Burundi: Kipindi cha jua kali chaikabili nchi, serikali inamulilia Mungu

Burundi: Kipindi cha jua kali chaikabili nchi, serikali inamulilia Mungu

Tangu septemba 2022 , takriban kwenye ardhi yote ya Burundi mvua haijanyesha. Kipindi cha kipwa kinarefuka, wananchi wako katika wasi wasi mkubwa na serikali anawaomba waumini kumulilia Mungu ili mvua ipatikane. HABARI SOS Medias Burundi

Wananchi katika mikoa ya Cibitoke (kaskazini-magharibi) wanapoteza matumaini kutokana na juwa kali.

” Hakuna hata tonya la mvua tangu septemba hadi sasa. Mashamba yote yamekauka. Baa la njaa lililokuwa linapiga hodi mlangoni kwa miezi, sasa linakuja kutukuta” , atahadharisha mkaazi mmoja wa Gihanga na Rugombo katika mikoa ya Bubanza na Cibitoke.Tarafa hizo mbili ni kati ya zile zenye mavuno mengi.

Mkoani Kirundo kaskazini, viongozi tawala wanafahamisha kuwa mkoa huo unakabiliwa na ukame mkubwa. Familia nyingi zinahofia kupata matatizo makubwa katika mkoa huo ambao zamani ulikuwa kama ghala la Burundi lakini unakabiliwa na ukame kwa miaka.

Mkoa wa Muramvya (kati kati) unaopakana na msitu wa Kibira unakabiliwa na hali kama hiyo kinyume na ilivyokuwa katika misimu mingine.

Kusini mashariki mwa nchi, ukame unakabili pia eneo hilo linalopakana na Tanzania na wakaazi wa eneo hilo wanalalamika kuwa wanakabiliwa na mtihani wa joto kali nyakati za usiku. Mikoa ya Bururi na Rumonge ( kusini magharibi) haikuepukika. Mikoa hiyo haijashuhudia mvua tangu septemba.

Kutokana na hali hiyo ya nchi, viongozi wanaomba viongozi wa kidini na waumini kumulilia Mungu ili mvua ipatikane.

[….] Ninawaomba kutoa maelekezo kwa wakuu wa tarafa, anza mawasiliano na viongozi wa dini/madhehebu/Parokia/Misikiti …..tangu kesho asubuhi na jumapili, wafanye maombi ya pamoja ili kumulilia Mungu mvua ipatikane nchini Burundi. Ni pia fursa kuwahamasisha wananchi kunyunyizia maji na/ kufanya umwagiliaji mahala pote inapowezekana ” , tunayasoma hayo katika ujumbe ulitumwa kwa ma gavana wa mikoa na meya wa jiji la kibiashara la Bujumbura siku ya ijumaa.

Vyanzo katika serikali ya Burundi wanalaani kuwa sera ya rais Ndayishimiye ya kuimarisha kilimo haitaweza kutekelezwa.

“Sera ya serikali ya kuweka kipau mbele kilimo imepata changamoto. Muongozo wa rais Neva kwamba ” Kila mdomo upate chakula na kila mfuko upate pesa hauwezekani”, walibaini.

Wananchi wa burundi wanaishi kwa kilimo na ufugaji. Ukame unaoikabili nchi ni pigo kubwa kwa taifa hilo la afrika ya kati.

Kawaida kipindi cha mvua kinachodumu miezi tisa, huanza na mwezi septemba na kumalizika katika mwezi mei, mwezi juni ukishuhudia mvua kwa kiwango kidogo. Mwaka huu hamna hata tonya la mvua lililoanguka tangu septemba iliyopita.

Katika mikoa mingi, magavana na ma askofu wa dini ya katolika, wametoa tangazo la kuwaalika waumini kufanya maombi maluum wekendi hii ili mvua iweze kurejea .

Previous Burundi: Pig disease kills several of them
Next Kabarore : teachers forced to give contributions