Mabanda : mwanaume mmoja aishi kwa kujificha akihofia kuuwawa na viongozi wa chama cha CNDD-FDD

Mabanda : mwanaume mmoja aishi kwa kujificha akihofia kuuwawa na viongozi wa chama cha CNDD-FDD

Alain Ndayikunda alitoroka kwake tangu mwezi mmoja uliopita. Anahofia kuuwawa na mkuu wa kitongoji cha Mara pamoja na mkuu wa chama cha CNDD-FDD eneo hilo wanaokiri hadharani. Mkaazi mwingine anazuiliwa jela kwa amri ya wafuasi hao wawili wa chama tawala. HABARI SOS Médias Burundi

Mkasa uliosababisha kutoroka kwa Ndayikunda ulianza mwezi februari. Alituhumiwa kosa la kuacha kutii amri za mkuu wa kitongoji pamoja na kiongozi wa eneo hilo wa chama cha CNDD-FDD.

” Tarehe 25 februari, alikutana na Égide Bizimana pamoja na Hakizimana ambao mmoja ni kiongozi wa Imbonerakure ( wafuasi wa tawi la vijana wa chama cha CNDD-FDD) na mkuu wa chama cha CNDD-FDD eneo la Mara. Walitaka kumuvua nguo lakini akajitetea. Mmiliki wa duka eneo hilo alitaja kitendo cha wanaume hao wawili kuwa ni kinyume cha sheria” mashahidi walieleza.

Kwa mjibu wa wakaazi, watu hao wawili walikuwa wamemaliza siku wakiiba watu wote wanaodai kuwa waliacha kushiriki katika kazi za umaa .

[…], kila mtu ambaye hakushiriki kazi za maendeleo alilazimika kununua biya mbili aina ya Primus kwa ajili ya wafuasi hao wawili wa chama cha CNDD-FDD. Lakini walipomukuta Ndayikunda nje na mgahawa, walimutuhumu kuvaa viatu vya askali jeshi. Na wakaanza kumushambulia wakilenga kumuvua viatu hivyo. Kwanza kabisa zilikuwa tuhuma za uongo lakini pia tabia yao ilikuwa ya kinyama. Na walikuwa wamelewa”, mashahidi walieleza.

Siku moja badaye, mkuu wa kitongoji alimutumia Ndayikunda waranti wa kukamatwa pamoja pia na mumiliki wa duka aliyethubutu kupinga mwenendo wao.

Akihofia yaliyomukuta mwaka wa 2018, Ndayikunda aliamuru kukimbia. Aliyeitika waranti huo hadi sasa anazuiliwa jela.

” Anatoka nje kwa ruhsa ya mkuu wa tarafa. Hata mwishoni mwa juma, aliomba ruhsa ya kwenda kushiriki katika mazishi. Anazuiliwa jela kwa kosa moja la kusema kuwa Ndayikunda alivamiwa kinyume cha sheria. Jiulizeni ambayo yangemukuta Ndayikunda iwapo angekamatwa ? wanasema wakaazi ambao pia wanalaani vitisho hivyo.

Viongozi wa eneo hilo wa chama cha CNDD-FDD wamesalia na chuki dhidi ya Ndayikunda. Wanamutuhumu kuacha kujiunga na chama tawala, kosa ambalo liliwahi kumugharimu mateso, kupigwa na kufungwa kwa siku chache. Wakati huo alituhumiwa kushirikiana na waasi ” ni tuhuma ambazo hazina msingi kulingana na waakazi.

Kulingana na vyanzo hivyo, Ndayikunda aliwashtaki waliomutesa lakini faili haikuendekea.

Familia yake inaomba viongozi wa juu kuwaonya wakuu wa chama cha CNDD-FDD eneo hilo kusimamia amani na usalama kwa ajili ya watu wote hususan kwa ajili ya Ndayikunda ili aweze kurudi nyumbani kwake na kuendelea na shughuli zake kama watu wengine.

Viongozi wa eneo hilo wa chama tawala pamoja na viongozi wa eneo hilo bado hawajatoa maelezo kuhusu mkasa huo.

Previous Rwanda : rais Kagame atoa msamaha kwa Paul Rusesabagina
Next Goma : angalau watoto 16 walifariki dunia kutokana na mazingira mabaya ndani ya kambi mpya ya wakimbizi wa ndani ya Majengo