Goma: wandishi wa habari kusimamishwa wakati wakiripoti juu ya mandamano dhidi ya kikosi cha EAC

Goma: wandishi wa habari kusimamishwa wakati wakiripoti juu ya mandamano dhidi ya kikosi cha EAC

Hali ya taharuki imeripotiwa katika mji wa Goma mkoa wa Kivu kaskazini mashariki mwa DRC kufuatia mandamano dhidi ya kikosi cha EAC jumatano hii. Askali polisi pamoja na wanajeshi wametumia nguvu kusimamisha wandishi wa habari waliokuwa wakiripoti juu ya mandamano hayo. Wandamanaji wamejeruhiwa na kupelekwa na polisi. HABARI SOS Médias Burundi

Shughuli zimezorota katika mji huo kufuatia wito wa kufanya mandamano ya amani uliotolewa na muungano wa mashirika ya wazalendo na vuguvugu la kushinikiza ili kikosi cha EAC kiweze kuondoka. Kikosi hicho kinakosolewa kwa kujiweka kati ya jeshi la jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo FARDC na waasi wa kundi la machi 23 ( M23) kuliko kushambulia.

Meya wa mji wa Goma alipiga marufuku mandamano hayo siku moja kabla kupitia tangazo la jumanne hii.

Viongozi wa manispa waliwatolea mwito walioitisha mandamano hayo kujikusanya katika kundi la watu watatu au wanne na kuweka waraka wao kwenye manispa, badala ya kuvuruga usalama wa ummaa kupitia mandamano “.

Mapema asubuhi ya jumatano hii, vikosi cha usalama vimetawanywa katika maeneo nyeti ya mji ili kuzuia na kusambaratisha mandamano.

Kwa mjibu wa mashahidi, askali polisi na wandamanaji wamekabiliana katika baadhi ya maeneo ya jiji.

Vyanzo vyetu vinafahamisha kuwa polisi pamoja na baadhi ya askali jeshi wametumia nguvu, kujeruhi na kukamata wandishi wa habari waliokuwa wakiripoti juu mandamano hayo pamoja pia na wafuasi wa vuguvugu la wazalendo la vita kwa ajili ya mabadiliko (LUCHA).

Wandishi wa habari wawili akiwemo Freddy Rivunangiza wa Prunelle.info wamesimamisha na polisi wakati wakiripoti juu ya mandamano hayo pamoja pia na vijana waliokuwa na nia ya kufikisha wakala wao kwa gavana.

” Mwenzetu Freddy Ruvunangiza aliyekuwa akiripoti juu ya mandamano hayo ya asubuhi kama wandishi wengine mjini Goma amekamatwa na askali polisi. Amepelekwa kwenye kamishena ya polisi kwenye manispa kwa ajili ya kusikiliza baada ya kuburuzwa na kupigwa makosi. Kosa lake la peke, ni kuripoti juu ya mandamano. Tunalaani vikali ukiukwaji huo wa uhuru wa kutoa habari” kimelaani kituo chake cha habari.

Upande wake, shirika la wandishi wa habari waliohatarini (JED), linalaani ” utumiaji huo wa nguvu wa polisi dhidi ya wandishi wa habari wanaofanya kazi yao ya kuripoti juu ya mandamano “.

” Merveille Kiro ( mwandishi wa habari wa kituo cha Blessing FM), Ali Asanka Darius (Mwandishi wa VOA, sauti ya amerika) pamoja pia na Héritier Munyafura( mwandishi wa -AFP), wote wakiwa wandishi wa habari mjini Goma wamejeruhiwa na polisi ya taifa jumatano hii wakati wakiripoti juu ya mandamano yanayodaiwa kuwa ya amani na ambayo yameandaliwa na vuguvugu la wazalendo. Polisi imetumia gesi ya kutoa machozi kusambaratisha wandamanaji waliofika mbele ya ofisi ya gavana. Ni mbele ya ofisi hiyo ambapo wandishi hao watatu wamefuatiliwa wakati wakijaribu kukwepa risasi na kujeruhiwa katika mazingira hayo sababu wakati wakikimbia, wamefuatiliwa na baadhi ya askali polisi ” limeandika shirika la JED.

Pamoja na hayo, mashirika ya kiraia katika kitongoji cha Bwitu ndani ya wilaya ya Rutshuru yanatoa tahadhari kuhusu wapiganaji wa M23 ambao yanasema wanazidi kuongezeka katika maeneo mengi ya Rutshuru.

Kiongozi wa mashirika ya kiraia ya ndani Chirac Mafula anafahamisha kuwa kundi la M23 halikuondoka kutoka maeneo chini ya udhibiti wao Katika wilaya ya Rutshuru kama ilivyotarajiwa kuanzia tarehe 15 januari, sawa na mkataba wa mkutano wa Luanda (Angola) .

” Wapiganaji wa M23 hawakuondoka. Wako katika maeneo ya Kishishe, Bambo, Tongo, maeneo ya karibu ya Kichanga pamoja na maeneo mengine ya miji katika kijiji cha Karibu cha Bwisha. Hawafanyi nenda rudi. Hata hivyo, wanaendelea kuimarisha ngome zao. Kwa hiyo wanaendelea kudanganya jamii ya kimataifa na kitaifa. Hatujuwi lengo lao “, alifahamisha kiongozi wa mashirika ya kiraia ya Bwito.

Viongozi wa nchi za afrika mashariki waliamuru kutuma kikosi cha kikanda katika eneo hilo la nchi hiyo yenye utajiri mkubwa wa madini ya afrika ya kati ili kujaribu kumaliza mzozo huo.

Wanasiasa na wanaharakati wanatuhumu kikosi hicho ” kushirikiana na adui” na wanaomba kifanye mashambulizi hususan eneo la Kivu kaskazini ambapo M23 inadhibiti maeneo mengi tangu juni 2022.

Jumanne hii, mbali na mkutano wa Davos, rais wa Kongo Félix Tshisekedi alifahamisha kuwa M23 bado haijaacha maeneo chini ya udhibiti wake “.

Viongozi wa Kongo bado wanakubaliana kuwa kundi hilo la zamani la watutsi lililochukuwa tena silaha mwisho wa 2021 kwa kutuhumu serikali ya Kongo kutoheshimu ahadi zake za kuwarejesha wapiganaji wake katika maisha ya kawaida linapata usaidizi kutoka Rwanda, jambo ambalo serikali ya Rwanda inatupilia mbali.

Previous Nyanza-Lac: katika mkuu wa chama cha CNDD-FDD anatishia kuwauwa baadhi ya wafuasi
Next Nyarugusu (Tanzania): wasi wasi kufuatia mvutano kati mashirika mawili ya misaada

About author

You might also like

Security

How is the Burundian army, long renowned for its bravery, in decline in North Kivu?

The Burundian army was reformed in 2004, with a new name of the Burundi National Defense Force (FDNB) replacing the old army, Burundian Armed Forces (FAB), which had been created

Justice En

Gitega : cascading transfers of inmates raise concerns

A total of 29 detainees from the central prison of Gitega (political capital) were transferred to the detention houses of Ruyigi (east), Muramvya (center) and Bujumbura (commercial city). They have

Human Rights

Uganda: mahakama ya ICC inathibitisha kifungo cha miaka 25 dhidi ya raia wa Uganda Dominic Ongwen

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC alhamisi hii iliidhinisha adhadu ya kifungo cha miaka 25 jela kwa kosa la uhalifu wa kivita na dhidi ya binadamu wa