Masisi : mapigano mapya kati ya FARDC na M23
Mapigano kati ya jeshi la FARDC ( jeshi la Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo) na waasi wa M23 yanaendelea katika maeneo mbali mbali ya wilaya ya Masisi. Baada ya kudhibiti maeneo mengi ya vitongoji vya Matanda na Kamuronza katika wilaya ya Masisi, waasi wa M23 walijaribu kukamata udhibiti wa mji wa kimkakati wa Mushaki uliyopo kwenye umbali wa kilometa 40 ya mji wa Goma (makao makuu ya Kivu kaskazini) jumatano hii. Mapigano yaliendelea hadi jioni. HABARI SOS Médias Burundi
Hali iliendelea kuwa ya wasi wasi katika kituo cha Mushaki ndani ya kitongoji cha Matanda , eneo la Bahunde katika wilaya ya Masisi tangu jumatano asubuhi.
Milio ya silaha ndogo na nzito ilisikika katika milima ya Mushununu na Malehe kwenye umbali wa kilometa takriban mbili kuelekea Mushaki kituo cha kimkakati kwenye umbali wa kilometa 45 magharibi ya mji wa Goma( makao makuu ya Kivu kaskazini).
” FARDC iliweza kurudisha nyuma mashambulizi ya adui aliyekuwa na lengo la kudhibiti eneo hilo la Masisi”, alifahamisha msemaji wa jeshi la Kongo kivu-kaskazini luteni kanali Guillaume Ndjike Kaiko.
Anahakikisha kuwa kituo cha Mushaki bado kinadhibitiwa na FARDC.
“Tulikuwa katika mapambano tangu asubuhi na kutokana na uzoefu wa jeshi la taifa, tuliweza kurudisha nyuma adui mbali na Mashaki “, alisisitiza msemaji huyo.
Kutokana na mapigano hayo, wakaazi wa Mushaki walilazimika kukimbia kwa mjibu wa vyanzo vyetu vya ndani.
Baadhi ya watu walikimbilia eneo la Mupfunyi-Karuba, karibu na Matanda na wengine walielekea katika jiji la Sake kwenye umbali wa kilometa 27 ya mji wa Goma daima magharibi ya mji huo.
” Tuliamuru kukimbia kwa kusubiri kuwa hali itarudi kuwa ya kawaida. Tunatumai kuwa mashuja wetu wa FARDC watachukuwa maeneo yote chini ya udhibiti wa waasi wa M23″, aliambia SOS Médias Burundi mkaazi wa Mushaki aliyekuwa akielekea eneo la Sake jumatano jioni.
Katika tamko lake, msemaji wa FARDC eneo la Kivu Kaskazini hakutoa maelezo kuhusu athari za mapigano hayo ya Mushaki sababu mapigano yaliendelea hadi jumatano jioni.
Ndege za kivuta za Kongo zinajumuika kwenye uwanja wa mapambano katika milima ya Mushununu , Malehe , Murambi na Ruvunda kwa mjibu wa mashahidi.
Hata hivyo, hali ya taharuki iliendelea kushuhudiwa tangu jumatano asubuhi katika eneo la Kahira kitongoji cha Bashali ndani ya wilaya ya Masisi kutokana na mapambano yanayoendelea kati ya FARDC na waasi wa M23 kwenye viunga vya Kitshanga na Kibarizo daima eneo hilo.
Kwa mjibu wa Innocent Baseme kiongozi wa mashirika ya kiraia eneo la Kahira, wakaazi walikimbia kuelekea kijiji jirani cha Osso Banyungu wakihofia usalama wao.
” Hali ni mbaya hapa kwetu sababu asilimia 85 ya wananchi wa Kahira walikimbia kuelekea vijiji jirani kwa kuhofia mapambano. Tuko eneo la Kahira lakini kwa hofu” alibaini Bwana Baseme.
Alizidi hata hivyo kuwa eneo la Kibarizo liko chini ya udhibiti wa waasi wa M23.
