Kivu-kaskazini : OCHA yatoa wito, wananchi waepushwe mapigano

Kivu-kaskazini : OCHA yatoa wito, wananchi waepushwe mapigano

Ofisi ya shirika la kuratibu misaada ya kiutu la umoja wa mataifa limetoa tangazo wikendi hii kuhusiana na hali ya kibinadamu Kivu kaskazini (mashariki mwa DRC). Shirika hilo linalaani kuona wananchi wa kawaida wakiteseka kutokana na mapigano kati ya kundi la M23 na FARDC ( jeshi la jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo). Linaomba wananchi waepushwe sawa na sheria za kimataifa. HABARI SOS Médias Burundi

Kupitia tangazo, OCHA imetoa tahadhari kuhusu hali ya maisha ya wakimbizi wa ndani katika maeneo mengi ya Kivu-kaskazini.

[…] wakimbizi wa ndani waliotoroka mapigano kati ya M23 na jeshi wanaishi katika mazingira yasiyofaa kwa binadamu ” yanasomeka ndani ya tangazo hilo.

Shirika hilo linasisitiza kuwa maisha ya watu yako hatarini na kuzidi kuwa ma elfu ya watu walijikuta kati ya mioto ndani ya maeneo ya Kitshanga ( wilaya ya Masisi), na maeneo ya karibu katika mkoa wa Kivu kaskazini na kulazimika kuyatoroka makaazi yao”.

Bruno Lemarquis mratibu wa misaada ya kiutu nchini DRC analaani kuona kuna ma elfu ya wananchi wanaoteseka kutokana na vita mashariki mwa nchi. Anaomba wananchi waepushwe sawa na sheria za kimataifa

Previous Masisi: the M23 progressing towards Sake city
Next Makamba: waziri mkuu atishia kuwafuta kazi au kuwatoa cheo majaji "wanaokula rushwa"