Goma: mwandishi wa habari Jimmy Shukrani Bakomera aachiliwa huru

Goma: mwandishi wa habari Jimmy Shukrani Bakomera aachiliwa huru

Mwenzetu huyo amechikiwa huru ijumaa hii asubuhi. Alikuwa katika gereza la ANR ( idara ya ujasusi ya Kongo) katika mji wa Goma (makao makuu ya mkoa wa Kivu kaskazini) tangu alhamisi mchana. Alituhumiwa “kushirikiana na kundi la M23”, kundi linalochukuliwa na viongozi wa Kongo kama kundi la “kigaidi “. HABARI SOS Médias Burundi

Jimmy Shukrani Bakomera aliambia SOS Médias Burundi kuwa ” nimeachiwa huru na niko salama na mzima, hakuna aliyeninyanyasa”.

Mwandishi huyo na ripota wa VOA( Sauti ya Amerika) alihojiwa kuhusu tuhuma dhidi yake za kushirikiana na wajumbe na watu wa karibu na kundi la M23.

” Niliulizwa kuhusu M23. Walinionyesha orodha ya wajumbe wa kundi la M23 wengi wao wakiwa raia wa Kongo. Niliwaambia kuwa sifahamu hata mmoja”, ametoa ushuhuda huo.

Ni afisa wa idara ya ujasusi ndani ya Masisi aliyesimamisha mwandishi huyo katika eneo la Karuba. Alimutuhumu kushirikiana na kundi la M23 baada ya kumukutaakifanya mahojiano na jamii ya wanaotumia lugha ya Kinyarwanda wanaoishi nchi DRC. Alikuwa akifanya ripoti kuhusu zoezi la kuorodhesha wapiga kura linalokosolewa na mashirika ya kiraia ndani ya mkoa wa Kivu-kaskazini kutokana na usalama mdogo unaoripotiwa mashariki mwa Kongo.

” Watu wanaotumia lugha ya Kinyarwanda wana haki ya kujieleza na hawatakiwi kufananishwa na washirika wa kundi la M23 na madawi wa nchi” anadai mwandishi huyo.

” Ninawashukuru wandishi wa habari na wanaharakati pamoja na watu wengine waliochangia ili niweze kuachiliwa huru”, amebaini Jimmy Shukrani Bakomera.

Tangu kuibuka tena kwa kundi la M23, wananchi wanaotumia lugha ya Kinyarwanda ambao wanaishi nchini DRC wanatuhumiwa kusaidia waasi na kufanya upelelezi kwa ajili ya Rwanda.

Kundi hilo la zamani la watutsi lililochukuwa silaha mwishoni mwa 2021 likituhumu viongozi wa Kongo kutoheshimu ahadi yake kuhusu kuwarudisha katika maisha ya kiraia wapiganaji wake, lilichukuwa udhibiti wa maeneo mengi ya Kivu kaskazini likiwemo eneo la Bunagana, jiji la mpakani na Uganda tangu mwishoni mwa juni 2022.

Viongozi wa Kongo bado wanakubaliana kuwa kundi hilo linapata usaidizi kutoka Rwanda jambo ambalo Rwanda inapinga kila siku.

Previous Burundi : viongozi wanahakikisha kukamatwa kwa mwanaharakati mwingine na kumuweka gerezani huku timu yote ikituhumiwa kufadhili ugaidi
Next Rwanda-DRC : jeshi la Kongo lapinga kuchokoza lile la Rwanda