Burundi :shirika la IDHB linahakikisha kuna utulivu na mvutano kati ya viongozi wa juu

Burundi :shirika la IDHB linahakikisha kuna utulivu na mvutano kati ya viongozi wa juu

Shirika la kutetea haki za binadamu nchini Burundi la IDHB limetoa ripoti yake ya kila mwaka ambapo linaeleza uwepo wa mvutano mkubwa kati ya viongozi wakuu wa Burundi ambao unaonekana kutoficha utulivu na nia ya kuendeleza ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu. Kwa mjibu wa watafiti wake, sio wakati kumaliza vita nchini Burundi. HABARI SOS Médias Burundi

Shirika la IDHB lilifuatilia mabadiliko ya kisiasa ya mwishoni mwa mwaka wa 2022.

” Rais Evariste Ndayishimiye alionyesha nguvu yake na kufanya kile ambacho watu hawakutarajia, kumufuta kazi waziri mkuu Alain Guillaume Bunyoni. Hatua hiyo ya kumufuta kazi waziri mkuu pengine ikaimarisha nguvu za utawala wa rais Ndayishimiye, lakini mchakato huo unaweza kuwa wa muda”, ripoti hiyo inasema.

Wakati huo huo, ripoti hiyo ya IDHB inasema kuwa ” Révérien Ndikuriyo katibu mkuu wa chama cha CNDD-FDD na mjumbe mwenye ushawishi katika mrengo wa kundi la wagumu, anaendelea kuonyesha uungwaji mkono kwa hayati rais Pierre Nkurunziza, na kutofautiana na rais Ndayishimiye na kwenda kinyume na mabadiliko yaliyoahidiwa na rais huyo.

Mifano

” Katika mwaka wa 2022, Ndikuriyo aliandaa mafunzo ya ” uzalendo kwa ajili ya ma elfu ya vijana Imbonerakure na alitoa kauli nzito katika baadhi ya sherehe za uhitimisho. Aliandaa pia mafunzo ya zaidi ya vijana Imbonerakure 200 katika mkoa wa Makamba kwa lengo la kuwatuma kufanya kazi katika sekta ya usalama binafsi zikilengwa nchini ya mashariki ya kati barani Asia “, watafiti wa shirika la IDHB wametaja.

2025 na 2027 kati kati

Licha ya mipasuko ya ndani, chama cha CNDD-FDD kinakubaliana kuhusu jambo moja kwa mjibu wa IDHB.

” Nia ya kutaka kushinda uchaguzi wa bunge wa 2025 pamoja na uchaguzi wa urais wa 2027. Ndikuriyo aliwambia Imbonerakure kuwa wanatakiwa kuhamasisha wajumbe wa vyama vya upinzani kujiunga na CNDD-FDD hadi 2023. Alizidi kusema kuwa badaye chama cha CNDD-FDD kitafikia hatua inayofuata na haitawezekana tena kujiunga na chama hicho. Vijana Imbonerakure walitoa vitisho kwa wapinzani vya kuwajeruhi na kuwauwa kwa iwapo watapinga kujiunga na CNDD-FDD” ripoti hiyo inasema.

Utulivu usio wa uhakika…..

Kuhusu uwanja wa haki za binadamu, mwaka wa 2022 ulikuwa sio wa damu nyingi.

” Mwaka huo ulishuhudia visa vya mauwaji na wapinzani wa serikali kutoweka vilipungua. Idadi ya visa vya unyanyasaji wa watu ambao wako katika mikono ya wajumbe wa idara ya ujasusi na polisi vilivyoripotiwa 2022 vilikuwa chini ukilinganisha na miaka iliyopita, lakini ni vigumu kuelezea athari za visa hivyo vinavyofichwa”. shirika la IDHB linasema.

Katika mikoa, wajumbe wa tawi la vijana wafuasi wa chama madarakani Imbonerakure walionekana watulivu ukilinganisha na miaka na kabla katika mienendo yao dhidi ya mahasimu hao wa chama kikuu cha upinzani cha CNL shirika hilo linapongeza.

