Burundi-Rwanda: Gitega inataka kuwahakikishia usalama wakimbizi wa Burundi mjini Kigali

Burundi-Rwanda: Gitega inataka kuwahakikishia usalama wakimbizi wa Burundi mjini Kigali

Jumatatu hii, Burundi ilituma wajumbe nchini Rwanda kwa ajili ya kuwahamasisha wakimbizi kutoka Burundi kurejea kwa hiari nchini Burundi. Ujumbe huo inaundwa na watu watano ikiwa ni pamoja na magavana watatu wa mikoa, miwili kati ya mikoa hiyo ikipakana na Rwanda ambayo inawapa hifadhi wakimbizi kutoka Burundi zaidi ya elfu 50. Ujumbe huo haukufanikiwa kuwaridhisha . HABARI SOS Médias Burundi

Wajumbe hao watano wa serikali ya Burundi wamepokelewa kwenye mpaka wa kusini ya Rwanda wa Gasenyi-Nemba. Hao ni pamoja na André Ndayambaje katibu wa kudumu katika wizara ya mambo ya ndani na usalama anayehusika na maswala ya usalama, kanali Léonidas Bandenzamaso gavana wa mkoa wa Bururi (kusini mwa Burundi), Albert Hatungimana gavana wa mkoa wa Kirundo pamoja na kanali Rémy Cishahayo gavana wa mkoa wa Kayanza ( kaskazini mwa nchi)

Walipokelewa kwenye kituo cha mpakani na Philippe Habinshiti katibu wa kudumu kwenye wizara ya Rwanda inayohusika na wakimbizi, Emmanuel Gasana na Alice Kayitesi ambao ni magavana wa mikoa ya mashariki na kusini mwa Rwanda.

Ujumbe huo ulipelekwa haraka mjini Kigali ( mji mkuu wa Rwanda) kwa ajili ya kukutana na wawakilishi wa kamati ya wakimbizi zaidi ya elfu nane kutoka Burundi wanaoishi mjini Kigali.

Mkono unaelekezwa….

Mkuu wa ujumbe huo André Ndayambaje anawakikishia.

” Tumekuja hapa ili kuwafahamisha kuwa sababu zilizowafanya mtoroke nchi hazipo tena, ikiwa ni upande wa usalama na uchumi, rejeeni nyumbani” , amebaini André Ndayambaje ndani ya ukumbi unaojaa wawakilishi wa wakimbizi kutoka Burundi. Kamati ya wawakilishi wa wakimbizi kutoka Burundi wanaoishi mjini Kigali, inaundwa kwa sehemu kubwa na wanaharakati na watu maarufu ndani ya mashirika ya kiraia, viongozi wa zamani wa nchi, wanajeshi wa zamani na baadhi ya wasomi.

Ndani ya ukumbi, wakimbizi walionekana kama hawakuridhika.

” Mazingira mazuri yote yamekamilika ili kuweza kuwapokea kwa shangwe. Tunataka muweze kusaidia katika maendeleo ya nchi. Tuko hapa kama wandugu. Tunataka muje kwa wingi kwa hiari. Hakuna tena sababu ya kuitwa mkimbizi kutoka Burundi”, alisisitiza afisa huyo mkuu katika taasisi ya polisi ya Burundi.

Majibu ya wakimbizi

” Tumeonyesha wazi kuwa kuna waliorudi na badaye wakauwawa, kupotea na wengine waliamuru kurudi uhamiaji hapa au mahala kwingine. Kwa wengine mali zao, nyumba na ardhi vilikamatwa ou kuibiwa na serikali ou wajumbe wake. Harafu kuna waranti wa kukamatwa zinazowakali baadhi yetu hapa. Kwa hali hiyo vipi mnaomba turudi nyumbani katika mazingira hayo?”, alieleza Patrice Ntadohoka mkuu wa kamati ya wakimbizi wasioishi kambini.

Na kuibua maswala ya kisiasa

” Tunaomba katiba ya 2018 iliyorudiria ile ya 2005 na makubaliano ya Arusha isimamishwe, kwa kifupi sheria irudi kufanya kazi ikizingatiwa kuwa korti ya afrika mashariki ilitoa uamzi na kusema kuwa muhula wa tatu ulikuwa kinyume cha katiba”, alifafanua Bwana Ntadohoka.

