Burundi: viongozi wakataza mashirika ya kutetea haki za manusura wa mauwaji ya watutsi kutoa heshma kwa watu wao

Burundi: viongozi wakataza mashirika ya kutetea haki za manusura wa mauwaji ya watutsi kutoa heshma kwa watu wao

Viongozi wa burundi wamekataza mashirika yote ya kutetea haki za jamii ya watutsi, manusura na wazazi kuelekea kwenye mnara wa Kwibubu ili kuomboleza kifo cha wanafunzi 150 wa jamii ya watutsi. Wahusika wameitaka serikali kubatilisha uamzi huo. HABARI SOS Médias Burundi

Katika tangazo la pamoja, mashirika hayo yameandika kuwa ni waziri wa mambo ya ndani aliyepinga sherehe hizo. Aliwakaribisha ofisini kwake mara tatu lakini akawapokea Mara mbili. Wawakilishi wa mashirika hayo wanalaani hatua hiyo ambayo haina misinga ya kisheria.
Isitoshi, wanaendelea kusema, ” waziri hakutupatia majibu kupitia barua wakati ambapo tuliomba ruhsa kupitia barua.”

” Sina majibu ya kuwapa kupitia barua ” alijibu Martin Niteretse waziri wa mambo ya ndani”. Wawakilishi wa mashirika ya manusura wazazi wa wanafunzi wa jamii ya watutsi waliuwawa walimuomba majibu kupitia barua ya kuwakataza kwenda kutoa heshma kwa watato kwenye mnara wa ukumbusho wa Kwibubu tarafani Giheta mkoa wa Gitega ( kati kati mwa Burundi). Aliwambia mara tatu kuwa wanatakiwa kuelekea kwenye makaburi ya hayati Melchior Ndadaye na washirika wake na kuweka shaada za mauwa sababu “Ndadaye alikuwa shujaa wa taifa”.

Jeanne Rutamuceru mjumbe wa shirika la manusura wa mauwaji kwenye shule ya Kibimba anasema ” ni ukiukwaji wa mkataba uliosainiwa na Burundi kuhusiana na haki za binadamu”.

” Cha kusikitisha ni kwamba amekataa na kutupatia siku nyingine ambako tunaweza kwenda kutoa heshma kwenye makaburi ya pamoja ya watu wetu”, alalamila Rutamuceru.

Aidha wakili Christian Ntakarutimana wa chama kimoja cha mawakili (Raja), chama cha CNDD-FDD inataka kutendea haki wahutu huku ikinyanyasa watutsi

” Chama cha CNDD-FDD anaendelea kujikama kama wakati ikiwa musituni” alitoa tuhuma hizo mkaazi mmoja.

Anaona kuwa Burundi haitatenda haki kwa wote katika kipindi ambacho kikundi cha zamani cha waasi cha kihutu kitakuwa madarakani.

Mashirika yanasema ni hatua inayoegamia upande mmoja ikizingatiwa kuwa mashirika ya haki za wahutu wanaruhusiwa kuomboleza watu wao waliouwawa. Wanaomba serikali kusimamisha hatua hiyo ambayo inaweza kuharibu mchakato wa maridhiano kati wa warundi.

Hii imekuwa mwaka wa tatu viongozi wa Burundi wakikataza mashirika yanayotetea haki za wahanga wa jamii ya watutsi kuelekea kwenye mnara wa Kwibubu.
Lakini ni mara ya kwanza ambapo hakuna wajumbe wanaruhusiwa kuwasili eneo hilo. Miaka miwili iliyopita idadi ndogo ( wasiozidi kumi) walikuwa wakiruhusiwa kuweka shaada za mauwa katika kukumbuka wahanga wa mauwaji ya Kibimba na kutoa hutba.

Kumbuka kuwa zaidi ya wanafunzi 150 wa kabila la Batutsi kwenye shule ya Kibimba walikusanywa ndani ya kituo cha mafuta eneo la Kwibubu tarehe 21 oktoba 1993 kabla ya kuuwawa kikatili. Baadhi walichomwa moto wengine wakakatwa vichwa. Ilikuwa baada ya kuuwawa kwa rais wa kwanza wa kabila la wahutu aliyechaguliwa kidemokrasia Melchior Ndadaye ambapo kifo chake kilifuatiwa na mauwaji ya raia wa kabila la watutsi kwenye ardhi yote ya Burundi.
Kiongozi wa shule peke alihukumiwa katika kesi hiyo.

Wakiwa madarakani tangu 2005 kutokana na makubaliano ya amani ya Arusha, kikundi hiki cha zamani cha waasi wa kabila la wahutu CNDD-FDD wanakosolewa kwa ” kupendelea wahanga wa kabila la Bahutu” huku wakikiuka haki za manusura wa jamii ya watutsi na mashirika yanayotetea haki za wathiriwa wa kabila la Batutsi.

Wengi katika Wale ambao wako madarakani walikuwa wahanga wa mauwaji ya mwaka 1972 yaliyosababisha vifo vya wahutu na watutsi. Wanatetea ili mauwaji hayo yachukuliwe kama mauwaji ya halaiki ” Genocide” jambo lilikamilishwa na bunge la taifa mwishoni mwa mwaka wa 2021 kupitia ripoti inapingwa ya tume ya ukweli na maridhiano ambayo Neva alipinga kuidhinisha mwezi mei mwaka huu.

Previous Bubanza: former MP Fabien Banciryanino sparks controversy
Next Burundi: from now on all field visits by administration staff will be financed by NGOs