Hata hivyo, shirika hilo liliorodhesha visa ambapo Imbonerakure waliwajeruhi wafuasi wa CNL.

” Imbonerakure na wafuasi wengine wa chama tawala kwa mara nyingi, waliwatishia wafuasi wa vyama vya upinzani na kuwalazimisha kujiunga na chama tawala, baadhi ya wafuasi wa vyama vya upinzani hatimae walilazimika kujiunga na chama cha CNDD-FDD kwa ajili ya kujilinda na kulinda njia za kujihudumia. Katika mikoa mingi, viongozi wa ndani waliwazuia wafuasi wa CNL kuongoza mikutano “, yanasomeka ndani ya ripoti hiyo.

Sababu zingine za utulivu ndani ya chama kulingana na IDHB ni sababu za nje ya chama tawala.

“Chama cha CNL licha ya kuwajibika uwanjani kinaonekana kupoteza pande ya nguvu zake. Kiongozi wa chama Agathon Rwasa aliamuru kujishusha ukilinganisha na miaka ya kabla na kutoa matamshi ya kukosoa kwenye nyakati tofauti na ukosoaji wake sio mkali kuhusiana na namna serikali inavyoshughulikia mzozo wa kiuchumi pamoja na mgogoro wa ndani “, tathmini hiyo unatolewa na watafiti.

” Utalivu mdogo unaoshuhudiwa katika maeneo mengi ya nchi unaweza kuleta afueni lakini warundi wanafamu kuwa sio sharti ngumu ili uvunjanji wa haki za binadamu uweze kurudi tena”. shirika la IDHB linasema.

Hali ya kutoadhimu….

Shirika la IDHB hata hivyo linaweka hadharani hali ya kutoadhibiwa inayoendelea kushuhudiwa kwa vijana Imbonerakure.

” Tuhuma zisizokuwa na msingi dhidi ya mfuasi wa chama cha upinzani zinaweza kumuletea matatizo makubwa. Wafuasi wa vyama vya upinzani wanakabiliwa na aina hiyo ya mateso kwa miaka kadhaa huku wengine wakinufaika na hali ya kutoadhibiwa” , ripoti hiyo inalaani.

Licha ya ahadi za rais Ndayishimiye, uwezo mkubwa wa Imbonerakure haukudhofishwa kwa kiwango kinacholingana katika nchi yote.

” Wanaendelea kufanya doria katika barabara usiku, wakiwa wamevalia sare na viatu vya kijeshi huku wakishikilia silaha bandia, mapanga, visu au fimbo wakionyesha vyombo vya mawasiliano aina ya Motorola ambavyo walipewa kwa sababu za kiusalama huku walikamata watu waliochelewa kuwasili nyumbani “, wachunguzi wa IDHB walihakikisha.

” Baadhi ya Imbonerakure waliendelea kutumia ukatili na katika maswala ya siasa. Baadhi ya visa hivyo vya ukatili vilifanyika kwa ngazi ya china huku baadhi wakiwa walikamatwa . Lakini katika idadi kubwa ya visa vya kisiasa, viongozi wa sheria hawakuweza kuwafuatilia tuliacha kuwachukulia adhabu” watafiti hao wanazidi kusema.

Msemaji wa serikali Prosper Ntahorwamiye hakuwa karibu ili aweze kujieleza juu ya madai hayo pamoja pia na afisa mkuu wa ofisi ya mawasiliano kwenye chama tawala Nancy Ninette Mutoni.

Hivi karibuni, aliwambia wandishi wa habari kuwa ” Imbonerakure ni mifano ya kuigwa na wanawaheshimu wengine”.

Kwa upande wao, viongozi wa nchi hiyo ndogo ya afrika mashariki wanaendelea kueleza kuwa ” Wanaotunga ripoti hizo hawana nia nyingine isipokuwa tu kuharibu sura ya Burundi, chama cha CNDD-FDD na vijana wake “.

Previous Mkutano wa baba François na waathiriwa wa mashariki mwa DRC: maumivu yenu ni maumivu yangu (baba mtakatifu)
Next Rumonge: a child killed and two others injured in torrential rains