Burundi: Viongozi walikatalia kwa mara ya tatu shirika la AC-GENOCIDE Cirimoso kuadhimisha kumbukumbu ya mauwaji ya Kibimba

Burundi: Viongozi walikatalia kwa mara ya tatu shirika la AC-GENOCIDE Cirimoso kuadhimisha kumbukumbu ya mauwaji ya Kibimba

Shirika la AC-GENOCIDE Cirimoso halikuruhusiwa kuelekea kwenye mrana wa ukumbusho wa mauwaji ya wanafunzi 150 wa kabila la watutsi waliuwawa tarehe 21 oktoba mwaka 1993 baada ya mauwaji ya rais wa kwanza kutoka kabila la Bahutu aliyechaguliwa kidemokrasia Ndadaye Melchior. Waziri wa mambo ya ndani amewaelezea wawakilishi wa shirika hilo ” Ndadaye ni shujaa wa kitaifa na hivyo kila mwananchi anatakiwa kujielekeza kwenye makaburi yake ili kumpa heshma. Kulingana na shirika hilo, huo ni ukiukwaji wa haki za binadamu na shambulio dhidi ya kumbukumbu ya wahanga wa mauwaji ya halaiki yaliyolenga wa Tutsi”. HABARI SOS Médias Burundi

Ni katika siku ya jumatano ambapo waziri wa mambo ya ndani amewapa taarifa wahusika. Martin Niteretse ameitisha mkutano katika ofisi yake ndani ya jiji kuu la kibiashara la Bujumbura ili kuwaambia sababu zilizopelekea kuwanyima ruhsa.

” Tarehe 21 oktoba ni siku ambapo tunaadhimisha kumbukumbu ya mauwaji ya rais Melchior Ndadaye. Ni shujaa wa kitaifa na kila mtu anakatiwa kwenye kwenye makaburi yake kutoa heshma”, amejaribu kuwaelewesha.

Hii ni mara ya tatu mfururizo ambapo viongozi tawala nchini Burundi wakiwazuia wajumbe wa shirika la AC-GENOCIDE Cirimoso kuadhimisha kumbukumbu ya mauwaji ya Kibimba ambapo wanafunzi zaidi ya 150 kutoka kabila la watutsi waliuwawa tarehe 21 oktoba 1993.

” Ni hatua isiyosaidia katika maridhiano. Waziri kwa mara nyingine ametuvunja moyo. Ndadaye aliuwawa na wafanyakazi wa serikali kadharika na hao watoto. Watu wanatakiwa kuwa na haki ya kukumbuka watu wao waliouwawa” alijibu Terence Mushano naibu wa kiongozi wa shirika la AC-GENOCIDE Cirimoso.
Na kulingana na Emmanuel Nkurunziza katibu wa shirika la AC-GENOCIDE Canada, ni shambulio dhidi ya kumbukumbu ya wahanga wa mauwaji halaiki yaliyolenga Watutsi”.

Tangu 2020, mashirika na wazazi wa wanafunzi hawaruhusiwi kuelekea kutoa heshma mbele ya watu wao kama wanavyotaka.

Katika miaka miwili iliyopita, viongozi wa Burundi walitoa sababu za kiafya zinazoambatana na janga la COVID-19 na usalama katika eneo la kuzaliwa rais Evariste Ndayishimiye ambapo alijenga makaazi.

Nikumbushe kuwa zaidi ya wanafunzi 150 wa kabila la watutsi kwenye shule ya sekondari ya Kibimba tarafani Giheta mkoa wa Gitega ( kati kati mwa Burundi) walikusanywa kwenye kituo cha mafuta cha Kwibubu tarehe 21 oktoba 1993 kabla ya kupata kifo cha kuhakikishwa. Baadhi waliachomwa moto,wengine kukatwa kichwa. Ni kufuatia mauwaji ya rais wa kwanza wa kabila la Bahutu Melchior Ndadaye aliyechaguliwa kidemokrasia.

Burundi inajumulisha makabila kama jirani yake Rwanda kaskazini ambapo mauwaji ya genoside dhidi ya kabila la watutsi yalifanyika na kukubaliwa na UN.

Nchini Burundi, wahutu na watutsi bado hawajakubaliana kuhusu kutoa jina la ukatili uliyosababisha vifo vya watu wao. Watutsi wanataka mauwaji ya mwaka wa 1993 yalitokea baada ya kifo cha rais Melchior Ndadaye, yachukuliwa kama ” jenoside ” wakati ambapo wahutu akiwemo rais wa zamani, mashirika ya ndani pamoja na vyama kadhaa vya kisiasa kikiwemo chama cha Frodebu cha Ndadaye wakishinikiza bila kuacha ili kutaja wenyewe kuwa mauwaji ya 1972 yaliyopelekea vifo vya wa Hutu na wa Tutsi yalikuwa mauwaji ya “Jenoside ” dhidi ya wahutu

Mwezi mei uliopita, rais Neva alijizuia kuidhinisha hatua ya bunge la taifa ya kukubalisha kuwa mauwaji ya 1972 yalikuwa mauwaji ya halaiki ” jenoside” dhidi ya wahutu nchini Burundi ” hatua iliyochikuliwa kwa kuzingatia ripoti isiyokubaliwa na pande zote ya kamati ya ukweli na maridhiano CVR

Previous Kakuma (Kenya) : Zaidi ya watu 200 wanaotafuta hifadhi ya ukimbizi wakubaliwa
Next Bubanza: former MP Fabien Banciryanino sparks controversy