Gitega: watu 24 watuhumiwa kufanya mapenzi ya watu wa jinsia moja wako jela

Gitega: watu 24 watuhumiwa kufanya mapenzi ya watu wa jinsia moja wako jela

Wakiwa wanaume, wanawake na vijana, watu hao 24 wako gerezani tangu februari 23 iliyopita katika jiji kuu la kisiasa la Gitega (kati kati mwa Burundi). Wanatuhumiwa kuunda jenge la wapenzi wa jinsia moja. HABARI SOS Médias Burundi

Wahusika hao walikamatwa na polisi kwa ushirikiano na idara ya ujasusi. Walikuwa wakishiriki katika warsha iliyoandaliwa na shirika moja la ndani maarufu “Muco “. Ni USAID iliyokuwa imetoa ufadhili wa mafunzo hayo kwa mjibu wa vyanzo vyetu.

” Askali polisi wengi na wajumbe wa idara ya ujasusi wakiambatana na viongozi tawala waliingia katika wakati watu hao wakiwa katika mapumziko”, vyanzo vyetu viliripoti.

Wajumbe wa kundi hilo wote walikamatwa papo hapo na kupelekwa katika jela la kamishena ya mkoa katika gari aina ya pick-up ya polisi pamoja na SNR ( idara ya ujasusi), walibaini hayo mashahidi.

Watu hao 24 walituhumiwa kuunda kundi la wapenzi wa jinsia moja.

” Kwenye eneo ambako walikamatwa, tuligundua kondomu nyingi, sindano pamoja na karatasi kuhusu haki na ulinzi wa watu wapenzi wa jinsia moja”, vyanzo vya polisi viliripoti hayo.

Chanzo katika walinda usalama ndani ya jiji la kibiashara la Bujumbura ambapo kuna taasisi nyingi za uongozi wa taifa hilo la Afrika mashariki kimehakikishia SOS Médias Burundi kuwa ” faili hiyo inashughulikiwa na idara ya ujasusi hata kama wafungwa wako mikononi mwa polisi”.

Msemaji wa polisi pamoja na yule wa korti kuu hawakupatikana ili kujibu maswali yetu. Msemaji wa korti kuu Agnès Bangiricenge hakujibu hata ujumbe ambao tumemtumia. Gavana wa mkoa wa Gitega Venant Manirambona hakupatikana kwenye simu yake ya mkoani.

Lakini jumatano hii, rais Evariste Ndayishimiye alizungumzia swala la haki za watu wa mapenzi ya jinsia moja katika nchi yake bila hata hivyo kutaja kesi hiyi ya Gitega.

[…] wapenzi wa jinsia moja wa Burundi hata na wale wanaoishi nje ya nchi, popote wanapoishi, hapa nchini #marekani wanatakiwa kupingwa na kuchukuliwa kama watu wasiofaa , ni watu waliolaaniwa”, alisisitiza katika kikao kilichoandaliwa na bunge.

Hadi disemba 2022, nchi 68 za dunia, zinaadhibu mapenzi ya watu wa jinsia moja. Nchi hizo zinapatikana barani Eshia, Afrika na mashariki ya kati. Angalau 11 kati ya nchi hizo zinashughulikia kosa hilo kwa adhabu ya kifo. Nchini Burundi, kosa hilo linaadhibiwa kwa kifungo cha hadi miaka miwili jela na faini.

Taarifa zinasema kuwa watuhumiwa hao 24 wamepata haki ya utetezi wa kisheria.

Previous Kakuma (Kenya): two Burundian refugees killed
Next Kivu-kaskazini : mandamano dhidi ya ziara ya rais Macron nchini DRC yanafahamisha bila ushawishi mkubwa