Tanzania : HCR yaahidi kuendelea kuwasaidia wakimbizi

Tanzania : HCR yaahidi kuendelea kuwasaidia wakimbizi

Muakilishi mkaazi wa HCR nchini Tanzania amekuwa ziarani ndani ya kambi za wakimbizi. Aliwatuliza nyoyo wakimbizi kuwa katika mwaka 2023, shirika hilo la umoja wa mataifa, litaendelea kuwasikiliza. Katika kambi za Nyarugusuru na Nduta, Mahoua Parums alipokelewa na wakimbizi kwa kumuambia mapendekezo yao ili waweze kupata mazingira mazuri katika maisha ya wakimbizi. Wakimbizi hao wana matumaini kuwa muwakilishi mpya wa HCR atapatia suluhu mapendekezo yao. HABARI SOS Médias Burundi

Mahoua alianza ziara yake katika kambi ya Nduta inayowapa hifadhi warundi na raia wa Kongo. Alikariri uamzi wa shirika hilo wa kuendelea kusaidia wakimbizi.

” Nilifanya mazungumzo mazuri na viongozi wa kambi, wawakilishi wa wakimbizi, wadau wengine pamoja pia na wakimbizi kuhusu ulinzi wao, uwezo wa kuishi, nishati na kuhusu changamoto zinazowakabili kwenye ardhi hiyo ya ukimbizini”, alifahamisha.

Viongozi wa kijamii wa wakimbizi walirejelea kwa mara kadhaa matatizo yanayowakabili.

” Mapendekezo yetu yamekuwa kama nyimbo, tunakariri kitu kimoja: usalama mdogo, kiwango kidogo cha chakula, watu kusimamishwa kiholela, na kurejeshwa nyumbani kwa nguvu. Pamoja na hayo, kuna pia marufuku ya beskeli na pikipiki, kutuzuia kufanya biashara yoyote na kuendesha kilimo”, wanasema wakimbizi ambao waliridhishwa na kuwasilisha matatizo yao kwa mara ya kwanza kwa muwakilishi mpya wa HCR nchini Tanzania.

Matokeo ya kuridhisha mwaka 2022……

Kazi iliyofanyika mwaka wa 2022 imepongezwa na HCR.

” Ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilometa 25, nyumba zaidi ya 3860 zilijengwa au kukarabatiwa, madarasa 8 yalijengwa, zaidi ya wakimbizi 6800 walipewa msaada wa kuni, kurejesha wakimbizi wa hiari yao, na huduma bora za afya kutolewa,…..anapongeza Bi Mahoua.

HCR ilifanya makubaliano na zaidi ya wakimbizi 247.000 idadi kubwa wakiwa raia wa Burundi na Kongo wanaosalia ukimbizini.

“HCR inafanya kazi na serikali pamoja pia na washirika wake ili kuhakikisha usalama wa wakimbizi. Kama ilivyokuwa 2022, tutaendelea kuwahudumia : nyumba, barabara, vyakula na vitu vingine, elimu, maji safi, usanifishaji, kuwarejesha nyumbani kwa hiari, kutoa fursa za kuwapeleka kwingine pamoja pia na huduma za afya, alitaja mwakilishi huyo.

Ahadi hizo zilichukuliwa kwa umakini na wahusika ndani ya kambi ya Nyarugusu. Walionekana kupoteza matumaini.

” Acha tusubiri kuona iwapo ahadi hizo zinatekelezwa. Hata na watangulizi wao, walikuwa na kauli nzuri lakini lilipofikia swali la kutetea mkimbizi wa Burundi aliyekamatwa kinyume cha sheria au kupotea, hatukuwahi kusikia sauti yao” walibaini wakimbizi.

Kutafuta suluhu la kudumu

HCR iliwaelezea wakimbizi kuwa inatafuta pole pole suhulu la kudumu kuhusu hadhi ya ukimbizi.

Ndani ya kambi ya Nduta, ujumbe ulipokelewa kwa njia tofauti.

” Hakika, ni njia nyingine ya kutuarifu kuwa ni lazima turudi nchini kwetu. Sababu alituambia kuwa suluhu inaomba idadi kubwa ya wakimbizi kuitikia mpango wa kurejea kwa hiari, kuwa idadi ndogo itapata uraia na kwamba wengine watapelekwa katika nchi zingine. Suluhu hizo mbili za mwisho hazikupewa kipau mbele, walibaini wakimbizi.

Huenda rais wa sasa wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akabadili msimamo lakini mtangulizi wake, John Pombe Magufuri katika mwaka wa 2018 alisema kuwa swala la kuwapa uraia wakimbizi wa Burundi lilisimama baada ya kuulizwa na hayati Pierre Nkurunziza rais wa Burundi. Ma rais hao wawili walifariki dunia miaka miwili baada ya matamshi hayo.

HCR pia haikuacha kusema kuwa inakabiliwa na ukosefu wa uwezo wa kifedha.

“‘Wahisani wengi walielekeza macho yao kwenye mzozo kati ya Urusi na Ukraine pamoja na janga la Covid-19 hali ambayo ilipelekea kusahawu tatizo la wakimbizi barani afrika. Tunaomba washirika wa UN kuzingatia mapendekezo yetu na hivyo kukidhi mahitaji ya wananchi hao ambao hawana makaazi” alitoa wito huo muakilishi wa HCR nchini Tanzania.

Tanzanie peke yake inawahifadhi wakimbizi zaidi ya laki moja na elfu 45 kutoka Burundi kwa mkibu wa HCR.

Previous Tanzania: UNHCR steps up its campaign for the return of Burundian refugees
Next Kivu-kaskazini : Hali ya utulivu inaripotiwa eneo la Sake baada ya siku ya hofu