Burundi : chama cha CNL kiliadhimisha miaka minne kwa shangwe

Burundi : chama cha CNL kiliadhimisha miaka minne kwa shangwe

Chama cha CNL kiliandaa Kongamano la kawaida kuadhimisha miaka minne ya uhai wa chama hicho tarehe 12 machi. Mbele ya ma elfu ya wafuasi pamoja na wageni wakiwemo wajumbe wa chama cha CNDD-FDD, Agathon Rwasa aliwaomba wafuasi wa chama kuungana. Ilikuwa fursa pia ya kuwaambia wafuasi kwamba sheria za chama zilirekebishwa kwa kuzingatia mhawanyo mpya wa Burundi katika mikoa mitano. HABARI SOS Médias Burundi

Ilikuwa furaha kubwa kwenye makao makuu ya chama cha CNL katika kata ya 9, kijiji cha Ngagara tarafa ya Ntahangwa kaskazini mwa jiji la kibiashara la Bujumbura. Basi za uchukuzi zilikuwa zikiwaleta wafuasi kutoka maeneo mbali mbali ya nchi ambao walikuwa wakiimba nyimbo za kumusifu kiongozi wao Agathon Rwasa tangu asubuhi. Mkoa peke wa Rumonge ulitumia basi 32 aina ya Coaster (moja inabeba angalau watu 35) .

Mbali na wageni kutoka vyama halali nchini Burundi kikiwemo chama tawala cha CNDD-FDD, walikuwepo pia wawakilishi wa balozi mbali mbali ukiwemo ubalozi wa Marekani. Alihudhuria pia mwakilishi wa chama cha upinzani cha ACT Wazalendo nchini Tanzania.

Wafuasi wa chama hicho kutoka mkoa mmoja walikaa pamoja katika uwanja huo mkubwa ambapo CNL ina mpango wa kujenga makao makuu ya chama ngazi ya taifa. Ma elfu ya watu walikuwa wakicheza na kuimba huku idadi ndogo ya wengine wakiwa nje ya uwanja huo baada ya kukosa nafasi ndani ya uwanja.

Vitenge vilivyosababisha taharuki

Katika hutba yake, Agathon Rwasa alikosoa vikali kampuni ya Afritextile inayotengeneza nguo nchini Burundi. Alisema kuwa awali kampuni hiyo iliahidi kuwatengenezea kitendo chenye nembo za chama lakini badaye, kampuni hiyo ilitoa hoja zisizo na msingi kwa ajili ya kutotengeneza kitenge hicho siku nyingi baada ya kufanya agizo huku kongamano likiwa linakaribia”.

Na kuendelea kuwa : Tulilazimika kufanya oda nyingine nje ya nchi lakini mamlaka ya mapato ya serikali na chama tawala walivuruga. Lakini hatimaye tulipata sare nyingine” , na hivyo kiongozi huyo kujipongeza na kudai kuwa anafurahi kuona ndugu zake wakivaa kitenge kingine.

Utawala na kasoro zake

Bwana Rwasa alirejelea umasikini unaowakabili wananchi wa Burundi katika sekta zote hususan mfumko wa bei. Alimushukuru rais Evariste Ndayishimiye ” aliyetangaza kuwa mara nyingi kuna visa vya unyanyasaji na utawala mbaya”. Na kuzidi kushambulia : ” sikubaliani naye anaposema kuwa hakuna ukosefu wa ajira nchini Burundi”. Kiongozi huyo wa chama kikuu cha upinzani nchini Burundi aligusia pia udhaifu wa utawala wa sasa uliodhihirika hususan wakati wa ziara za hivi karibuni za mawaziri katika mikoa. Kwa mjibu wa Rwasa, ” sekta zote zimewakilishwa katika mikoa. Sekta hizo, hutoa ripoti kwa mawaziri husika “.

Pamoja na hayo, aliwatolea ushahuri wafuasi wa CNL akiwasihi kuacha kuwashambulia wafuasi wa zamani wa chama sababu ” agashitsi ka kera kavumbika umuriro” ( mapenzi yao kwa chama ni makubwa )”

Katika kongamano hilo, ulichukuliwa uamzi wa kupanga upya uongozi wa chama chao kwa kuzingatia mgawanyo mpya wa nchi ambao utatangazwa hivi karibuni na rais wa jamuhuri “. Mkuu wa chama hicho alifahamisha pia kuwa tayari sheria za ndani ya chama zilirekebishwa kwa kuzingatia mtiribuo huo mpya.

Hakuhudhuria sherehe hizo zilizojumulisha nyimbo na michezo na kumalizika jioni, mbunge Katty Kezimana aliyechaguliwa hivi karibuni kuwa mbunge katika bunge la EALA, bunge la jumuiya ya afrika mashariki lenye makao yake mjini Arusha nchini Tanzania licha ya upinzani wa kiongozi wa CNL .

Previous Goma: ma mia ya visa vya ubakaji yaripotiwa eneo la Kanyarutchinya
Next Fizi : mapigano kati ya kundi la Mai Mai na Twirwaneho