Vita nchini DRC: M23 yaacha sehemu ya ngome zake

Vita nchini DRC: M23 yaacha sehemu ya ngome zake

Ijumaa hii, kundi la M23 limefahamisha rasmi kuwa wapiganaji wake wamejiondoa kwenye ngome zao za Kibumba. Ni kwenye umbali wa takriban kilometa 20 kutoka mjini Goma, makao makuu ya mkoa wa Kivu kaskazini (mashariki mwa DRC). Kundi hilo la silaha limefafanua kuwa limetaka kuonyesha nia yake ya kuchangia katika kurejesha amani ya kudumu baada ya mazungumzo ya hivi karibuni kati yake na wawakilishi wa jeshi la Kongo, kikosi cha kikanda na mchakato wa kuhakiki wa CIRGL (kongamano la kimataifa la kanda ya maziwa makuu). HABARI SOS Médias Burundi

Ni msemaji wa kundi la M23 aliyetangaza habari hiyo ijumaa hii.

” Licha ya mashambulizi dhidi ya ngome zetu na mauwaji ya wananchi wetu yanayofanywa na muungano wa serikali, kundi la M23 linaunga mkono juhudi za kikanda na kukubali kuacha ngome zake za Kibumba na kuziweka chini ya mamlaka ya kikosi cha kikanda cha EAC” limefamisha tangazo la kundi hilo la silaha lililosainiwa na Lawrence Kanyuka msemaji wake wa kisiasa.

Na kuzidi kuwa” tunatumai kuwa serikali ya Kinshasa itachukuwa fursa hii na mikono miwili na itafanya juhudi pia ili kurejesha amani katika nchi yetu”.

Tarehe 12 hadi 22 disemba, kundi la M23 lilipokea wajumbe wa kikosi cha kanda la EAC, mchakato wa kuhakiki wa CIRGL pamoja pia na wawakilishi wa jeshi la FARDC ( jeshi la jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo).

Kibumba ni eneo la wilaya ya Nyiragongo chini ya udhibiti wa kundi la M23 tangu miezi miwili iliyopita. Mapigano makali yalifanyika kati ya kundi la M23 na jeshi la Kongo eneo hilo kusababisha idadi kubwa ya wananchi kukimbia.

Msemaji wa jeshi la Kongo hakupatikana ili kujieleza juu ya hatua hiyo ya M23.

Lakini akizungumza na wandishi wa habari kutoka eneo la Kibumba, jemedali Jeff Nyagah, kamanda wa kikosi cha kikanda aliwaomba wananchi ” kurejea makwao ” na kuwaahidi kuwa watakuwa salama.

Tangu juni mwaka huu, kundi hilo la zamani la watutsi lililochukuwa tena silaha mwishoni mwa mwaka wa 2021 linatuhumu viongozi wa Kongo kuacha kutekeleza ahadi zake za kurudisha wapiganaji wake katika maisha ya kawaida. Kundi hilo lilichukuwa udhibiti wa maeneo mengi ya mkoa wa Kivu kaskazini likiwemo eneo la Bunagana jiji la mpakani na Uganda.

Hivi karibuni, serikali ya Kongo lilituhumu kundi hilo la waasi kufanya mauwaji ya wananchi 272 wakiwemo watoto 17 katika vijiji viwili, huku umoja wa mataifa ukisema waliuwawa ni watu 130. Kundi la M23 linatupilia mbali tuhumu hizo na kuomba uchunguzi huru ufanyike.

Viongozi wa Kongo wanaendelea kukubali kuwa Rwanda inaunga mkono waasi hao, jambo ambalo serikali ya Rwanda inaendelea kukanusha na kutupilia mbali.

Previous Bubanza: an armed band of thieves sows panic
Next War in the DRC: the M23 gives up part of its positions