Tanzania : HCR yaimarisha kampeni yake ya kuwasihi wakimbizi wa Burundi kurejea makwao

Tanzania : HCR yaimarisha kampeni yake ya kuwasihi wakimbizi wa Burundi kurejea makwao

Kamishena mkuu wa shirika la umoja wa mataifa la wakimbizi Filippo Grandi alikuwa ziarani nchini Tanzania. Alisisitiza juu ya kurejea makwao ” kwa hiari ” kwa wakimbizi wa Burundi nchini Tanzania. Wakimbizi hao wanahofia kuchuliwa hatua madhibuti kwa ajili ya kuwalazimisha kurudi makwao. HABARI SOS Médias Burundi

ijumaa, mkuu huyo wa HCR alipokelewa kwa mazungumzo na rais wa Tanzania. Swala la wakimbizi wa Burundi lilikuwa kwenye agenda.

” Nilizungumza na rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuhusu njia ya kuimarisha mpango wa kuwarejea nchini na kwa hiari wakimbizi kutoka Burundi. Juhudi zenye nia ya kuandaa mazingira mazuri kwa ajili ya kurejesha makwao wakimbizi zinatakiwa kuongezeka na zinahitaji utashi wa wadau wote hususan wadau wa maendeleo” alibaini Filippo Grandi.

Kabla ya kuelekea nchini Tanzania, mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya juu alipita nchini Burundi siku ya alhamisi. Rais Evariste Ndayishimiye alimpokea kwa mazungumzo.

” Walizungumzia hasa kuhusu kazi inayotakiwa kufanyika kwa ajili ya kuwawezesha waliorejea nchini kujichanganya na raia wengine, ikizingatiwa kuwa wanaendelea kurudi katika nchi yao kwa wingi”, alisisitiza rais wa Burundi.

Kamishna mkuu wa shirika hilo la umoja wa mataifa upande wake alisema kuridhishwa na hali ya usalama nchini Burundi.

” Nilipokelewa na rais Ndayishimiye miaka miwili baada ya ziara yangu ya mwisho nchini Burundi kwa lengo la kustawisha nchi. Tuliangazia umuhimu wa kuunga mkono mchakato wa kuwasaidia waliorejea nchini kujichanganya na raia wengine wa Burundi na kuimarisha kwa mara nyingine mapokezi ya wakimbizi kutoka Kongo” , alibaini.

Wasiwasi wa wakimbizi kutoka Burundi nchini Tanzania ambao hawajakuwa tayari kurejea nchini kwa hiari.

” Tunajuwa kuona dalili zisizodanganya ” alijibu raia wa Burundi ambaye yuko ukimbizi kwa mara ya tatu katika kambi ya Nyarugusu.

Raia huyo wa Burundi ana kumbukumbu mbaya.

” Mwaka 2013, nilikuwa katika kambi ya Mtabila hapa nchini Tanzania. Kabla ya kubomoa kambi hiyo, visa vinavyofanana na hivi vilitokea : ziara za mara kwa mara za viongozi wa HCR na viongozi wa Burundi ndani ya kambi. Jumbe nyingi za Go and see, go and come to tell” kama ilivyo kwa wakati huu, wito kwa ajili ya kurejea nchini kwa hiari, hatua kali na mazingira mabaya ya maisha…..” anakumbuka.

Na kuzidi kusema : ” baada ya kuona kuwa tumepinga, siku moja asubuhi, kambi ya Mtabila ilibomolewa, tukapelekwa ndani ya ma lori kwa nguvu. Vifo vilitokea. Hatari ya kutokea tena hali kama hiyo ni kubwa. Sijakuwa mtu wa kukatisha tamaa lakini ninahisi” alifafanua mkimbizi huyo mwenye umri wa takriban miaka 50.

Katika duru yake ndani ya kambi za wakimbizi kwa kipindi cha wiki mbili, muakilishi mkaazi wa HCR nchini Tanzania Mahoua Parums alithibitisha kuwa swala la wakimbizi wa Burundi linatakiwa kupewa jibu la kudumu. Kurejea “kwa hiari ” ndio njia inayopewa kipau mbele.

Tanzania inawapa hifadhi zaidi wa wakimbizi laki 2 elfu 47 wakiwemo warundi laki moja na elfu 45.

Previous Kivu-kaskazini : Hali ya utulivu inaripotiwa eneo la Sake baada ya siku ya hofu
Next Nyabihanga : Imbonerakure wawili gerezani