Mkutano wa baba François na waathiriwa wa mashariki mwa DRC: maumivu yenu ni maumivu yangu (baba mtakatifu)

Mkutano wa baba François na waathiriwa wa mashariki mwa DRC: maumivu yenu ni maumivu yangu (baba mtakatifu)

Mkuu wa kanisa katoliki alikutana jumatano hii alasiri na wawakilishi wa wahanga wa maovu yanayotendeka mashariki mwa Kongi ambako makundi mengi ya silaha ya ndani na nje yanaripotiwa. Aliwapokea pia wawakilishi wa wakimbizi wa uraia mwingi wakiwemo warundi kutoka kambi ya Mulongwe ndani ya mkoa wa Kivu kusini. Aliwasikiliza na kufanya maombi pamoja nao kwa ajili yao. Pope aliwaambia kuwa “maumivu yenu ni maumivu yangu”. Wahusika walimushukuru mkuu huyo wa Vatican ambaye “alikuja kutufariji”. HABARI SOS Médias Burundi

Kwa umakini zaidi na kwa kipindi cha muda mrefu, baba François alisikiliza ushuhuda wa waathiriwa: watoto, akinamama na wanaume kutoka maeneo mbali mbali ya mashariki mwa nchi hiyo kubwa ya afrika ya kati.

Na ili kuonyesha kuwa anawajari, kwa baadhi alionyesha ishara ya mkono, wengine aliwapa tasbihi na kwa wengine mkufu kabla ya kuwabariki.

Wanawake walikuwa wengi ambao walitoa ushuhuda kuhusu mateso waliofanyiwa na wanaume wenye silaha. Mfano ni mwanamke mmoja aliyepandisha mikono kuonyesha namna ilivyokatwa, athari ya mashambulizi yenye unyama wa kuzidi kipimo.

Bijou Makumbi Kamala ni mvulana mzaliwa wa Goma makao makuu ya Kivu-kaskazini. Alitekwa na watu wenye silaha ambao waliishi naye kwa muda wa mwaka mmoja na miezi saba. Hata kama anadai kuwa aliweza kutoroka badaye, alijifungua watoto wawili. Matokeo ya kisa cha upakaji.

Orodha ya maovu ni ndefu: ubakaji, mauwaji, kukata viungo vya muili….Wasichana wadogo kama Léonie Matumaini mwenye asili ya Béni anakumbuka ukatili ambao alishuhudia.

” Wajumbe wa familia yangu waliuwawa nikishuhudia, wauwaji walinikabidhi kisu walichotumia kutekeleza mauwaji hayo ili nikirudishe kwa wanajeshi”.

Lakini aliwasamehe ” niwaweka mbele ya msalaba wa ushindi wa yesu kristu kisu kinachofanana na kile kilichowauwa wajumbe wa familia yangu mbele ya macho yangu”.

Bijou ambaye maisha yake yaligeuka tangu siku alipokutana na watu wenye silaha asubuhi akielekea mtoni katika wilaya ya Walikale anaishi katika huzuni mkubwa.

“Watoto wangu hawatamfahamu kamwe baba yao” alalamika msichana huyo ambaye alivamiwa na mkuu wa kikundi cha waasi.

“Marafiki wangu wengine waliotekwa pamoja na mimi katika siku hiyo hawakuweza kurudi. Sijuwi iwapo walifariki au la, mama huyo bado anajiuliza.

Aiméda anakumbuka namna alivyotekwa nyara pia na kufanywa mtumwa wa ngomo ndani ya mbuga ya wanyama ya Kahuzi Biega.

Pamoja na kubakwa na watu wengi, anasema kuwa walikuwa wakilazimishwa kula nyama ya mtu.

” Kila siku, watu watano hadi kumi walikuwa wakibaka kila mmoja wetu. Walikuwa wakitupa chakula cha ugali wa mahindi na nyama za watu”, alitoa ushuhuda huo.

Ladislas Kambale ambaye atatimiza miaka 17 badaye mwezi julai alishuhudia kisa cha mauwaji ya baba yake, kaka mkubwa aliuwawa katika mazingira ya kutatanisha na mama yake kutekwa nyara na watu wenye silaha. Hakuweza kurudi.

” Kulingana na kijana hiyo ambaye hawezi kusinzia usiku, ni vigumu kuelewa kiwango hicho cha ubaya- ukatili huo wa kinyama”.

