Rwanda-DRC : Paul Kagame akosoa mandamano dhidi ya Macron

Rwanda-DRC : Paul Kagame akosoa mandamano dhidi ya Macron

Rais wa Rwanda anaona kuwa mandamano yaliyoandaliwa nchini DRC dhidi ya ziara ya hivi karibuni ya rais wa Ufaransa Emmanuel Macron mjini Kinshasa hayana umuhimu. Anahakikisha pia kuwa Kigali haihusiki kamwe katika mzozo wa Kongo lakini anadai kuwa nchi yake iko tayari kujihami iwapo itavamiwa. HABARI SOS Médias Burundi

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anataraji kufanya ziara ya siku nne barani Afrika ambapo atazuru nchi ya Gabon, Angola, Kongo na RDC ambapo wananchi walianza mandamano dhidi ya ujio wa Macron.

Kulingana na Paul Kagame, mwenendo huo hautakuwa na matunda.

” Ninataka kuwaambia wandamanaji kuwa hawajuwi kinachoendelea au kile wanachopinga. Ziara yenyewe sio tatizo na haingekuwa sababu ya kuitisha mandamano. Ni kama vile mandamano dhidi ya Rwanda, tatizo sio hilo, Rwanda haihusiki”, alisisitiza rais Paul Kagame katika mkutano na wandishi wa habari siku ya jumatano jioni katika mji mkuu Kigali.

” Badala yake, mandamano hayo yangeomba viongozi wao kuwajibika na kuwauliza kwa nini hawajatoa jibu la kudumu la mzozo na kama sio sababu hizo, wanapoteza muda wao au walidanganywa”, alizidi kusema.

Bwana Kagame anapuzia pia tishio la Kongo dhidi ya nchi yake.

Kwa mjibu wa rais wa Rwanda, vitisho vya DRC dhidi ya nchi yake na kuangusha utawala wa Rwanda havina umuhimu.

Alifahamisha kuwa kuna habari kwamba DRC inatafuta uungwaji mkono kutoka kwa nchi marafiki za Afrika ya magharibi kuhusu mpango huo ambao ” hautatekelezeka ” .

” Mbali na sababu zozote za kusambaza vitisho hivyo ndani ya umma, viongozi wa Kongo wana haki hiyo. Lakini hiyo haiwezi kuwa tatizo kubwa kwetu. DRC haiwezi kushawishi kikosi cha jumuiya ya maendeleo ya Afrika magharibi (SADC) kuwaunga mkono katika vita dhidi ya Rwanda, nchi hizo zilikuwa na mpango wa kusaidia kurejesha amani katika eneo hilo la mashariki. Lakini mimi katika kuelewa kwangu, sioni sababu SADC inaweza kuanguka katika mtego huo”, alizidi kusema.

Rais wa Rwanda hata hivyo, alitoa tahadhari kwa makundi yote yenye nia ya kusambaratisha nchi yake

” Aliwahakikishia wananchi wake, vitisho havina msingi na sio sahihi. Kuweni na amani, hali hiyo haistahili kuwavuruga, ninawaomba raia wa Rwanda na wengine wote kufanya shughuli zao za kila siku”, alithibitishia wananchi wake.

” Sisi tunataka amani, hatutaki vita lakini iwapo tutavamiwa, shahuri yake ya yule anatakaye tuanza. Maafisa wa usalama wa Rwanda walijiandaa tangu zamani”, alithibitisha kwa sauti kali.

Uhusiano kati ya Rwanda na Kongo unazidi kuzorota tangu kuibuka kwa kundi la M23. Kundi hilo la waasi la zamani la watutsi lilichukuwa silaha tena mwishoni mwa 2021 likituhumu serikali ya Kongo kutoheshimu ahadi zake kuhusu kuwarejesha katika maisha ya kawaida wapiganaji wake. Viongozi wa Kongo wanadai kuwa kundi hilo hupata usaidizi wa serikali ya Rwanda.

Rwanda upande wake inatuhumu RDC kushirikiana na kundi la FDLR la waliotekeleza mauwaji nchini Rwanda kwa kuwapa sare na silaha na risasi kwa lengo ya kuvuruga ardhi ya Rwanda”. Rais wa Kongo Félix Tshisekedi alitaja kuwa kundi hilo lilidhofika na kugeuka la wezi”, na kwamba haliwezi kuwa tishio kwa Rwanda.

Kwa mara kadhaa, tangu juni 2022, Kigali na Kinshasa zinatuhumiana kuchokozana. Angalau wanajeshi wawili wa Kongo waliuwawa na maafisa wa usalama wa Rwanda wakiwatuhumu kuvuka mpaka kati ya nchi hizo mbili na kuwapiga risasi wananchi na maafisa wa idara ya uhamiaji.

Nchi za ukanda huu zinasumbuka kutafuta maridhiano kati ya nchi hizo mbili za kanda ya maziwa makuu ya afrika na jumuiya ya kiuchumi ya Afrika mashariki na pia katika kutafuta suluhu la kudumu la mzozo wa usalama mashariki mwa nchi hiyo kubwa ya Afrika ya kati tangu miongo mitatu.

Previous Kivu-kaskazini : mandamano dhidi ya ziara ya rais Macron nchini DRC yanafahamisha bila ushawishi mkubwa
Next North Kivu : timid demonstration against President Macron's arrival in the DRC