Beni: waasi nane wa ADF wauwawa
Jeshi la Kongo linafahamisha kuwa liliwauwa waasi nane na kuwakamata wengine 5 wa ADF (kundi la waasi wa Uganda) alhamisi hii katika kijiji cha Kisasu Ngandu. Ni katika wilaya ya Beni mkoa wa Kivu-kaskazini (mashariki mwa DRC). HABARI SOS Médias Burundi
Ni msemaji wa kikosi cha Sokola 1, kaskazini-kubwa aliyefahamisha hayo.
” Ni matokeo ya mapigano kati ya watu wetu na kundi la ADF katika usiku wa alhamisi kuamkia ijumaa kusini mwa eneo la Karuruma katika kijiji cha Bashi. Kwenye eneo la mapigano magaidi watatu wa ADF waliuwawa moja kwa moja. Miili mingine mitano ilipatikana baada ya mapigano”, aliripoti kepteni Antony Mualushayi.
Anazidi kuwa silaha aina ya AK-47 na vifaa vya mawasiliano vilikamatwa pia.
[…], baada ya kushindwa, aduwi alielekea katika mbuga ya wanyama ya Virunga. Tunawaomba raia wakaazi wa karibu na hifadhi hiyo ya kimataifa kuwa makini”, alizidi kusema.
” Kikundi cha ADF kwa sasa linakabiliwa na mashambulizi ya jeshi huku kikijaribu kulipiza kisasi wakati huu wa siku kuu. Huduma zetu maalum zilifichua mtandao wa magaidi wa ADF uliokuwa ikiandaa mashambulizi dhidi ya mji wa Béni “, alimalizia.
You might also like
Buganda: kijana Imbonerakure auwawa na mwanajeshi
Kisa hicho kilitokea alhamisi hii kwenye transversale ya nne katika kijiji cha Nyamitanga mkoa wa Cibitoke (kaskazini-magharibi mwa Burundi). Mwanajeshi alimpiga risasi kijana Imbonerakure (mfuasi wa tawi la vijana la
Makamba : taxi drivers on strike against untimely police fines
Drivers of so-called probox transport vehicles have been on strike since Monday. They are protesting against untimely fines imposed on them. They are either accused of improper loading or exceeding
Gitega: Imbonerakure commit crimes with impunity
On September 2, Vital Ndabemeye died at Sainte Thérèse hospital in Gitega (central Burundi). He had been hospitalized after being seriously beaten up and injured by Imbonerakure (members of the