Mtoto wa pili katika familia yake, mwanafunzi wa darasa la sita mwenye asili ya wilaya ya Beni aliishi nyakati ngumu siku ya kuuwawa kwa baba yake.

” Baba yangu yeye, aliuwawa wakati nikiwepo. Nilishuhua namna wanavyomukata vipande harafu wakamkata kichwa na kukiweka ndani ya chungu”, alisema na kukumbusha kuwa sasa anaishi na dada zake wawili.

Yatima huyo pia alichagua kusamehe

” Mimi na watoto wengine ambao wako hapa tulitoa msamaha kwa wauwaji. Ni kwa sababu hiyo ninaweka mbele ya msalaba wa ushindi, mpanga unaofanana na ule uliotumiwa kumuuwa baba yangu”.

Watumishi wa Mungu pia hawakuepukika na ukatili unaoripotiwa mashariki mwa nchi hiyo yenye utajiri mkubwa wa madini.

Niliona ukatili : watu wanavyokatwa kama vile bucha anavyokata nyama, akinama wanaotolewa mimba, wanaume wanaokatwa vichwa ” anataja padri Guy-Robert Mandro Deholo aliyekatwa vidole vya mkono. Alitoa ushuhuda wa mtu kwa jina la Désiré Dhetsina aliyepotea miezi michache iliyopita pasina kuacha habari.

Katika ushuhuda ambao aliandaa kabla ya kupotea kwake, manusura huyo wa kambi ya wakimbizi ya Bule katika kitongoji cha Bahema Badjere wilayani Djugu, anasema kuna mpango wa kumaliza watu unaoendelea kila siku.

Waathiriwa walimushukuru baba mtakatifu ambale” alikuja kutufariji”.

Wakimbizi

Baba anayejichukuwa kama mjumbe wa amani ” akiwa kwenye makao ya kanisa mjini Kinshasa, alikutana na wawakilishi wa wakimbizi wenye uraia mwingi wakiwemo warundi. Angelique Malipo anapewa hifadhi katika kambi ya wakimbizi ya Mulongwe ndani ya Kivu Kusini.

Aliwakilisha wakaazi wa kambi ya Mulongwe na Lusenda kambi nyingine ya wakimbizi kutoka Burundi ndani ya mkoa wa kivu-kusini yenye wakimbizi 41.836.

” Tumemkabidhi barua inayolaani ukatili ambao unatukabili, tumemuarifu kuhusu mauwaji, unyanyasaji, ubakaji dhidi yetu kila siku, ameambia SOS Médias Burundi.

Angélique Malepo ameridhika.

” Ninafuraha nyingi kuona baba amepokea barua kutoka kwa wakimbizi kutoka Burundi ndani ya kambi ya Mulongwe na Lusenda. Anafahamu zaidi kuhusu hali yetu iwapo atasoma barua hiyo”.

Baba François alilaani nguvu za nje na ndani zinazopora eneo hilo la Kongo”, ambazo zinadhibiti vijiji na kujihusisha na ugavi wa eneo hilo”.

Kwa wahanga, baba mtakatifu alisema” maumivu yenu ni maumivu yangu”, na kutoa wito kuhusu kusitisha uporaji wa madini ya DRC ambao kwa mjibu wake, unasababisha waathiriwa wasiokuwa na hatia.

Goma pasina baraka

Mwanzoni papa François angejielekeaa mjini Goma makao makuu ya mkoa wa Kivu-kaskazini mashariki. Ni kulingana na ratiba iliyoonyeshwa katika mwezi julai uliopita kabla ya safari yake kuahirishwa kutokana na sababu za tatizo lake la mguu. Haikuwa hivo.

” Ningependa kufika Goma lakini kutokana na vita hatuwezi kuwasili” , alihakikisha baba huyo wa kwanza katika historia kutoba bara la amerika ya kusini akiwa ndani ya ndege siku ya jumanne. Kanda hilo linakabiliwa na mapigano kati ya kundi la M23 na FARDC ( jeshi la jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo).

” Dunia imetusahawu”, amelaani askofu mkuu wa Goma Willy Ngumbi Ndengele siku chache zilizopita.

Previous Meeting of Pope Francis with victims of eastern DRC : your suffering is my suffering (the sovereign pontiff)
Next Burundi :shirika la IDHB linahakikisha kuna utulivu na mvutano kati ya viongozi wa juu