Bujumbura : watetezi watano wa haki za binadamu waripoti mahakamani
Watetezi watano wa haki za binadamu waliripoti mahakamani jumatatu hii mchana. Kesi ilisikilizwa katika gereza kuu la Bujumbura maarufu Mpimba. Kulingana na sheria ya jinai nchini Burundi, uamzi ungetolewa jumatano hii. HABARI SOS Médias Burundi
Ni mahakama ya Ntahangwa (kaskazini mwa Bujumbura) katika jiji la kibiashara iliyowasikiliza. Majaji walitoa sababu za ukosefu wa kifedha ili kuweza kuwasili kusini mwa jiji kuu la kiuchumi ambako kuna gereza hilo.
Wanaharakati hao walisaidiwa na mawakili watetezi wawili SOS Médias Burundi ilipata taarifa hizo. Mawakili hao hawakutaka kuzungumzia kesi hiyo ambayo pia inaongelewa kidogo na mashirika ya kutetea haki za binadamu.
Wahusika walikuwa walisikilizwa na jaji tarehe 16 februari iliyopita siki mbili baada ya kukamatwa kwao. Walihojiwa kuhusu ” visa vya kuhatarisha usalama wa ndani ya taifa na matumizi ya pesa yenye utata” chanzo cha karibu na faili hiyo kiliarifu SOS Médias Burundi.
Katika maelezo yake kwa wandishi wa habari wa ndani tarehe 16 februari, waziri wa Burundi wa mambo ya ndani na usalama alibaini sababu zilizopelekea watetezi hao wa haki za binadamu kukamatwa.
“[…], watu hao hutumika na shirika lililojiondoa nchini Burundi wakati wa muhula wa 2015-2020 lakini pamoja na kujiondoa, shirika hilo liliendelea kutumika na mashirika ya kiraia yaliyoidhinishwa pamoja na yale yasio rasmi nchini Burundi “, alifahamisha waziri Martin Niteretse.
Chanzo cha pesa kinacholeta utata
Kwa mjibu wa Martin Niteretse, shirika hilo hutoa ufadhili wa pesa kwa mashariki ya kiraia kwa njia ya uficho.
” Ripoti zinazotungwa na mashirika hayo na kutumwa katika wizara ya mambo ya ndani hazionyeshi kamwe matumizi ya pesa hiyo. Kwa hiyo tulifanya uchunguzi taratibu tangu miezi mitatu iliyopita na tukagundua mashariki hayo yaliyoidhinishwa na ambayo hayakuidhinishwa hutumika na shirika hilo la kigeni”, alibaini kiongozi huyo wa Burundi ambaye alizidi kusema kuwa watu wanne walikamatwa wakiwa kwenye uwanja wa ndege wa Bujumbura wakielekea Kampala katika mkutano ” ulioandaliwa na shirika hilo katika lengo la kuanzisha jopo la uongozi”.
Ugaidi
” Matokeo tulionayo kwa sasa yanaonyesha kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kufadhili ugaidi kupitia fedha hiyo. Tunatakiwa kuwa makini kuhusiana na pointi hizo ili pasiwe chochote kinachoweza kuvuruga amani na utulivu wa umaa ” alimalizia.
Kosa la ugaidi huadhibiwa kwa kifungo cha kati ya miaka kumi na ishirini pamoja na faini ya kati ya laki mbili hadi milioni moja sarafu za Burundi kwa mjibu wa sheria ya jinai nchini Burundi. Na iwapo kisa hicho kimesababisha kifo cha mtu mmoja au watu wengi, adhabu yake ni kifungo cha maisha jela.
Tangu rais Ndayishimiye alipoingia madarakani katika mwaka wa 2020, wanaharakati watatu akiwemo mmoja aliyekamatwa baada ya kiapo chake, wote walikuwa wameachiliwa huru. Kabla ya watetezi hao watano kukamatwa, hakuna mtetezi wa haki za binadamu aliyekuwa jela katika nchi hiyo ndogo ya Afrika mashariki.