Rwanda-Burundi : michezo kwa ajili ya kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi za polisi
Rwanda inayapokea mashindano ya kikanda ya jumuiya ya ushirikiano wa wakuu wa polisi ya Afrika mashariki, EAPCCO, (The Eastern Afrika Police Chefs cooperation Organisation). Katika uzinduzi wa michuano hiyo, timu ya taifa ya polisi ya Burundi ilichuana na timu ya polisi ya Rwanda. Timu ya mpira wa miguu ya wenyeji ilishinda ile ya polisi ya Burundi (PNB) bao 3 kwa 1 katika mechi ya kwanza jumanne tarehe 21 kwenye uwanja wa Kigali uliopewa hivi karibuni jina la Pelé ilikuwa saa tisa. Mashindano hayo yanaendelea hadi 27 machi. HABARI SOS Médias Burundi
Michezo mingine ni pamoja na mpira wa wavu, volley ball, Netball, Karaté, michezo wa kulenga shabaha pamoja pia na riadha.
Hata kama michuano hiyo inajumulisha timu za akinamama na wanaume kutoka nchi za jumuiya ya Afrika mashariki, kati ya Burundi na Rwanda michuano hiyo inaonyesha sura nyingine.
” Mashindano hayo yana umuhimu mkubwa kwetu taasisi za usalama sababu yanatusaidia kubadilishana ujuzi, kujuana zaidi na kukutana pia. Kuhusu Rwanda na Burundi, ni hatua nyingine katika ushirikiano na kurejesha uhusiano na tuna uhakika kuwa mashindano hayo yatachangia katika mpango wa kukabiliana na uhalifu wa kuvuka mpaka wa pamoja”, alifahamisha meja jemedali wa polisi Jean Damascène Nkeshimana mkuu wa ujumbe kutoka Burundi.
Na kuzidi kuwa :” Tunataka pia kubadilishana habari muhimu kuhusu wahalifu na wanaovuruga usalama. Hatutaweza kuvumilia aina hiyo ya uhalifu kupitia mtandao huo unaoimarishwa na michuano hiyo”.
Polisi ya Burundi inafahamisha kuwa ilipokelewa vizuri mjini Kigali, ikizingatiwa kuwa ni mara ya kwanza wajumbe wengi wa idara hiyo ya usalama wakiwasili eneo hilo na kusalia kwa zaidi ya wiki moja tangu mzozo wa kidiplomasia kuanza kati ya nchi hizo mbili mwaka wa 2015.
” Tulipewa mapokezi mazuri. Tuyizangumzia pia na wenzetu wa Rwanda, yalikuwa mapokezi ya hali ya juu. Hakuna askali wetu hata mmoja aliyekosa kitu malahi alipopewa hifadhi. Tunayahakikisha “, alibaini hayo daima meja jemedali wa polisi Jean Damascène Nkeshimana.
Mbali na Rwanda na Burundi, nchi zingine zinazoshiriki mashindano hayo ni pamoja na Uganda, Tanzania, Kenya, Sudani kusini na Ethiopia.
Nchi ya DRC haikuwakilishwa. Nchi hiyo kubwa ilisusia mashindano hayo kutokana na kuzorota kwa uhusiano kati yake na Rwanda mwenyeji wa michuano hiyo kulingana na vyanzo katika diplomasia mjini Kigali.
Nchi zingine ambazo hazikuhudhuria mashindano hayo ni Djibouti, Eritrea, visiwa vya Usheli sheli , Somalia na Comore.
Rwanda imekuwa nchi ya nne kuandaa michuano hiyo ya askali polisi wa EAPCCO baada ya Uganda, Kenya na Tanzania
About author
You might also like
Rwanda-DRC: ndege ya kivita ya Kongo kwa mara nyingine imevunja sheria na kuingia katika anga ya Rwanda
Serikali ya Rwanda ilifahamisha kuwa anga yake imeingiliwa na ndege la kivita ya DRC(Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo). Viongozi wa Rwanda wamekitaja kisa hicho kama ” cha uchokozi” kinachokiuka makubaliano
Burundi : two residences of former Prime Minister Alain Guillaume Bunyoni targeted by a police search
The two residences are located in the commercial capital Bujumbura and in the province of Rutana (southeastern Burundi). They were searched by police and intelligence on Monday. The Attorney General
Ituri : nearly 30 ADF attackers killed, others captured and hostages released, according to the army
The Congolese army has taken stock of its operations during the month of January 2023 in Ituri province (eastern DRC). It claims to have killed 28 and captured 14 ADF