Makamba: waziri mkuu atishia kuwafuta kazi au kuwatoa cheo majaji “wanaokula rushwa”

Makamba: waziri mkuu atishia kuwafuta kazi au kuwatoa cheo majaji “wanaokula rushwa”

Ijumaa iliyopita, waziri mkuu wa Burundi alikuwa ziarani mkoani Makamba (kusini mwa Burundi). Katika mkutano na wananchi, iliripotiwa kuwa vyombo vya sheria mkoani Makamba unasimama vibaya, watu masikini hawawezi kushinda kesi. Visa vya rushwa viliripotiwa hadi ngazi ya juu hususan korti ya rufaa. Gervais Ndirakobuca alitishia kuwafuta kazi majaji ou kuwanyanganya cheo majaji ” wala rushwa”. HABARI SOS Médias Burundi

Kwa mjibu wa mashahidi, mkutano huo ulioongozwa na waziri mkuu ulihudhuriwa na wakaazi wengi. Waliwatuhumu majaji kuegamia upande mmoja na kula rushwa.

” Takriban matatizo yaliyoibuliwa ijumaa hiyo yalihusu kutopata haki, rushwa na matumizi mabaya ya mamlaka”, mashahidi walioshiriki kwenye mkutano huo waliripoti.

Kwa mfano, akinamama wawili walituhumu majaji kukata kesi katika mkasa wa talaka na waume zao wakati ambapo hawakuwahi kusikilizwa.

[…], rais wa nchi alitoa amri kwa mkuu wa mahakama ya mkoa kunipa haki lakini bado hawajafanya hivyo tangu miezi sita iliopota, alilaani mama huyo muathiriwa mbele ya waziri mkuu. Mwezi juni 2022, alikuwa amepeleka mashtaka yake kwa rais Neva alipokuwa ziarani mkoani Makamba.

Mwanamke mwingine alituhumu mkuu wa korti ya rufaa ya kuficha faili yake kwa miezi mingi.

” Alinielekeza mara nyingi Bujumbura na katika korti ya rufaa ya Bururi wakati ambapo faili yangu ilikuwa ndani ya kabati yake. Ni unyama. Badaye alinipa miadi katika siku mbili. Wakati nilipowasili, alinifahamisha kuwa nilishindwa kesi wakati ambapo sikuwahi kuripoti mahakamani. Kesi haikuwahi kusikilizwa. Siwezi kushinda kesi katika mahakama ya rufaa ya mkoa wa Makamba kwa sababu niko masikini” mama huyo alimuambia bwana Ndirakobuca akitokwa na machozi.

Takriban maswala yote yalioibuka yalihusisha visa vya rushwa inayokabili sekta ya sheria mkoani Makamba.

” Hapa kuna madalali wanaohusika na kukusanya rushwa kwa ajili ya baadhi ya majaji. Wanaonekana kila siku katika mahakama na korti mkoani Makamba kama wafanyakazi wa kawaida. Wanaita wenye kuleta mashtaka moja baada ya mwingine na kuwaambia kuwa kama hawakupitia kwao hawawezi kushindwa kesi, alibaini mupeleka mashtaka mmoja.

Gervais Ndirakobuca alilaani yanayotokea katika vyombo vya sheria mkoani Makamba.

“[….], majaji wanaojificha nyuma ya kile kinachofahamika kama uhuru wa majaji, hamuwezi kupata uhuru huo wakati mukiendelea kula rushwa. Majaji kama hao watapelekwa katika korti za chini kuliko kupewa cheo. Wengine watafutwa kazi iwapo hawatajirekebisha, alitishia.

Hivi karibuni, viongozi wa kisheria mkoani Makamba walipewa vyeo licha ya kutowajibika, wanalaani wakaazi wanaodai kuwa ” kama ni mufuasi wa chama cha CNDD-FDD, wanakukingia kifua kwa njia moja ama nyingine.

Previous Kivu-kaskazini : OCHA yatoa wito, wananchi waepushwe mapigano
Next Masisi: kundi la M23 linasonga mbele kuelekea jiji la Sake