Burundi-EAC: Joseph Ntakarutimana alichaguliwa kuwa spika wa bunge la EALA

Burundi-EAC: Joseph Ntakarutimana alichaguliwa kuwa spika wa bunge la EALA

Kumuchaguwa mbunge Joseph Ntakarutimana kuwa spika wa bunge la EAC kumeifanya Burundi kuwa nchi muhimu katika maamuzi ya jumuiya hiyo. Burundi kwa sasa inaongoza taasisi tatu muhimu ambazo ni baraza la ma rais, bunge la jumuiya na korti la jumuiya ya Afrika mashariki. HABARI SOS Médias Burundi

Mbunge kutoka Burundi Joseph Ntakarutimana alichaguliwa na wenzake wa jumuiya ya Afrika mashariki kwa 85,7 % ya kura. Uchaguzi huo ulifanyika jumanne hii mjini Arusha Tanzania kwenye makao makuu ya EAC.

Nchi saba zinazounda jumuiya hiyo ya kiuchumi zote zinawakilishwa na wabunge 9 kila moja wanaoshiriki vikao mjini Arusha.Kwa jumla wabunge 63 walishiriki uchaguzi huo, na 54 walimpigia kura mbunge Joseph Ntakarutimana. Anamrejelea mbunge kutoka Rwanda Martin Ngoga kwa muhula wa miaka mitano. Alichukuwa jukumu hilo kuanzia jumanne hii.
Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye alikuwa wa kwanza kumpongeza.

” Ninatuma pongezi zangu kwa mbunge Joseph Ntakarutimana kwa ushindi wake katika uchaguzi wa EALA. Ninawahakikishia sapoti yangu kama mkuu wa baraza la marais wa EAC[…]”.

Joseph Ntakarutimana ni Kabila la Tutsi mwenye asili ya mkoa wa Ngozi kaskazini mwa Burundi. Wanaomfahamu wanasema ni mwanasiasa mkongwe tangu mwaka wa 1993 chini ya chama cha Sahwanya Frodebu kilichopata ushindi katika uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia uliandaliwa na taifa hilo dogo la afrika mashariki. Alijiunga na chama cha CNDD-FDD badaye ambapo alijiona akipewa nyadhifa kubwa kubwa na ni mjumbe wa baraza la wazee wa busara cha chama hicho zamani kundi la waasi wa kihutu.

Kwa sasa ni naibu katibu mkuu wa chama madarakani cha CNDD-FDD.

Nchi yake inashikilia nafasi tatu muhimu ndani ya jumuiya ya afrika mashariki.

Rais wa Burundi mwenyewe anaongoza vikao vya ma rais wa nchi saba wanachama ambazo ni Burundi, Rwanda , Uganda, Tanzanie, Kenya, Sudani ya kusini na jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo aliyoijiunga hivi karibuni.

Taasisi mwingine inayoongozwa na raia kutoka Burundi ni korti kuu ya EAC inayoongozwa na Nestor Kayobera.

Baadhi ya wabunge kutoka Burundi akiwemo Olivier Nkurunziza kiongozi wa chama cha UPRONA chenye msimamo wa karibu na chama tawala, anaridhishwa na kuona nchi yake inakwenda kuongoza bunge la jumuiya ya Afrika mashariki katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Bwana Ntakarutimana alikuwa mgombea peke baada ya muakilishi wa Sudani kusini kujiuzuru na kuunga mkono Burundi.

Joseph Ntakarutimana alikula kiapo jumatatu kama mbunge wa EALA.

Awamu ya tano ya bunge la jumuiya ya afrika mashariki inaundwa na wabunge ambao nchi wanazowakilisha hazina uhusiano mzuri wakati nchi zingine zimemaliza hivi karibuni kujiunga.

Baadhi ya wabunge wa EAC wanatumai kuwa Joseph Ntakarutimana ataweza kumudu matatizo hayo.

Aliyasema pia wakati alipoapishwa na kusisitiza kuwa ” anataka wote waelewane na wawe na mtazamo mmoja na kwamba hapatakuwa tofauti wakati wa mijadara ” na kuzidi kuwa atawajibika kama mpatanishi katika tofauti zote”.

Previous Bujumbura: hali inakuwa ngumu kwa aliyekuwa waziri mkuu Alain Guillaume Bunyoni
Next Ituri/Nord-Kivu: 27 bodies of civilians killed by ADF fighters discovered in Irumu and Beni territories