Masisi : jeshi la FARDC linajaribu kuwaondoa waasi wa M23, waasi wamewashinda

Masisi : jeshi la FARDC linajaribu kuwaondoa waasi wa M23, waasi wamewashinda

Mapigano makali yaliripotiwa kati ya jeshi la Kongo na waasi wa M23 katika maeneo mengi ya wilaya ya Masisi ndani ya mkoa wa Kivu kaskazini mashariki mwa Kongo siku ya jumanne tarehe 31 januari 2023. Jeshi la Kongo lilipiga mabomu kwenye mgome za M23 katika eneo la jiji la Kitchanga, lililoanguka katika mikono ya waasi wiki moja iliyopita. Lakini waasi wamejihami. HABARI SOS Médias Burundi

Mapigano yaliripotiwa katika maeneo mengi kama Burungu, Kilolirwe, Kitshanga ndani ya kitongoji cha Bashali.

” Mapigano yaliendelea siku nzima katika maeneo ya Rusinga/ Ndondo ni kwenye umbali wa kilometa takriban mbili kutoka Kitchanga kuelekea Mweso katika kitongoji cha Bashali Mukoto ndani ya Masisi lakini pia eneo la Kitobo kilometa tatu kuelekea Kitchanga. Hakuna upande uliorudisha nyuma mwingine. Ndege ya FARDC ilirusha mabomu kwenye ngome za M23 lakini Kitshanga imesalia chini ya udhibiti wa M23″, alitoa ushuhuda huo mkaazi wa Kitchanga aliyezungumza na SOS Médias Burundi jumanne jioni majira ya saa tano usiku.

Familia nyingi zimesalia hadi sasa katika uwa wa kituo cha Monusco ( ujumbe wa umoja wa mataifa nchini RDC) eneo la Kitchanga. Wengine hawakupata nafasi ndani ya kituo hicho. Walisalia katika maeneo ya karibu. Ma kumi ya wandishi wa habari wa ndani pia wanaosubiri kuokolewa, wamepewa hifadhi ndani ya kituo hicho cha umoja wa mataifa. Ni budi kufamisha pia kuwa mapigano mengine yaliripotiwa kwenye njia ya kaskazini kuelekea Kishishe kwa siku nzima. Waasi walikuwa na lengo la kupenya na kuelekea katika kitongoji cha Mutanda ndani ya kijiji cha Bwito, kwa mjibu wa vyanzo vya ndani.

Mapigano yaliibuka tena hivi karibuni kati ya FARDC na waasi wa kundi la machi 23. Pande hizo mbili zinatuhumiana kuvunja mkataba wa kusitisha mapigano, kundi la M23 likielezea sababu za kuanza tena makabiliano kuwa ni kwa lengo la ” kuwalinda watutsi waliowachache dhidi ya mauwaji ya halaiki yaliyoandaliwa na Kinshasa pamoja na washirika wake”.

Hali ya mashariki mwa Kongo imetokana na kuharibika kwa uhusiano kati ya DRC na Rwanda. Nchi hizo mbili ya kanda ya maziwa makuu ya Afrika zinatuhumiana uhaini.

Tangu kuibuka tena kwa kundi la M23 waasi wa zamani wa jamii ya watutsi waliochukuwa sihala mwishoni mwa 2021, wanatuhumu viongozi wa Kongo kushindwa kutekeleza ahadi zake za kurejesha wapiganaji wake katika maisha ya kawaida. Viongozi wa Kongo wanahakikisha kuwa kundi hilo linapata usaidizi wa Rwanda. Nchi hiyo imekuwa ikitupilia mbali madai hayo ni kutuhumu upande wake Kinshasa kushirikiana na kundi la FDLR la waliotekeleza mauwaji ya halaiki nchini Rwanda kwa kuwapa sare silaha na risasi ili waweze kusambaratisha ardhi yake.

Baada ya kumufukuza balozi wa Rwanda mjini Kinshasa na kuwakamata watu wawili wenye asili ya Rwanda ambao walikuwa wafanyakazi wa shirika la misaada la Afrika kwa ajili ya maendeleo ya afya kwa tuhma za kuwa wapelelezi na kupanga shambulio dhidi ya ndege ya rais wa Kongo Félix Tshisekedi, viongozi wa Kongo waliamuru jumanne hii waondolewe maafisa wa jeshi la Rwanda waliokuwa wakihudumu katika uongozi kuu wa jeshi la EAC wenye makao yake mjini Goma ( makao makuu ya Kivu-kaskazini) Hali hiyo ilipelekea Rwanda kuitisha maafisa wa jeshi wote wanaohudumu katika michakato ya kikanda ambao wako katika nchi hiyo ya Afrika ya kati kwenye hiyo siku hiyo hiyo.

Previous Bujumbura: two sites declared areas of public utility
Next Burundi: IDHB notes a precarious lull and a fierce struggle at the top of the regime