Nyarugusu (Tanzania): wasi wasi kufuatia mvutano kati mashirika mawili ya misaada

Nyarugusu (Tanzania): wasi wasi kufuatia mvutano kati mashirika mawili ya misaada

Katika kambi ya Nyarugusu, mashirika mawili ya misaada yanashindana katika sekta ya elimu. Mashirika hayo ni pamoja na “Save the children” na “IRC”. Kama madhara, shule hazikufunguliwa jumatatu hii. HABARI SOS Médias Burundi

Mashirika hayo mawili yanataka kuhudumu katika sekta ya elimu katika kambi za wakimbizi nchini Tanzania.Kawaida shirika la Save the children ndilo linahudumu katika sekta hiyo.

” Kwa wakati huu, mashirika mengine yaliachia nafasi shirika la Danish Refugee Council (RDC), shirika jingine la International Rescue Commitee linataka kupewa nafasi katika sekta ya elimu. Kwa hiyo mvutano unaripotiwa kati ya mashirika hayo mawili ya misaada. Tuna pia hofu kuhusiana na mishahara yetu”. anaeleza mwalimu mmoja katika kambi ya Nyarugusu.

Madhara ya mzozo huo ni shule kutofunguliwa jumatatu hii. Wanafunzi wamefukuzwa bila kuambiwa lini watarudi shuleni.

” Wanafunzi wetu wamekwenda sheleni lakini waalimu hawakuwepo. Waalimu wanaotoka nje ya kambi hawakuruhusiwa kuingia kambini. Kwa hiyo hatungetoa visomo wakati wenzetu wa Tanzania wakiwa wameshinda. Tunaomba swala hilo lijadiliwa kwa ngazi ya juu ili visomo katika awamu ya pili ya mwaka wa shule iweze kuendelea kama kawaida “, waalimu walielezea wakimbizi.

Kwenye kambi ya Nyarugusu, shule tano ziko chini ya uangalizi wa shirika la Save the children tangu miaka 7 iliyopita.

Katika kambi mbali mbali, urasibu wa mashirika ya misaada unahusisha HCR na serikali ya Tanzania. Wazazi wanaomba tatizo hilo liondolewe ili visomo visije kusimama kwa muda mrefu hususan katika darasa za mtihani na zile za kumalizia kidato.

Tatizo hilo linaripotiwa pia katika ya Nduta hata kama visomo bado kusimama.

Kambi hizo mbili zinajumulisha zaidi ya wakimbizi kutoka Burundi laki moja na elfu 26.

Previous Goma: wandishi wa habari kusimamishwa wakati wakiripoti juu ya mandamano dhidi ya kikosi cha EAC
Next Rumonge : the interior minister orders the closure of a dozen bars