Rwanda-DRC: mwanajeshi wa Kongo wa pili kuuwawa na jeshi la Rwanda
Jeshi la Rwanda limefamisha kuwa limemuuwa mwanajeshi wa Kongo jumamosi tarehe 19 novemba. Jeshi linaendelea kuwa amevuka mpaka na kuanza kuwapiga risasi wanajeshi wake. HABARI SOS Médias Burundi
Ni kupitia tangazo ambapo jeshi la Rwanda limetangaza kifo cha mwanajeshi huyo wa FARDC (Jeshi la jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo) .
Tamko hilo linasema kuwa alikuwa akipiga risasi kwenye ngome za jeshi la Rwanda wakati alipopigwa risasi na kufariki.
Kisa hicho kimetokea katika eneo la mpakani linalojulikana kama “petite barrière”. Ni kati ya wilaya ya Rubavu (magharibi mwa Rwanda) na mji wa Goma (makao makuu ya mkoa wa Kivu ya kaskazini) mashariki mwa DRC.
Viongozi wa Kongo hawajasema lolote kuhusu kisa hicho.
Mwanzoni mwa mwezi juni mwaka huu, mwanajeshi mwingine wa Kongo aliuwawa na polisi wa Rwanda kwenye kizuizi hicho wakati akiwapiga risasi maafisa wa idara ya uhamiaji na raia wa kawaida, kwa mjibu wa jeshi la Rwanda.
Tukio hilo kilisababisha malalamiko makubwa ndani ya miji ya mashariki mwa Kongo. Mashirika ya kiraia na makundi mengine ya shinikizo yaliomba viongozi wa Kongo ” kufunga mipaka yake na Rwanda “.
Katika visa hivyo viwili, jeshi la Rwanda linafahamisha kuwa lilitoa taarifa kwa shirika la CIRGL (kongamano la kitaifa katika kanda la maziwa makuu)
You might also like
Matana: 12 individuals arrested after the death of a child
The body of Bienvenue Nshimirimana (4 years old) was found this Sunday in a forest at Matana. It is in the commune of Matana, Bururi province (southern Burundi). At least
Masisi : jeshi la FARDC linajaribu kuwaondoa waasi wa M23, waasi wamewashinda
Mapigano makali yaliripotiwa kati ya jeshi la Kongo na waasi wa M23 katika maeneo mengi ya wilaya ya Masisi ndani ya mkoa wa Kivu kaskazini mashariki mwa Kongo siku ya
North Kivu: the M23 accused of murdering civilians demands an independent investigation
A hundred civilians were killed by gunmen assimilated to the March 23 movement (M23) rebels this week in the village of Kisharu, Binza groupement and in Kishishe, a village in
