifungo cha miaka 25 na mahakama hiyo. HABARI SOS Médias Burundi
Jaji Ibanez Carranza aliyewajibika kama jaji mkuu katika kesi ya rufaa, alizungumzia ugumu wa maswala yaliyoibuliwa na upande wa utetezi.
Jaji huyo alisisitiza pia kuwa kesi hiyo inamuhusisha mtuhumiwa mmoja ambaye alitekwa na kundi la wapiganaji wa Mungu la LRA akiwa na miaka tisa na kumpa mafunzo na kumuingiza katika wapiganaji wake.
Licha ya historia yake na unyanyasaji aliyoishi, majaji katika chumba cha awali waliamuru kuwa bwana Ongwen alitakiwa kuwajibishwa juu ya jukumu lake katika maovu yaliotendwa na kundi la LRA”.
Katika kesi hiyo ya rufaa dhidi ya bwana Ongwen, chumba cha rufaa kilitathimini na kilitupilia mbali madai 90 yaliyoibuliwa na upande wa utetezi.
Chumba cha rufaa badaye kilithibitisha kwa kauli moja uamzi kuhusu hatma ya mtuhumiwa huyo ndani ya kesi hiyo. Chumba hicho kwa kauli moja kilipasisha na kuidhinisha adhabu dhidi yake. ” uamzi kuwa alihusika na adhabu alizokatiwa ziliidhishwa mara moja”.
Dominic Ongwen, alitekwa na kundi la wapiganaji la LRA chini ya uongozi wa Joseph Kony akiwa njiani kuelekea shuleni akiwa na miaka tisa. ICC ilitangaza pia kuwa itaanza kesi dhidi Joseph Kony hata kama bado hajakamatwa”.
Akivalia suti nyeusi na tayi, bwana Ongwen hakusikiliza maamuzi ya kesi dhidi yake, aliendelea kuonyesha kwa ishara ya mkono kuelekea umaa unaosikiliza.
Upande wa utetezi unadai kuwa ” adhabu dhidi yake zingetakiwa kusimamishwa sababu yeye mwenyewe ni muathiriwa wa kundi la LRA kama mtoto mwanajeshi”.
Kundi la LRA linatuhumiwa mauwaji ya zaidi ya watu laki moja na kuteka watoto elfu 60 wa kiume ambao waligeuzwa kuwa wanajeshi huku akinadada wakigeuzwa kuwa watumwa wa ngono kwa mjibu wa takwimu za UN.
You might also like
Kirundo: pregnant women demand free ultrasound
The minister for health suspended the payment of ultrasound bill at the Kirundo hospital (northern Burundi) as is done elsewhere in other public health structures. However, pregnant women who request
Tanzania: 6 Tanzanians received 15 years in prison over taking part in lynching two Burundi refugees
Two Burundians living in the Nduta camp were killed last week over allegation of collaborating with a group of refugees in rapping Tanzanian women who go to the fields and
Zambia : nearly 30 Burundians detained for illegal immigration
Zambian police say they have arrested 29 Burundians for illegal immigration. They went through Tanzania and wanted to reach South Africa. Activists cry out against human trafficking and ask Burundian
