Rwanda : rais Kagame atoa msamaha kwa Paul Rusesabagina

Rwanda : rais Kagame atoa msamaha kwa Paul Rusesabagina

Adhabu ya kifungo dhidi ya Paul Rusesabagina na Callixte Nsabimana alias Sankara ilifutwa kupitia msamaha wa rais. Walikuwa wamekatiwa mmoja kifungo cha miaka 25 jela na mwingine miaka 15 jela. Wafungwa wengine 18 walioadhibiwa kwa kosa la ugaidi wakiwemo warundi walishuhudia vifungo vyao kupunguzwa kwa mjibu wa sheria ya Rwanda. HABARI SOS Médias Burundi

Ni hatua iliyochukuliwa na baraza la mawaziri la ijumaa baada ya kuzingatia maombi ya wahusika.

Paul Rusesabagina na Calixte Nsabimana alias ‘ Sankara ‘, walipatikana na kosa la ugaidi na kuunda makundi ya waasi.

Tarehe 20 mwezi septemba 2021, chumba cha kushughulikia uhalifi wa kimataifa na wa kuvuka mipaka cha korti kuu kilimuadhibu kiongozi huyo wa kundi la FLN linalotajwa kama kundi la kigaidi kwa kosa la ugaidi na kumukatia kifungo cha miaka 25 jela.

Alikamatwa mwezi agosti 2020 akitoka nchini Marekani na kudai kuwa kukamatwa kwake ni utekaji na kinyume cha sheria na kesi yake ikaanza januari 2021.

Rusesabagina na watuhumiwa wenzake akiwemo Nsabimana msemaji wa zamani wa kundi la waasi la FLN walipatikana na makosa ya kuunda kundi la silaha, kujiunga na kundi la kigaidi pamoja pia na kufadhili ugaidi.

Uhalifu wanaotuhumiwa ulifanyika tangu 2018 wakati wapiganaji wa kundi la FLN walitekeleza mashambulizi dhidi ya Rwanda, na kusababisha mauwaji ya watu tisa wakaazi wa mkoa wa kusini mwa Rwanda.

Walisababisha pia majeraha mengi na hasara nyingi za vifaa na kiuchumi.

Rusesabagina na Sankara walipewa adhabu ya kifungo cha miaka 20 jela.

Sankara alikatiwa kifungo cha miaka 15 jela baada ya kukiri makosa na kuomba msamaha.

Wajumbe wengi wa kundi hilo walikamatwa wakitoka katika msitu wa Nyungwe ambao ni muendelezo wa msitu wa Kibira upande wa Burundi. Kati yao walikuwemo wananchi wa Burundi.

Tangazo la baraza la mawaziri la ijumaa chini ya uongozi wa rais wa Rwanda Paul Kagame linahakikisha kuwa watuhumiwa wenzake 18 wa Rusesabagina na Sankara walipunguziwa adhabu.

Jumatatu iliyopita, rais wa Rwanda Paul Kagame alifahamisha kuwa mazungumzo yanaendelea kuhusu ” hatma ya Paul Rusesabagina na kuzidi kuwa kuna uwezekano akaachiliwa huru.

Alitoa maelezo hayo katika mahojiano kando na mkutano wa hivi karibuni kuhusu usalama wa dunia mjini Doha nchini Qatar.

” Sisi sio watu wanaotaka kusalia katika kona moja bila kufanya juhudi zozote za kuelekea mbele” , alizidi kueleza.

” Kuna mazungumzo kuhusu njia zote za kumaliza tatizo hilo bila kuharibu undani wa mkasa huo na ninamatumaini kuwa njia ya kufuata itapatikana ” alizidi kusema.

Rais wa Kagame alirejelea pia baadhi ya visa katika historia ya Rwanda ambapo nchi hiyo ilichukuliwa hatua ambazo baadhi walidai haziwezekani.

Alitaja mifano ya watu waliopatikana na kosa la kufanya mauwaji ya kimbari ya 1994 dhidi ya watutsi ambao walipewa msamaha na kurejea katika jamii ya wanyarwanda.

Tangu kukamatwa kwake Rusesabagina katika mwaka wa 2020, nchi kama Marekani au Ubelgiji ambako alipewa uraia ziliendelea kuomba aachiliwe huru.

Previous Rwanda : President Kagame pardoned Paul Rusesabagina
Next Mabanda : mwanaume mmoja aishi kwa kujificha akihofia kuuwawa na viongozi wa chama cha CNDD-FDD