Goma: mwandishi wa habari azuiliwa na idara ya ujasusi

Goma: mwandishi wa habari azuiliwa na idara ya ujasusi

Jimmy Shukrani Bakomera mwandishi wa habari na ripota wa VOA (Sauti ya Amerika) Kirundi-Kinyarwanda anazuiliwa na idara ya ujasusi ya Kongo tangu alhamisi hii. HABARI SOS Médias Burundi

Mwenzetu huyo alikamatwa alhamisi hii mchana. Alikuwa katika eneo la Karuba ndani ya wilaya ya Masisi mkoa wa Kivu-kaskazini mashariki mwa DRC.

” Alikuwa ameniambia kuwa anakwenda kufanya ripoti kuhusu mchakato wa kuwaorodhesha wapiga kura katika eneo la mashariki ambao ungeanza alhamisi hii”, alibaini mwandishi wa habari aliyezungumza na ripota huyo wa VOA kabla ya kwenda uwanjani.

Jimmy Shukrani Bakomera anazuiliwa katika jela moja ya idara ya ujasusi Goma (makao makuu ya Kivu kaskazini).

” ijumaa hii Jimmy atapelekwa mjini Kinshasa. Anatuhumiwa kushirikiana na kundi la M23″, ofisi ya idara ya ujasusi mjini Goma imeliambia gazeti la SOS Médias Burundi.

” Amekatazwa kuzungumza na watu “, ofisi hiyo imezidi kusema.

Januari iliyopita, mwenzetu huyo alijeruhiwa na polisi wakati akiripoti juu ya mandamano dhidi ya kikosi cha EAC mjini Goma. Wandishi wa habari wengine walikamatwa na kujeruhiwa pia. Sauti ya Amerika haijatoa maelezo yoyote kuhusu kukamatwa kwa mwandishi huyo tangu tulipoweka hewani habari hii.

Wandishi wengi wamekamatwa na idara za usalama za Kongo na kuzuiliwa katika gereza la polisi au jeshi pasina kufahamisha waajiri wao au familia.

DRC iko kwenye nafasi ya 125 kwa jumla ya nchi 180 kuhusu kuheshimu uhuru wa vyombo vya habari katika orodha ya shirika linalotetea haki za wandishi wa habari la maripota wasio na mipaka.

Previous Burundi : authorities arrest the fifth activist, jail the team suspected of funding terrorism
Next Burundi : viongozi wanahakikisha kukamatwa kwa mwanaharakati mwingine na kumuweka gerezani huku timu yote ikituhumiwa kufadhili ugaidi