Kakuma (Kenya) : Zaidi ya watu 200 wanaotafuta hifadhi ya ukimbizi wakubaliwa

Kakuma (Kenya) : Zaidi ya watu 200 wanaotafuta hifadhi ya ukimbizi wakubaliwa

Zaidi ya watu 200 walipokelewa katika vituo viwili vya muda ndani ya kambi ya wakimbizi ya Kakuma kaskazini magharibi mwa Kenya mnamo siku zilizopita. Hayo ni wakati ambapo zaidi ya wakimbizi 3500 wa burundi wa kambi ya Kakuma wanataka kurejea katika nchi yao baada ya miaka kadhaa ya ukimbizi. HABARI SOS Médias Burundi

Ripoti ya shirika la HCR-Kenya inasema kuwa nchi hiyo inaendelea kuwapokea raia wa Burundi wanaotafuta hifadhi.

Kwa mfano, kamati ya wakimbizi na HCR inahakikisha kuwa zaidi ya watu 200 raia wa Burundi walipokelewa katika kipindi kisichozidi mwezi mmoja.

Msafara wa kwanza wa watu 60 ulifika mwanzoni mwa mwezi septemba. Msafara wa pili na tatu ulifika katika mwezi oktoba ukiwa na watu 70, shirika la HCR linasema.

Wakimbizi wanaowasili wanaundwa kwa sehemu kubwa na akinamama na watoto kulingana na viongozi wa kijamii.

” Wanakuja na ma basi ya uchukuzi. Tunawapokea akinamama na watoto. Wanatoka moja kwa moja Burundi, Rwanda, Tanzania na Uganda. Wanasema kuwa wanakimbia usalama mdogo na hali duni ya maisha katika kambi ndani ya nchi hizo jirani ya Kenya”, alibaini viongozi mmoja wa kijamii.

Kwa mjibu wa taarifa zetu, warundi hao kwa sasa wanapewa hifadhi katika vituo vya muda ndani ya kambi ya Kakuma wakisuburi faili zao zishughulikiwe ili wapate hifadhi ya ukimbizi.

” Vituo hivyo viwili vimezidiwa na idadi ya watu sababu mbali na Burundi, kuna pia raia wa somalia, sudani kusini na Ethipia.Tunaomba HCR iweze kuharakisha mchakato wa kuwapa hifadhi ya ukimbizi au kuandaa kituo kingine ili kuepuka majanga” alibaini kiongozi mmoja wa kijamii eneo la kakuma.

wakati huo huo, kambi inaorodhesha wakimbizi wa burundi wanaotaka kurudi makwao.
” Hakika ni hali ya kukanganya na hatuelewi kinachoendelea. Hapa tunawapokea warundi lakini wakati huo, orodha ya wanaotaka kurudi nchini inaendelea kuwa ndefu siku baada ya siku.Jana niliona kuwa wanakadiriwa 3500″ alifahamisha raia wa Burundi anayejitolea katika mmoja kati mashirika ya kihisani katika kambi ya Kakuma.

Kambi ya Kakuma inawapa hifadhi wakimbizi zaidi ya laki mbili wakiwemo warundi elfu 20.

Previous Burundi : authorities prevent for the third consecutive year AC-GENOCIDE Cirimoso from commemorating the Kibimba massacres
Next Burundi: Viongozi walikatalia kwa mara ya tatu shirika la AC-GENOCIDE Cirimoso kuadhimisha kumbukumbu ya mauwaji ya Kibimba