Bujumbura: hali inakuwa ngumu kwa aliyekuwa waziri mkuu Alain Guillaume Bunyoni

Bujumbura: hali inakuwa ngumu kwa aliyekuwa waziri mkuu Alain Guillaume Bunyoni

Jumanne hii alasiri, mawajeshi na polisi walinzi wa makaazi ya aliyekuwa waziri mkuu Alain Guillaume Bunyoni wamerudishwa katika kambi zao. Hayo ni baada ya msako kufanyika kwenye makaazi yake binafsi ya Gasekebuye kusini mwa jiji kuu la kibiashara la Bujumbura.Atakuwa na haki ya kulindwa na askali polisi watano peke na nyakati za mchana. HABARI SOS Médias Burundi

Ni askali polisi na jeshi wa kikosi maluum cha kulinda taasisi na viongozi wakuu wa nchi akiwemo rais na mkuu wa chama tawala cha CNDD-FDD.

Kwa mjibu wa vyanzo vya usalama ambavyo vimeomba majina yao yahifadhiwe,” vituo vya doria kwenye makaazi ya kibinafsi ya aliyekuwa waziri mkuu vimebomolewa ” jumanne hii alasiri.

Majira ya asubuhi, afisa huyo ambaye hakuwahi kuishi katika makaazi ya ma waziri wakuu na makamu wa rais wamepokea wahudumu wa SNR( idara ya ujasusi) na askali polisi ambao wamefanya msako kwenye makaazi yake, vyanzo vya karibu na faili hiyo vimetoa ushahidi huo.

” Hakuna vitu vya haramu vilivyokamatwa. Lakini gari zote za kazi zimechukuliwa kwa idara ya usalama”, shahidi mmoja amesema.

Kwa mjibu wa vyanzo vyetu, askali polisi na jeshi waliokuwa walinzi wa makaazi ha waziri mkuu wa zamani wametumwa katika kambi zao.

Polisi watano peke ndio wanasalia kumlinda. Wanatakiwa kutoka eneo hilo nyakati za usiku”, kinahakikisha chanzo cha polisi.

Chanzo kingine cha usalama kimeambia SOS Médias Burundi aliyekuwa waziri mkuu huenda akasimishwa na ” .Chumba chetu cha habari, hakijanikiwa kujuwa wapi imetoka amri ya kumunyanganya wakinzi. Lakini vikosi hivyo viwili vinavyohusika na kulinda taasisi na viongozi wakuu wanapewa amri na watu wa karibu na rais , waliomufukuza mwezi septemba mwaka huu

Wiki iliyopita wakati rais wa Burundi akiwa nchini Marekani kuhudhuria mkutano kati ya Marekani na nchi za afrika, nchi hiyo yenye nguvu duniani kwa mara nyingine ilimurudisha Alain Guillaume Bunyoni kwenye orodha ya watu wanaokabiliwa na vikwazo.

Marekani inamtuhumu kushiriki katika “visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu”.

Afisa huyo amekuwa akitajwa katika ripoti za mashirika ya kimataifa kwa tuhuma : visa vya rushwa na kuwanyanyasa wapinzani” katika nchi hiyo ndogo ya afrika mashariki pamoja pia na Congo.

Previous Burundi-Rwanda: Gitega inataka kuwahakikishia usalama wakimbizi wa Burundi mjini Kigali
Next Burundi-EAC: Joseph Ntakarutimana alichaguliwa kuwa spika wa bunge la EALA