Mahama (Rwanda): Hatma ya wakimbizi wa burundi mashakani

Mahama (Rwanda): Hatma ya wakimbizi wa burundi mashakani

Ujumbe mwingi rasmi na usio rasmi unawalika wakimbizi wa burundi katika kambi ya Mahama nchini Rwanda kurejea “kwa hiari” nyumbani. Kwa wahusika, Hatma yao iko katika hali ya wasi wasi. Wanahofia kuwa hatua za kuwalazimisha kurejea nyumbani kwa nguvu zitachukuliwa kama ilivyofanyika nchini Tanzania. Viongozi wa Rwanda wanawatukiza. HABARI ya SOS Médias Burundi

Dalili za awali zinawatia wasi wasi wakimbizi wa Burundi katika kambi ya Mahama mashariki mwa nchi hiyo karibu na mpaka wa Tanzania.

“Katika hizi wiki mbili, hawatupi tena mitungi ya gesi na kama unao, kujaza gesi ni shida. Chakula cha kila siku kwa mara nyingine kimepunguzwa. Hali si nzuri tunapozungumza na wadau wa HCR, nii dhahiri kuna kitu wanajuwa. Afisa mmoja wa wizara inayohusika na wakimbizi MINEMA kwanza alimuambia masikiyoni mmoja kati yetu kuwa programu ya kurejesha wakimbizi nyumbani inatakiwa kuongeza kasi na kwamba hatua za kuwalazimisha kurejea zinatakiwa kuchukuliwa”, walieleza wakimbizi wakiwemo na viongozi katika jamii hiyo.

Hivi karibuni mwezi septemba uliopita, wizara ya wakimbizi MINEMA ilitoa pendekezo kwa jopo la uongozi wa wakimbizi kujiunga na kamati ya : “Go and see” ambayo ilipaswa kuelekea nchini Burundi ili “kuangalia hali ya usalama na ukiukwaji wa haki za binadamu ili mwishowe wakirejea ndani ya kambi, waanze kuwahamisha wakimbizi wengine kurejea kwa hiari au la”.
Pendekezo hilo lilitupiliwa mbali na wahusika. Na wajumbe wa bodi ya uongozi wa wakimbizi wa burundi wakalipinga.

“Tunafahamu kinachoendelea nchini Burundi, hatuna budi kuwasili humo. Pia usalama wetu hautakuwa wa hakika, na isitoshi, nani atatembea na maafisa waliomukimbiza? Zoezi hilina umuhimu sababu tunajuwa kuwa mauwaji ya kuvizia, ukiukwaji wa haki za binadamu, na watu kupotezwa yanaendelea kuripotiwa nchini humo”, walifafanua wakimbizi hao.

Kwa wakati huu, wakimbizi wanafikiria kuwa ni mkakati mpya ulioundwa.

“Tunafahamu kuwa iwapo HCR na wizara ya wakimbizi wanalenga kitu fulani, lazima wakifikie. Kutufanya kuwa na njaa ni kitu ambacho hatutaweza kuvumilia. Kama hatuna chakula ni dhahiri kuwa tutalazimika kuchukuwa hatua ya kurejea nyumbani” alilalamika mkimbizi mmoja na kuiambia SOS Medias Burundi.

Na kama sio hivo, njia nyingine bila shaka itakuwa kuteuwa wajumbe wa tume malum ya “Go and see” yaani nenda ukaangalie ambao hawana sifa nzuri hasa kwa wakimbizi wa kambi ya Mahama.
” Hawatakosa watu hapa Kigali ambao watadai kuwakilisha wakimbizi. Kuna watu hapa wanaoshirikiana na serikali kwa uficho na hao bila shaka watakubaliana na hilo. Ni kuonyesha kuwa hatma yetu iko mashakani hapa” walisema

Kufungua mipaka, ni tishio kubwa……

Tangu serikali ya Burundi kufungua mipaka na Rwanda mwishoni mwa mwezi septemba, wasi wasi ulianza kuripotiwa katika kambi ya Mahama.

“Ikizingatiwa kuwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Kigali na Gitega unazidi kuimarika, ni wazi kwamba tutatolewa kafara kwa maslahi ya hali ya juu. Ombi la kwanza na la muhimu kwa serikali ya Burundi ni wakimbizi kurejea makwao na kambi ya wakimbizi ya Mahama inayochukuliwa kama tishio kubwa na Gitega ifungwe. Je Kigali itapinga ombi hilo, hiyo ni hesabu ambayo ni rahisi sana. Na pia usalama utaimarishwa ikizingatiwa kuwa maaduwi wanaweza kupenya” walieleza viongozi wa kijami katika kambi ya Mahama.
HCR haijatoa majibu ya moja kwa moja lakini hata hivyo inafahamisha kuwa wakimbizi katika kambi ya Mahama hawajahudhuria kwa kampeni ya kuwarejesha nyumbani kwa wingi na kwa hiari”.

“Tangu mwanzoni mwa zoezi hilo mwezi agosti 2020 na 2021, kila wiki misafara miwili ya wakimbizi zaidi ya 300 ilikuwa ikiondoka. Lakini kwa kipindi hichi, ni msafara mmoja wenye chini ya watu 150 kila wiki, na kwa mara kadhaa tunafanya msafara mmoja kwa wiki mbili”, alifahamisha afisa wa shirika la HCR. Ni kwa sababu hiyo, tathmini mpya ya hali hiyo ni lazima ifanyike, walifamisha maafisa wa wizara ya wakimbizi na HCR ndani ya kambi hiyo inayowapa hifadhi karibu wakimbizi elfu 40 kutoka nchini Burundi.

Kigali inatuliza rasmi

“Kwa wale ambao hawataiki kurudi nyumbani ambao wahisi usalama wao utakuwa haujalindwa, tutaendelea kuwahidhi, kambi haitafunga milango kwa wanaotafuta hifadhi ya ukimbizi hata kama masharti ni magumu kwa sasa,” alifahamisha hayo katibu wa kudumu katika wizara ya wakimbizi.

Kulingana na HCR, Rwanda inawapa hifadhi zaidi ya wakimbizi kutoka burundi zaidi ya elfu 48, huku elfu 39 wakiwa katika kambi ya Mahama. Serikali ya Burundi imekuwa ikiomba kambi hiyo ifungwe. Inayochukuliwa kama eneo kubwa la kuwajiri wapiganaji dhidi ya serikali ya Burundi hasa kutoka mkoa wa Kivu-kusini mashariki mwa DRC ambako vikosi viwili vya jeshi la burundi vilitumwa rasmi tangu kati kati mwa mwezi agosti

Previous Muyinga: more than 50 opponents in detention
Next Burundi: lack of fertilizers for farming season A