Nyanza-Lac: katika mkuu wa chama cha CNDD-FDD anatishia kuwauwa baadhi ya wafuasi

Nyanza-Lac: katika mkuu wa chama cha CNDD-FDD anatishia kuwauwa baadhi ya wafuasi

Ijumaa iliyopita, Reverien Ndikuriyo katibu mkuu wa chama cha CNDD-FDD alikuwa ziarani katika tarafa ya Nyanza-Lac mkoa wa Makamba (kusini mwa Burundi). Alitishia kuwauwa wafuasi wa chama wanaosota kidole kasoro za ndani ya tarafa hiyo pamoja na wale wanaunga mkono msimamo wa kumufuta kazi mkuu wa tarafa. Kwa kutoa mfano, alirejelea kisa cha mwanajeshi wa zamani kwa jina la Pascal Ninganza maarufu Kaburimbo aliyeuwawa tarafani Matana (mkoa wa Bururi kusini mwa nchi) katika mwaka wa 2020. Septemba 2019, Reverien Ndikuriyo aliyekuwa spika wa baraza la seneti aliamuru Kaburimbo auwawe. Katika ujumbe wake wa sauti, alikuwa aliahidi kutoa tuzo ya millioni tano (takriban dola 2.500) kwa atakayemumalizia maisha . Vikosi vya ulinzi vilimituhumu mwanajeshi huyo wa zamani kuwapa hifadhi waasi na kutoa mafunzo ya kijeshi kwa ” waasi” katika eneo hilo. Waakazi wanapigwa na mshangao. HABARI SOS Médias Burundi

Tarafa ya Nyanza-Lac inakabiliwa na mzozo wa uongozi kwa miezi kadhaa. Hata hivyo, kauli za mkuu wa chama zinatia hofu kwa mjibu wa Wakaazi.

” Kuliko kuwa kama mpatanishi, badala yake alitishia kuwauwa wafuasi wote wa chama cha CNDD-FDD wanaothubutu kusota kidole kile kinachokwenda vibaya katika tarafa hiyo. Tulitaraji ataongea katika njia ya kupata suluhu na kwa amani, lakini kilichofanyika ni kinyume chake”, mashahidi walielezea.

Kabla ya kuanza hutba yake, Bwana Ndikuriyo aliamuru washirika wote katika mkutano huo kuzima simu zao.

” Zima simu zenu. Hakuna anaye ruhusiwa kurikodi haya. Ambaye atajaribu kurikodi chochote hapa anaweza hata kuuwawa. Tukitaka tunaweza hata kumuuwa yoyote yule anayekuwa na mwenendo mbaye. …hayo ni kati yetu”, alizidi kutishia akijidai kuwa ni yeye alitoa kichwa cha Kaburimbo mwaka wa 2019.

[…], muliwahi kusikia, wakinituhumu daima kumuuwa Kaburimbo. Kosa liko wapi la kuuwawa mtu kama yule. Hata Petero katika biblia alitaka kuuwa mtu kwa ajili ya kimuhami Yesu. Na kwa sasa yeye ndie msingi wa kanisa katoliki. Kwa hiyo kumuondoa muhalifu kwa ajili ya kuwahami wananchi sio dhambi”, alizidi kujitetea katibu mkuu wa chama tawala.

Wafuasi wa chama cha CNDD-FDD waliokuwa ndani ya ukumbi wanasema kushangazwa na kusikia kuwa Reverien Ndikuriyo anatishia wale ambao wanapinga matumizi mabaya ya fuko la tarafa.

” Pasina kupita pembeni, alichukuwa msimamo wa kumuunga mkono Marie Goreth Iradukunda mkuu wa tarafa ya Nyanza-Lac na ofisi yake. Alikiri pia kuwa wale wanaotaka kumuondoa kwenye wadhifa huo Irankunda hawataweza kamwe”, na kulaani walioshiriki kwenye mkutano wa ijumaa iliyopita.

Katika kusisitiza, bwana Ndikuriyo alikumbusha kuwa baadhi ya viongozi wa chama tarafani Nyanza-Lac walifukuzwa na kwamba mkuu wa tarafa aliteuliwa na sheria ya kirais na kwa hiyo ni mtu asiyeguswa.

Wafuasi wasiokuwa wapiganaji wa zamani walilengwa

Na kuzidi kuwa , ” kuna wale wanaotaka kujihusisha na yale yanayofanyika hapa na pale ndani ya nchi hii wakati ambapo hawajuwi tulikotoka. Sisi ni Bagumyabanga (jina la wafuasi wa chama cha CNDD-FDD) wa uhakika. Tulipigwa risasi mahala pote kwenye muili wetu, baadhi kwenye tumbo, zingine kwenye miguu lakini kuwa wale ambao hawajawahi kwenda vitani ambao hawakuwahi kuguswa na madhara ya vita lakini wanataka kujilinganisha na kujifanya wa kwanza kunufaika. Hilo haliwezi kukubaliwa”, ni kumudhulumu aliyekuwa mpiganaji.

Wafuasi wa chama cha CNDD-FDD wanaotaka mkuu wa tarafa na ofisi yake waachishwe kazi, wanadai kuwa Reverien Ndikuriyo “anataka kuwatisha”.

Mwanzoni mwa disemba 2022, baraza la tarafa ya Nyanza-Lac lilimusimamisha mkuu wa tarafa na ofisi yake. Lakini walikataa kutekeleza hatua hiyo. Wajumbe wa baraza la tarafa walimutuhumu matumizi mabaya ya fuko la tarafa na kujikabidhi ardhi za serikali.

Bwana Ndikuriyo anapanga kuendelea na ziara yake katika vijiji vyote vya nchi.

Previous Nyanza-Lac: the CNDD-FDD secretary general threatens to kill some activists
Next Goma: wandishi wa habari kusimamishwa wakati wakiripoti juu ya mandamano dhidi ya kikosi cha EAC