Minembwe : kundi la Mai Mai limemuuwa mzee mmoja na kupora ng’ombe 150
Ndagara Buhimba (Miaka 80) aliuwawa siku ya jumatatu alasiri. Kundi la Mai Mai lilirejuhi pia watu 2 na kuiba ng’ombe 150. HABARI ya SOSMedias Burundi
Muhanga alikuwa katika malisho yaliyo katika eneo la Monyi wakati waasi wa Mai Mai waliopomuuwa kulinga na mashahidi.Ni katika kanda ya Minembwe wilaya ya Fizi katika mkoa wa Kivu ya kusini mashariki mwa DRC.
Kifo cha mzee huyo kutoka jamii ya Banyamulenge kinathibitishwa na familia yake.
” Asubuhi hii ndipo muili wake umepatikana.Ni vitendo vya kinyama vinavyofanyika hapa. Watu wanauwawa kama wanyama wanachinjwa”, amelalamika mkaazi mmoja.
Vyanzo sehemu hiyo vinahakikisha kuwa watu wengine wawili walijeruhiwa wakati wa shambulio hilo ‘a ng’ombe 150 kuibiwa.
Msemaji wa kundi la Mai Mai hakuwa karibu ili aweze kujieleza juu ya malalamiko hayo. Wakuu wa jeshi na viongozi tawala pia hawajasema lolote.
Siku ya jumapili, kijana mdogo aliuwawa kwa kukatwa na panga na askali wa jeshi la FARDC ( jeshi la jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo ) katika eneo hilo la Minembwe , kisa ambacho kilisababisha mandamano katika shule zote ijumatatu eneo la Minembwe.
Wakaazi wa eneo la Minembwe ambao wengi wao ni kutoka jamii ya Banyamulenge wanalituhumu jeshi la Kongo kutuwahami wakati wakilengwa na mashambulizi ya makundi ya silaha.
Ni tangu miaka mitano tukiuwawa bila hata hivo jeshi la FARDC kuingilia kati ili kutulinda wakati ambapo tuko raia wa Kongo ” analalamika diwani mmoja
You might also like
RDC-EAC: mchakato wa kuhakiki na kufuatia hali mashariki mwa DRC unaelekea kuanzishwa
Jumuiya ya Afrika mashariki inapanga kutuma wajumbe wa mchakato wa kuhakiki na kufuatia hali mashariki mwa DRC ambao ni muhimu sana ili kumaliza mzozo. Hayo ni kulingana na tangazo lililowekwa
Ituri/Kivu-kaskazini: miili ya raia wa kawaida 27 waliouwawa na wapiganaji wa ADF imepatikana katika eneo la Irumi na Béni
Miili 2O ya watu waliouwawa na waasi kutoka Uganda wa ADF (kundi la waasi) iligunduliwa katika vijiji vingi vya eneo la Irumi mkoa wa Ituri mashariki mwa DRC. Maiti zingine
Nairobi: the protagonists in the Congolese crisis meet without the M23
Since Monday, November 28, a meeting is talking place in Nairobi, for six days without the M23, to deal with the Congolese crisis. The M23, a rebel movement which seized
