Kivu-kaskazini : Hali ya utulivu inaripotiwa eneo la Sake baada ya siku ya hofu

Kivu-kaskazini : Hali ya utulivu inaripotiwa eneo la Sake baada ya siku ya hofu

Mapigano kati ya jeshi la jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo na waasi wa M23 katika jiji la Sake ndani ya wilaya ya Masisi mkoa wa Kivu kaskazini (mashariki mwa DRC) yalisababisha hofu alhamisi hii. Tangu ijumaa hii hali ilirudi kuwa ya kawaida. Wananchi waliokuwa wametoroka makaazi yao walianza kurejea katika kata zao huku shughuli zikianza pole pole. HABARI SOS Médias Burundi

Kulingana na mashirika ya kiraia ya ndani, usalama uliimarishwa. Nduwayo, ripota wa shirika la kiraia eneo la Sake alifahamisha kuwa wananchi walianza kurejea katika jiji la Sake alhamisi jioni. Idadi ya wanajeshi pia iliongezwa.

” Tangu jana jioni wakaazi wanaendelea kurejea na wengi wao ni wale waliokuwa wamekimbia kuelekea Shasha na Minova na wilaya ya Kalehe ndani ya mkoa jirani wa Kivu kusini. Hakika , kuna nenda rudi ya wananchi hapa sake lakini shughuli zinaanza pole pole” alihakikisha mwanaharakati huyo wa shirika la kiraia eneo la Sake.

Anazidi kuwa mapigano kati ya jeshi la taifa na waasi wa M23 yalifanyika kwenye umbali wa kilometa 8 kutoka Sake.

” FARDC wako kwenye mapigano dhidi ya waasi wa M23 eneo la Karenga ni kwenye umbali wa kilometa 8 kutoka hapa. Tuna imani kwa wanajeshi wetu ma shujaa ambao hadi sasa wanatuhakikishia kuwa wana mpango wa kurejesha udhibiti wa maeneo yaliyochukuliwa na adui tangu muda mrefu ” wanasema hayo viongozi tawala wa ndani.

Na kuzidi kusema : ” Tunaomba wananchi kuwa tulivu na kuwaamini wanajeshi wa FARDC. Tujizuie pia kusambaza uvumi kwa sababu hali hiyo inaweza kututumbukiza katika hali mbaya”.

Kauli ni kama hiyo katika jeshi. Msemaji wake anawatolea mwito wananchi kuwa watulivu na kuwaamini wajumbe wa taasisi za usalama.

” Tunawathibitishia wananchi kuwa jeshi la FARDC liko kwenye mapambano na lengo letu ni kumuondoa aduwi na kumurudisha pale alipotoka. Jeshi letu linasalia kuwa jeshi linalowalinda wananchi “, anahakikisha luteni kanali Guillaume Ndjike Kaiko msemaji wa jeshi la jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo ndani ya mkoa wa Kivu kaskazini.

Alhamisi jiji hilo la Sake lilishuhudia mapigano na kusababisha wakaazi kutoroka.

Watu walianza kukimbia asubuhi kutokana na mapigano makali kati ya FARDC na waasi wa M23 eneo hilo.

Uongozi wa FARDC katika mkoa wa Kivu kaskazini uliimarisha jeshi ndani ya eneo hilo ili kuwahakikishia wananchi utashi wa jeshi la ulinzi kushinda kundi la M23.

Baadhi ya wananchi katika kitongoji cha Mubambiro kilometa mbili karibu na Sake wanasema kujawa wa hofu. Licha ya hali kutulia, wakaazi wanasema kutoelewa kinachoendelea.

” Tuna majeshi wa FARDC mashujaa ambao ni jukumu lao kutulinda na mipaka ya nchi lakini hatuelewi kwa nini adua anasalia katika hali ya ushindi dhidi ya jeshi, hali hiyo inaweka pabaya. Tunaomba juhudi zote zifanyike ili kukimbiza waasi wa M23″, wanalalamika wakaazi wa Kongo eneo la Sake waliozungumza na SOS Médias Burundi

Previous Tanzania : HCR yaahidi kuendelea kuwasaidia wakimbizi
Next Tanzania : HCR yaimarisha kampeni yake ya kuwasihi wakimbizi wa Burundi kurejea makwao