Meheba (Zambia): Malalamiko ya wakulima
Raia wenye asili ya Burundi, Rwanda, na Kongo wanalalamika juu ya kukosa haki ya kujumuika katika vyama vya ushirika. Wanatupilia mbali upendeleo unaofanywa wakati wa kugawa mbolea ya kizungu kwa jamii zingine za wakimbizi wanaoishi katika kambi ya Mebeba nchini Zambia. Wanaomba kujumulishwa na wenyewe. HABARI SOS Médias Burundi
Jamii za warundi, Rwanda na Kongo wanawatuhumu waratibu wa vyama vya ushirika ” kuwakatalia kujiunga na vyama vya ushirika”.
” Vyama vyote vya ushirika vinaundwa na wakimbizi kutoka Angola na Zambia. Tulijaribu kuingia bila mafanikio. Tulipitia kwa wafundi wa kilimo na hapo tukashindwa”. alieleza raia mmoja kutoka Burundi.
Hayo ni wakati mbolea zenye viwango vizuri hutolewa kupitia vyama vya ushirika.
” Kwa franka 350 peke sarafu za Zambia (20 USD), mjumbe wa chama cha ushirika anapata mifuko 6 ya mbolea, kilo 30 za mbegu za mahindi na kilo 10 za mbegu za soya. Hayo ni wakati nje ya vyama vya ushirika, mfuko mmoja wa mbolea bei yake ni kati ya 800 na 1000 sarafu za Zambia ( 46-50 USD), zaidi ya mara mbili “, alibaini mkimbizi mmoja anayedai kuwa hakutendewa haki .
Mkimbizi mwengine alifahamisha kuwa ” kwenye shamba la mita 50 kwa 50, unaweza kutumia mifuko miwili ya mbolea kwa thamani ya kitita cha kwacha 2000 sarafu za Zambia. Na tunalazimika kuweka mbolea mara mbili kwa msimu mmoja ili tupate mavuno mazuri. Ni hali ambayo mkimbizi hawezi kumudu “.
Wakimbizi wa Burundi, Rwanda na Kongo wanaomba nchi hiyo iliyowapa hifadhi na HCR kuingilia kati na kumaliza tatizo hilo.
Ni hatari inayoleta tofauti kubwa kati ya jamii za wakimbizi. Kawaida wakimbizi wote wangetakiwa kuwa na haki sawa”. walisisitiza viongozi wa kijamii ndani ya kambi ya Meheba nchini Zambia.
HCR haigawi tena nafaka za vyakula kwa wakimbizi ispokuwa kwa madhaifu. Makundi ya wakimbizi wengine yanashahuriwa ” kugharamia wenyewe mahitaji yao kupitia shughuli za kilimo na biashara “.
Kambi ya Meheba inapatikana katika msitu mdogo kaskazini-magharibi mwa Zambia. Inahifadhi zaidi ya wakimbizi elfu 27 wakiwemo warundi elfu mbili.
You might also like
Tanzania: wakimbizi wa Burundi wanaomba mwaka huu uwe mwaka wa mateso kupungua
Mwaka wa 2022 wakimbizi wa Burundi wanaoishi katika kambi za Nyarugusu na Nduta wanasema kuwa walikabiliwa na changamoto nyingi na kuathiriwa na manyanyaso mengi. Wanaomba HCR na viongozi wa Tanzania
Terror at Nakivale camp : hunted albinos, a mother and her children mysteriously disappear
SOS Médias Burundi Nakivale, June 10, 2025 – At the Nakivale refugee camp, located in the Isingiro district of southwest Uganda, the albino community is experiencing a growing climate of
Nyarugusu (Tanzania): mkimbizi mwenye asili ya Burundi alipatikana akiwa maiti
Mkimbizi kutoka Burundi mwenye umri wa miaka takriban miaka 40 aliuwawa na watu wasiojulikana karibu ya kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu nchini Tanzania. Polisi inasema ni tukio la wizi lililokwenda
