Masisi: kundi la M23 linasonga mbele kuelekea jiji la Sake

Masisi: kundi la M23 linasonga mbele kuelekea jiji la Sake

Mapigano makali kati ya FARDC (jeshi la jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo) na kundi la M23 yanaendelea katika wilaya ya Masisi ndani ya mkoa wa Kivu kaskazini mashariki mwa Kongo. Jeshi la FARDC linazidi kupoteza ngome zake za kimkakati na kuchukuliwa na waasi. HABARI SOS Médias Burundi

Jumatatu hii, vijiji viwili vinavyopatikana magharibi ya mji wa Goma (makao makuu ya mkoa wa Kivu kaskazini) vilianguka katika mikono ya M23.

Vijiji vya Kalake na Tuonane kwenye kilometa 7 kutoka jiji la Sake vilianguka katika mikono ya kundi la M23 baada ya mapigano makali yaliojiri alasiri ya jumatatu hii, vyanzo vya ndani vilithibitisha.

Kundi la M23 lilichukuwa udhibiti wa vijiji hivyo viwili kupitia kijiji cha Ruvunda ambacho kinazungukwa na ma zizi ya ng’ombe.

” Tuliwaona waasi wa M23 wakiondoka kwenye ngome zao ndani ya kitongoji cha Kamuronza, alitoa ushahidi huo kwa SOS Médias Burundi mkaazi mmoja jumatatu hii jioni.

Hivi karibuni, kundi la M23 lilichukuwa udhibiti wa jiji la Kitchanga lilolo kwenye umbali wa kilometa 80 kaskazini magharibi ya mji mkuu wa Kivu kaskazini. Jeshi la Kongo linatapa taabu kuwafukuza kutoka jiji hilo la kimkakati.

Hadi sasa, hakuna tamko la FARDC (jeshi la Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo) kuhusu kusonga mbele kwa waasi jumatatu hii.

Mapigano yanaendelea licha ya wito wa ma rais wa nchi wanachama wa jumuiya ya afrika mashariki wa kuacha vurugu na kusitisha vita mara moja, ombi ambalo pia lilitolewa na baba mtakatifu wakati wa ziara yake ya hivi karibuni na ya kwanza nchini DRC na Afrika.

Kupitia tangazo, kundi hilo la zamani ya wa tutsi lililochukuwa silaha mwishoni mwa 2021 likituhumu viongozi wa Kongo kutoheshimu ahadi yake ya kuwarejesha katika maisha ya kawaida wapiganaji wake, hivi karibuni, lilielezea kuwa lilianza mapigano tena kwa ajili ya kuwalinda Watutsi wa Kongo wanaolengwa na mauwaji ya kuangamiza yaliyoandaliwa na serikali ya Kinshasa. Viongozi wa Kongo upande wake, bado wanakubaliana kuwa kundi hilo linapata usaidizi kutoka nchini Rwanda.

Katika tamko la hivi majuzi, jeshi la Kongo lilituhumu Rwanda kuwatuma wanajeshi wake mamluki ambao ndio walichukuwa udhibiti wa Kitchanga. Viongozi wa Kongo wanatuhumu pia Rwanda kuandaa mauwaji ya watutsi wa Kongo ili kupata hoja ya kuelezea sababu za sehemu ya wanajeshi wake kuvamia Kongo “.

Uhusiano kati ya mataifa hayo mawili ya maziwa makuu unazidi kudorora tangu kundi la M23 kuibuka tena. Rwanda upande wake inatuhumu serikali ya Kongo kushirikiana na kundi la FDLR la waliotekekeza mauwaji ya halaiki nchini Rwanda kwa kuwapa silaha, risasi na sare za jeshi kwa lengo la kusambaratisha utawala wa Rwanda”.

Hali mashariki mwa nchi hiyo kubwa ya afrika ya kati inaendelea kuwa mbaya zaidi licha ya uwepo wa kikosi cha kikanda pamoja na Monusco (ujumbe wa umoja wa mataifa nchini DRC). Vikosi hivyo vinakosolewa na sehemu ya mashirika ya kiraia, wanasiasa pamoja na makundi ya shinikizo kwa kile yanasema kutowajibika na washirika kwa sababu ya kutoshambulia kundi la M23. Jumatatu hii yaliandaa mandamano katika mkoa wa Kivu kaskazini kwa ajili ya kuonyesha upinzani wao dhidi ya kikosi cha EAC na Monusco ambavyo mashirika hayo yanadai ni kama ” watazamaji na wa scouts” wanaoangalia tu.

” Haileweki, iwapo M23 imeamuru kuchukuwa eneo, wanamaliza kwa kuwafurusha FARDC ” ametoa tathmini hiyo muangalizi mmoja wa mzozo wa Kongo ambaye anadai kuwa lengo kubwa la waasi ni kukata mawasiliano ya mji wa Goma na maeneo mengine.

Kundi hilo la waasi linadhibiti maeneo mengi ya mkoa wa Kivu kaskazini tangu mwishoni mwa juni 2022 likiwemo eneo la Bunagana, jiji la mpakani na Uganda.

Previous Makamba: waziri mkuu atishia kuwafuta kazi au kuwatoa cheo majaji "wanaokula rushwa"
Next Nakivale (Uganda): Uganda to collect tax in the refugee camp