Rwanda-DRC : jeshi la Kongo lapinga kuchokoza lile la Rwanda

Rwanda-DRC : jeshi la Kongo lapinga kuchokoza lile la Rwanda

Alhamisi hii, viongozi wa jeshi la Kongo eneo la Bukavu katika mkoa wa Kivu kusini (mashariki mwa DRC) walijieleza kuhusu kisa kilichoripotiwa na Rwanda siku moja kabla. Rwanda ilidai kuwa wanajeshi wa Konho walivuka na kuingia katika eneo la mpakani la kati kati. FARDC upande wake inasema waliohusika na kitendo hicho ni genge la raia wa Kongo waliokuwa kinyume cha sheria. Jeshi la Kongo ambalo linasikitika kwa kupoteza mwanajeshi wake, linasema mmoja kati ya majambazi wanne aliuwawa, na wanne wengine walikamatwa pamoja na silaha na risasi vilikamatwa pia. HABARI SOS Médias Burundi

Ni jemedali Yav Avul Ngola Robert kamanda wa kikosi cha 33 aliyejieleza kupitia tangazo.

” Jeshi la FARDC lilishituka liliposikia taarifa kuwa ardhi ya Rwanda ililengwa na shambulio kutoka kwa wanajeshi wetu”, alisema kwa kushangaa na kutuhumu Rwanda kulichukuwa tukio hilo na kulitumia kwa lengo la udanganyifu” kwa ajili ya kusambaratisha mkoa wa mkoa wa Kivu- kusini kama inavyofanya ndani ya mkoa wa Kivu kaskazini”.

Kupitia tangazo hilo, jeshi la Kongo linafahamisha kuwa kundi la raia wa Kongo waliokuwa kinyume cha sheria walishambulia ngome mmoja katika zile zinazopatikana eneo la Rusizi II. Tangazo hilo linaeleza zaidi na kuhusu matokeo.

” Upande wa genge hilo, mtu mmoja alifariki na wawili wengine kujeruhiwa, wanne walikamatwa na silaha aina ya AK-47, na risasi kukamatwa” , yanasomeka ndani ya tangazo hilo.

Maelezo hayo yalitolewa baada ya Kigali kutangaza kuwa jeshi lake lilirudisha nyuma uvamizi wa jeshi la Kongo jumatano alfajiri. Kisa hicho kilitokea kati ya kanda ya Rusizi ndani ya mkoa wa magharibi mwa Rwanda na mkoa wa Kivu kusini mashariki mwa Kongo , kulingana na tangazo la jeshi la Rwanda.

Si kwa mara ya kwanza nchi hizo jirani zikituhumiana visa vya uchokozi.

Mwezi novemba na juni 2022, wanajeshi wawili wa Kongo waliuwawa na jeshi la Rwanda. Visa hivyo viwili vilitokea katika maeneo ya mpakani maarufu “Petite Bariere “. Ni kati ya kanda ya Rubavu ( magharibi mwa Rwanda) na mjini wa Goma (makao makuu ya Kivu kaskazini) mashariki mwa DRC. Na hivi karibuni, jeshi la Rwanda lilishambulia ndege ya kivita ya Kongo iliyokuwa imevuka na kuingia katika anga ya Rwanda kwa mjibu wa viongozi wa Rwanda. Serikali ya Kongo ilipinga madai hayo.

Previous Goma: mwandishi wa habari Jimmy Shukrani Bakomera aachiliwa huru
Next Bujumbura : suspension of the celebration of the 4th anniversary of the CNL party