Na kusisitiza : ” ni kweli, tunaona kuwa rais wa sasa ana nia nzuri, lakini ana washirika wabaya. Washirika wake hawatutaki. Kwanza ashughulikie hayo, harafu sisi tutarudi sababu Burundi ni nchi yetu pia”.

Ujumbe kutoka Burundi ulikuwa unakwepa .

“Ni jambo la kawaida kukimbia nchi kama una sababu zinazoeleweka. Lakini kwa sasa amani na usalama vimeimarika kwenye ardhi yote ya taifa. Harafu baadhi ya taarifa zenu kuhusu nchi sio sahihi, sababu munakaa mbali na nje ya nchi. Tunawakikishia kuwa mutashughulikiwa vizuri. Lakini kuna waliokimbia kutokana na mizozo ya ardhi au kesi, matatizo ya kiuchumi na sababu zingine. Tutaangalia njia ya kumaliza matatizo hayo ili kuondoa vizuwizi vyote”, alibaini André Ndayambaje.

Kigali ilisalia kuwa mpatanishi

Katibu wa kudumu kwenye wizara ya wakimbizi alipongeza Burundi kwa kuanzisha mchakato huo, ambao kwa mjibu wa Philippe Habinshiti ndio suluhu la kudumu kwa swala wa wakimbizi.

” Ni vizuri kuja kuwahamasisha na kujaribu kuwakubalisha wakimbizi kurudi nyumbani baada ya kuwaonyesha hali ya usalama ” alisema.

Serikali ya Rwanda inakubali kuwa itawasaidia wakimbizi kutoka Burundi wanaotaka kurudi makwao.

” Tuko hapa kwa ajili ya kuwasaidia katika mchakato huo wa kurudi nyumbani kwa hiari, lakini kwa wale wanaojihisi kuwa hawana amani, tutaendelea kuwapa hifadhi kama tunavyofanya kwa wakimbizi wengine ” alibaini Philippe Habinshiti.

Gitega inaridhishwa na ushirikiano huo wa Kigali

” Tumepata ushirikiano tofauti kama kutoka wizara ya maswala ya nje ya nchi, wizara ya wakimbizi lakini pia HCR. Tuliwaomba pia watusaidie katika ratiba ya kurejesha wakimbizi kwa hiari. Walikubali kutusaidia. Tunataka kuwaondolea mzigo huo wa wakimbizi wa Burundi serikali ya Rwanda” alihakikisha mkuu wa ujumbe kutoka Burundi.

Jumanne hii, ujumbe huo utaelekea katika kambi ya Mahama inayowapa hifadhi wakimbizi 39 elfu kutoka Burundi.

Kampeni hiyo inafanyika kwa mara ya kwanza tangu 2015 kwa wakimbizi hao zaidi ya elfu 80 kutoka Burundi waliokimbilia nchini Rwanda kati kati ya mzozo uliosababishwa na muhula mwingine wa rais Pierre Nkurunziza uliokuwa wa utata.

Kulingana na MINEMA (wizara ya Rwanda inayohusika na wakimbizi) zaidi ya wakimbizi kutoka Burundi elfu 30 walirudi nchini kwa tangu 2020. Hata hivyo wizara hiyo inahakikisha kuwa hakuna utashi mkubwa kwa wakimbizi wa Burundi kurejea kwa hiari.

Kwa sasa zaidi ya wakimbizi kutoka Burundi elfu 50 wanapewa hifadhi nchini Rwanda, idadi kubwa wakiishi ndani ya kambi ya wakimbizi ya Mahama.

Kampeni hii inajiri miezi miwili baada ya mipaka kati ya mataifa hayo mawili ya maziwa makuu kufunguliwa rasmi.

Mwezi uliopita, ujumbe kama huo ulikuwa nchini Tanzania katika kambi ya Nyarugusu ambako ulitangaza kuwa taifa hilo dogo la afrika mashariki lina mpango wa kurejesha wakimbizi elfu 70 katika mwaka wa 2023.

Previous Meheba (Zambia): Malalamiko ya wakulima
Next Bujumbura: hali inakuwa ngumu kwa aliyekuwa waziri mkuu Alain Guillaume Bunyoni