Burundi : viongozi wanahakikisha kukamatwa kwa mwanaharakati mwingine na kumuweka gerezani huku timu yote ikituhumiwa kufadhili ugaidi

Burundi : viongozi wanahakikisha kukamatwa kwa mwanaharakati mwingine na kumuweka gerezani huku timu yote ikituhumiwa kufadhili ugaidi

Waziri anayehusika na mambo ya ndani na usalama alihakikisha rasmi kukamatwa kwa mjumbe mwingine a wa mashirika. Jina lake ni Prosper Runyange anayehusika na maswala ya ardhi katika shirika la APDH (shirika kwa ajili ya amani na kuendeleza haki za binadamu). Mjumbe huyo aliongeza idadi ya wengine wanne waliokamatwa wakiwa kwenye uwanja wa ndege wa Bujumbura tarehe 14 februari. Wote watamaliza usiku wa pili gerezani kulingana na vyanzo vya usalama na kutoka idara ya magereza. HABARI SOS Médias Burundi

Watetezi wote watano wanazuiliwa katika gereza kuu la Bujumbura maarufu Mpimba tangu alhamisi hii, vyanzo vingi katika jiji la kibiashara vimearifu SOS Médias Burundi.

Matamshi ya viongozi tawala wa Burundi

Waziri wa Burundi wa mambo ya ndani na usalama alitangaza sababu zilizopelekea watetezi hao wa haki za binadamu kukamatwa.

[…], wanafanya kazi kwa ushirikiano na shirika lililojiondoa nchini Burundi katika utawala wa 2015-2020, lakini kwa bahati mbaya, shirika hilo liliendelea kufanya kazi na mashirika ya kiraia yaliodhinishwa na ambayo hayakufanya hivyo nchini Burundi”, alifahamisha waziri Niteretse.

Ufadhili wa kutatanisha

Kwa mjibu wa Martin Niteretse, shirika hilo la kigeni hutoa ufadhili kwa mashirika hayo katika njia usiokuwa rasmi.

” Ripoti zinazotungwa na mashirika hayo na kutumwa katika wizara ya mambo ya ndani, maendeleo ya umaa na usalama wa wananchi hazijaonyesha ufadhili huo. Kwa hiyo,tulifanya uchunguzi pole pole miezi mitatu iliyopita na kugundua kuwa mashirika hayo baadhi yakiwa waliidhinishwa na mengine yakiwa bado yanashirikiana na shirika hilo la kigeni”alizidi kusema afisa huyo wa Burundi anayezidi kusema kuwa watu hao wanne walikamatwa kwenye uwanja wa ndege wa Bujumbura wakati wakielekea katika mkutano ulioandaliwa na shirika hilo kwa lengo la kuteuwa kamati tendaji”.

Ugaidi

” Matokeo tulionayo kwa sasa, yanaonyesha kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kufadhili ugaidi kupitia pesa hiyo. Tunakatiwa kuwa makini katika sekta zote ili pasiwepo chochote kinachoweza kuvuruga amani na utengamano wa umma”, alimalizia.

Visa vya ugaidi huadhibiwa na kifungo cha miaka kati ya kumi ishirini jela na faini ya franka za Burundi kati ya laki mbili na milioni moja kulingana sheria ya makosa ya jinai nchini Burundi. Wakati kitendo cha ugaidi kimesababisha kifo cha mtu mmoja au watu wengi, muhusika anachukuliwa adhabu ya kifungo cha maisha jela.

Tangu rais Ndayishimiye alipofika kwenye utawala katika mwezi juni 2020, wanaharakati watatu akiwemo mmoja aliyekamatwa baada ya kiapo chake, waliachiliwa. Kabla ya watetezi hao watano wa haki za binadamu kukamatwa, hakuna mwanaharakati hata mmoja aliyekuwa jela katika taifa hilo la Afrika mashariki.

Mwendeshamashtaka mkuu wa jamuhuri hakutaka kujibu maswala yetu licha ya kupokea ujumbe na kuusoma.

Previous Goma: mwandishi wa habari azuiliwa na idara ya ujasusi
Next Goma: mwandishi wa habari Jimmy Shukrani Bakomera aachiliwa huru