Nduta (Tanzania) : kijana mkimbizi kutoka Burundi alipatikana akiwa maiti baada ya kukosekana

Nduta (Tanzania) : kijana mkimbizi kutoka Burundi alipatikana akiwa maiti baada ya kukosekana

Mélance Kwizera mwenye umri wa miaka karibu 20 alipotea wiki moja iliyopita. Alipatikana akiwa maiti karibu na kambi na kuzikwa haraka na jamii ya eneo hilo. Wakimbizi wanaomba uchunguzi ufanyike. HABARI SOS Médias Burundi

Marafiki na majirani wa kijana huyo wanasema kuwa walimuona mara ya mwisho mwanzoni mwa wiki iliyopita.

” Wakati tulipomuona, alikuwa akitoka nje ya kambi akivalia sera za vuguvuga la wa scout. Alikuwa na mazoea ya kutoka kwenda kushiriki katika maombi pamoja na shughuli za kundi la scout. Lakini siku hiyo, huenda alitoka kwa ajili ya shughuli zingine au kwa ajili ya kutafuta kuni za kupikia. Tangu siku hiyo hakurudi”, wanasikitika.

Habari hiyo mbaya ilianza kusambaa ndani ya kambi jumatatu jioni.

” Watanzania walituarifu kuwa kijana wa vuguvugu la scout alipatikana akiwa amefariki karibu ya kambi. Wakati tulipoona picha, tulimufahamu. Alikuwa Mélance Kwizera. Walituonyesha mahali alipozikwa haraka ili kuepusha muili wake kuharibika “, marafiki zake wanaeleza.

Wakimbizi wanadai kuwa kisa hicho kinachoongeza idadi ya mauwaji mengine, visa vya watu kutekwa na kupotezwa kinaachiria kuwa uhusiano kati ya wakimbizi na jamii iliyowapokea sio mzuri hata kidogo.

Familia ya muhanga pamoja viongozi wa kundi la scout ndani ya kambi ya Nduta wanaomba uchunguzi wa kina wa polisi ufanyike kwa ajili ya kuonyesha mazingira ya mauwaji hayo.

Wakimbizi wanalaani visa vya mauwaji ya kawaida na ya kuvizia pamoja na watu kupotezwa ambavyo vimerudi kushuhudiwa ndani ya kambi hiyo inayowapa hifadhi wakimbizi kutoka Burundi zaidi ya elfu 76. Wakimbizi wawili wenye asili ya Burundi waliuwawa na wananchi wa Tanzania tarehe 14 februari iliyopita karibu na kambi ya Nduta wakiwatuhumu kuwabaka wanawake wa Tanzania waliokuwa wakitafuta kuni na wengine waliokuwa wakielekea shambani. Polisi eneo hilo ilifahamisha hayo na kudai kuwa kati ya wakimbizi 12 na 16 huuwawa kila mwaka nje ya kambi nchini Tanzania.

Wiki hii, wajumbe wa polisi kwa ushirikiano na viongozi wa kambi ya Nduta walizidisha mikutano ya kuhamasisha kuhusu ujirani mzuri kati ya wakimbizi na jamii iliyowapokea.

Previous Masisi : mapigano mapya kati ya FARDC na M23
Next Uvira : zaidi ya watu wengine 300 kutoka Burundi wakimbilia nchini DRC