” Kwa sasa, eneo la Kibarizo liko chini ya udhibiti wa M23. Na hapa Kahira ni kundi la wazalendo linaodhibiti eneo lote. Tunatumai kuwa mashuja wetu wa FARDC watachukuwa maeneo yote chini ya udhibiti wa waasi”.
Mapigano mengine waliripotiwa kwenye milima ya Bigogwe ambapo waasi wanajaribu kuteka ngome za FARDC katika maeneo ya karibu na Kibarizo na Kahira.
Tangu mwanzoni mwa juni 2022, kundi la M23 lilichukuwa udhibiti wa maeneo mengi katika mkoa wa kivu kaskazini mashariki mwa Kongo likiwemo eneo la Bunagana kwenye mpaka na Uganda. Tangu siku chache zilizopita, waasi wanaosema kuwa walivunja mkataba wa kusitisha vita kwa ajili ya kulinda kabila la wachache watutsi wanaokabiliwa na mauwaji wa halaiki yaliyoandaliwa na serikali ya Kinshasa ” linaendelea kusonga mbele kwenye uwanja wa mapambano hususan katika wilaya ya Rutshuru, Masisi, na Nyiragongo maeno yaliyo karibu na mji wa Goma. Kundi hilo la zamani la watutsi lilichukuwa tena silaha mwishoni mwa 2021 likituhumu viongozi wa Kongo kutoheshimu ahadi zake za kurejesha wapiganaji wake katika maisha ya kawaida. Serikali ya Kongo imekuwa ikituhumu kundi hilo kupata usaidizi kutoka Rwanda.
Serikali ya Rwanda imekuwa ikitupilia mbali madai hayo ikituhumu upande wake viongozi wa Kongo kushirikiana na kundi la waliofanya mauwaji ya kimbari nchini Rwanda la FDLR kwa kuwapa sare, silaha na risasi kwa lengo la ” kusambaratisha ardhi ya Rwanda”
Mapigano yanaendelea licha ya wito wa hivi karibuni wa viongozi wa jumuiya ya mashariki wa kusitisha vurugu katika mkutano wa kilele wa wakuu wa nchi wanachama wa EAC uliofanyika katika jiji kuu la kibiashara la Bujumbura Burundi mwanzoni mwa mwezi huu. Ombi hilo lilitolewa pia na papa François wakati wa ziara yake ya hivi karibuni mjini Kinshasa.
Katika kanda hii, EAC ilituma kikosi. Kikosi hicho kimefanikiwa kukata njia kwa ajili ya kuwasilisha misaada na maeneo kati kati. Idadi kubwa ya wanaharakati wa Kongo wanadai kuwa kikosi hicho ” hakifai ” kama kile cha Monusco (ujumbe wa umoja wa mataifa nchini DRC )” , na wanaomba kirudishwe kwao.
Mandamano mengi yalifanyika katika maeneo tofauti ya miji ya mkoa wa Kivu kaskazini na Kivu kusini hususan kwa ajili ya ” kulaani kikosi hicho”.
About author
You might also like
Kayanza: four people including a woman sentenced to life jail in a murder case
They were sentenced by the First Instance Court of Kayanza (north Burundi). In addition to this sentence, the detainees will have to pay a fine of 20 million Burundi francs
Makamba-Rutana: the ruling party launches a forced fundraising campaign
Residents of Rutana and Makamba provinces (southeast of Burundi) are called upon to respond to the CNDD-FDD party’s fundraising campaign for the elections due in 2025. Members of the ruling
Goma-Gavana mwanajeshi kwa wananchi: askali jeshi wa kikosi cha EAC sio maadui zetu
Gavana wa kijeshi wa mkoa wa kivu kaskazini aliwaomba wananchi wakaazi wa mkoa huo kuacha kushambulia kwa maneno askali waliotumwa mashariki mwa DRC chini ya kikosi cha kikanda cha jumuiya