Nyabihanga : Imbonerakure wawili gerezani

Nyabihanga : Imbonerakure wawili gerezani

Emmanuel Ndimurirwo na César Sinduhijimana wanazuwiliwa katika gereza la kamishena ya polisi ya mkoa wa Mwaro (kati kati mwa Burundi) tangu jumatano wiki iliyopita. Wawili hao ni wenye asili ya tarafa ya Nyabihanga (katika mkoa huo huo), wanatuhumiwa wizi na unyanyasaji. HABARI SOS Médias Burundi

Ni Emmanuel Ndimurirwo maarufu l’homme ambaye huenda alibaka mtoto wa kike mkaazi wa kijiji cha Miterama tarafa ya Nyabihanga. Kwa mjibu wa vyanzo eneo, hali ilikwenda vibaya baada ya ukatili huo.

Baada ya siku kadhaa, mtuhumiwa huyo wa ubakaji alijikuta akiwa hana tena nguvu ya kufanya kitendo cha ndoa na mke wake, vyanzo vya karibu na faili hiyo vinadai ni kutokana na ” uchawi”.

Alitafuta uungwaji mkono kutoka kwa afisa wa idara ya ujasusi tarafani Nyabihanga pamoja na César Sinduhijimana ambaye ni kiongozi wa tawi la Imbonerakure wafuasi wa chama cha CNDD-FDD.

” Malengo yake ilikuwa kumutisha mtoto huyo wa kike ili amutibu Emmanuel”, kwa mjibu wa vyanzo vyetu.

” Wanaume hao walimutishia wakiwa na visu mkononi, na mtoto huyo wa kike akakubali kulala mara mbili na Emmanuel “.

Wazazi wa mtoto huyo walitoa mashtaka na wanaume hao wote watatu walikamatwa na kupelekwa kwenye kamishena ya polisi ya Mwaro.

Mkuu wa idara ya ujasusi wa Mwaro aliachiwa huru siku chache badaye.

Emmanuel Ndimurirwo ni mwalimu. César Sinduhijimana yeye ni kiongozi wa shule ya msingi.

Familia ya muhanga inaomba ” mtoto wao apewe ulinzi”. Familia hiyo inaomba uchunguzi huru ufanyike.

Kisa ambapo kinafanya wanaume hao wawili kufuatiliwa, kilifanyika wiki mbili zilizopita.

Previous Tanzania : HCR yaimarisha kampeni yake ya kuwasihi wakimbizi wa Burundi kurejea makwao
Next Busoni: one dead and over a hundred people poisoned