Kivu-kaskazini : mandamano dhidi ya ziara ya rais Macron nchini DRC yanafahamisha bila ushawishi mkubwa

Kivu-kaskazini : mandamano dhidi ya ziara ya rais Macron nchini DRC yanafahamisha bila ushawishi mkubwa

Mandamano hayo yaliandaliwa alhamisi hii mjini Goma tangu asubuhi. Makundi ya ushawishi pamoja vuguvugu la wananchi yanapinga ujio wa rais wa ufaransa Emmanuel Macron nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo. Mandamano hayo yamesusiwa na viongozi wakuu wa vuguvugu la wananchi na makundi mengine ya ushawishi ambao wanakumbusha kuwa Ufaransa ilichangia pakubwa ili kuondoa vikwazo dhidi ya kuingiza silaha nchini DRC. HABARI SOS Médias Burundi

Kwenye mabango ya wandamanaji, imeweza kusomeka : ” tunapinga ujio wa Macron nchini DRC”, ufaransa ni mshirika mnafiki “, Macron ni sawa-Rwanda, Macron ni sawa na M23”.

Wandamanaji wameteremka kuelekea eneo la cercle sportif ya Goma ( makao makuu ya Kivu Kaskazini) na badaye kwenye jumba la wafaransa.

Mikononi mwao walikuwa na bendera ya Ufaransa ambayo badaye waliichoma moto mbele ya jumla la wafaransa.

Kwa mjibu wa Espoir Aspirine mwanaharakati katika vuguvugu la Lucha, ( vita kwa ajili ya mabadiliko), ziara ya rais wa Ufaransa ni ” tishio kubwa kwa DRC ambayo inakabiliwa na uvamizi wa Rwanda”.

” Hatukubaliani na ujio wake sababu Ufaransa ni nchi hatari. Mnafahamu inachofanya Ufaransa nchini Mali na kwingine. Inaweza kuwa zamu ya DRC. Tunasisitiza : hapana na hapana ziara ya Macron nchini RDC “, alisisitiza Espoir Aspirine.

Kulingana na Aristote Amani wa Véranda Mutsanga , lengo la Emmanuel Macron ni moja : kukamilisha mpango wa kugawanya nchi ya Kongo.

” Kila mtu anataka kuwa na madini ya Coltan, dhahabu, shaaba na utajiri mwingine wa DRC. Kugawanya Kongo ni mpango wa jamii ya kimataifa. Macron pia anajumuika katika mpango huo sababu anajaribu kutafuta mbinu za kuwakubalisha viongozi wa Kongo. Hatutakubali kamwe nchi yetu imeguliwe ” alisisitiza.

Kuhusu swala la usalama unaoendelea kuwa mbaya katika mkoa wa Kivu kaskazini, wandamanaji hao waliomba viongozi wa Kongo ” kuchukuwa majukumu yao na kumaliza tatizo la usalama mdogo “.

” Hayo yote ni madhara ya vita ambayo tulilazimishwa na Rwanda pamoja na nchi zingine za ukanda huu. Ma mia ya raia wa Kongo walipoteza maisha katika maovu hayo. Viongozi wa Kongo wanatakiwa kuchukuwa majukumu yao na kumaliza vita katika eneo hilo la mashariki mwa RDC . Na kama ni swali la kushinda vita, tuko tayari hata kuingia hadi nchini Rwanda kwa ajili ya kupambana vita vikali dhidi ya Kagame”, alieleza Héritier Nyamwami mmoja kati ya walioandaa mandamano hayo.

Rais wa Ufaransa aliandaa ziara rasmi katika nchi nyingi za Afrika ya kati ikiwemo DRC na Rwanda.

Wanaharakati watofautiana kuhusu ziara ya Emmanuel Macron nchini DRC

Mandamano dhidi ya ziara ya rais wa Ufaransa nchini DRC yaliyoandaliwa alhamisi hii hayakuwa makubwa.

Viongozi wakubwa ya vuguvugu la wananchi hawakuonekana. Kati yao ni Sankara Bin Kartumwa.

Mjumbe huyo wa Lucha katika mji wa Goma ameona kuwa hakuna sababu kwa raia wa Kongo kufunga barabara na kususia nchi iliyosaidia kuondoa vikwazo kuhusu kuingiza silaha nchini DRC.

” Baadhi yetu wanafikiria kuwa ni bora kufunga barabara dhidi ya Emmanuel Macron sababu anatoa ufadhiri kwa nchi iliyotuvamia. Sisi tuko katika wale wanaosema kuwa hiyo haiwezekani kwa sababu kama vikwazo vilivyoikabili nchi yetu viliondolewa, basi, Ufaransa ilikuwa na jukumu kubwa katika kulinda maslahi ya DRC. Lakini tunaendelea kudai kuwa kumuzuia Emmanuel Macron kuingia nchini Kongo, ni kama kuunga mkono ubovu wote wa serikali ya Félix ” alizidi kueleza Bwana Kartumwa.

Emmanuel Macron ni kama kipindi joto. Bora ni kushambulia virusi. Virusi yenyewe ni serikali ya Kongo. Ni budi kukumbusha kuwa serikali haikutekeleza ahadi ya kuboresha hali ya raia wa Kongo ambaye ni haki kwao. Viongozi wangetumia ujio wa rais wa Ufaransa ili kutetea haki yao na kumutumia kama balozi wetu kuhusu yote yanayoendelea katika nchi yetu. Tunatakiwa kujadili ushirikiano wenye faida kwa pande zote na Ufaransa” alibaini mwanaharakati huyo wa Lucha.

Rwanda daima ilipinga tuhuma dhidi yake kuwa inaunga mkono kundi la M23. Kundi hilo la zamani la watutsi lilichukuwa tena silaha 2021 likituhumu viongozi wa Kongo kutotekeleza ahadi zake kuhusu kurudisha katika maisha ya kawaida wapiganaji wake. Kundi hilo linadhibiti maeneo mengi katika wilaya tatu za mkoa wa Kivu kaskazini mashariki mwa nchi likiwemo eneo la Bunagana kwenye mpaka na Uganda. Viongozi wa kijeshi katika mkoa huo walitangaza kufunguliwa kwa njia muhimu tatu katika maeneo chini ya udhibiti wa waasi.

” Njia hizo ziko chini ya uangalizi wa waasi. Na kama viongozi wanatangaza kuwa njia hizo zinaweza kutumiwa , bila shaka mazungumzo kati ya FARDC (jeshi la jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo) na waasi yalifanyika ” tathmini hiyo ilitolewa na mwandishi wa habari wa eneo.

Tangu kuibuka tena kwa kundi la M23, viongozi wa Kongo walipinga kuzungumza na kundi hilo ambalo wanalitaja kama ” kundi la kigaidi “.

Previous Gitega: watu 24 watuhumiwa kufanya mapenzi ya watu wa jinsia moja wako jela
Next Rwanda-DRC : Paul Kagame akosoa mandamano dhidi ya Macron