Bukinanyana : angalau watu 117 walipatikana na Covid-19

Bukinanyana : angalau watu 117 walipatikana na Covid-19

Janga la Covid-19 linaripotiwa katika tarafa ya Bukinanyana. Ni katika mkoa wa Cibitoke Kaskazini magharibi mwa Burundi. Angalau watu 117 walipatikana na virusi vya Covid-19 tangu mwanzoni mwa wiki hii. Viongozi tawala na wakuu katika sekta ya afya walizindua kampeni kwa ajili ya kudhibiti mambukizi ya ugonjwa huo kwenye vitongoji vyote. HABARI SOS Médias Burundi

Idadi ya wanafunzi wanaopatikana na Covid-19 inazidi kuongezeka kwenye shule ya sekondari ya Butara. Ni wanafunzi 36 kulingana na viongozi wa elimu tarafani Bukinanyana. Shule ya tarafa hiyo upande wake imeorodhesha wagonjwa 9.

Ongezeko la visa vya Covid-19 imeleta wasi wasi mkubwa kwa wazazi hususan kwenye shule ya Butara ambayo ni shule ya mabweni yenye wanafunzi 250.

” Wagonjwa wanapewa matibabu kwenye hospitali ya Ndora na afya yao inazidi kuboreka, anahakikisha daktari mmoja.

Wanafunzi wengine waliosalia katika mabweni wamejawa na wasi wasi.

” Tunahofia mambukizi mengine na hakuna sababu za kutulia kwa sasa”, amehakikisha mwakilishi wa wanafunzi.

Mtetezi mmoja wa haki za binadamu anathibitisha kuwa, mambukizi ya virusi hivyo yanaweza kuchukuwa kasi kubwa kutokana na msongamano wa wanafunzi.

Msimamo ni kama huo kwa mzazi ambaye mtoto wake alipatikana na maradhi hayo. Anaomba mtoto wake apewe ruhsa ya kwenda kuhudumiwa nyumbani akidai kuwa wanafunzi hawapati chakula cha kutosha wakati ambapo wanaumwa.

Hali ya wakaazi wa karibu na shule hiyo pia si nzuri. Angalau 72 kati yao tayari walipimwa na kupatikana na virusi vya Covid-19 wiki hii.

Mikutano ya kuwahamanisha wananchi kuhusu kuheshimu kanuni za usafi na watu kuwa mbali na wengine ilianzishwa katika ngazi zote na viongozi tawala pamoja pia na wadau wa afya.

Mkuu wa tarafa ya Bukinanyana upande wake anahakikisha kuwa ” hali imedhibitiwa”.

Anawatolea mwito viongozi wa chini ” kuzidisha mikutano ya kuwahamasisha raia kuhusu kudhibiti mambukizi ya virusi hivyo.

Kulingana na takwimu za SOSMedias Burundi, angalau watu 296 walipatikana na Covid-19 tangu tarehe 16 januari 2023 nchini kote. Tarafa ya Bukinanyana na shule tatu za mkoa wa Bururi kusini mwa nchi zikiorodhesha visa zaidi.

Tangu kupatikana kwa kisa cha kwanza katika nchi hiyo ndogo ya afrika mashariki machi 2020, angalau watu 23984 walipewa chanjo dhidi ya ugonjwa huo kwa jumla ya wale 50470 waliopatikana na virusi hivyo na 1.866.744 walijipimisha.

Angalau wagonjwa 38 walifariki dunia kufuatia ugonjwa huo kwa mjibu wa ripoti ya kamati ya kitaifa inayohusika na kudhibiti ugonjwa wa Covid-19. Tarehe tano januari, nchi hiyo ndogo ya afrika mashariki iliondoa sharti la kupimwa Covid-19 kwa wasafiri wote na kuifanya nchi hiyo ya Burundi nchi ya mwisho ya jumuiya ya afrika mashariki kusimamisha sharti hilo.

Previous Mukaza : the rag burns between the administrator and the district council
Next Burundi: the company FOMI is still struggling to produce sufficient chemical fertilizers

About author

You might also like

Society

Cibitoke : increase in transport tickets following the hunt for fuel traffickers

Witnesses indicate that transport has become a headache. Basic necessities are on the rise following the measure to suspend illegal fuel trafficking from the DR Congo since Wednesday, July 24.

Society

Kayogoro: a nurse and a microscopist in detention

A microscope from Kayogoro hospital in Makamba province (southern Burundi) was stolen more than a week ago. The police arrested three suspects, including two employees, as part of an investigation.

Health

Muyinga: moshi unaotokana na viripuzi vinavyotumiwa katika migodi ya dhahabu husababisha maradhi ya mapaafu na kifo

Wakaazi wa kijiji cha Kamaramagambo tarafani Butihinda mkoa wa Muyinga (kaskazini mashariki mwa Burundi) wanasema kuwa moshi unaoletwa na viripuzi vinavyotumiwa kuvunja mawe makubwa ndani ya migodi na kusababisha maradhi