Nyarugusu (Tanzania): Kampeni dhidi ya Malaria

Nyarugusu (Tanzania): Kampeni dhidi ya Malaria

Shirika la HCR kwa ushirikiano na serikali ya Tanzania imeandaa Kampeni ya kunyunyizia dawa katika majumba, maeneo ya maji taka yaliyoganda pamoja pia na maeneo ya wazi yaliyo karibu na makaazi ya watu ndani ya kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu. Badaye vyandarua vilivyonyunyiziwa dawa vitatolewa kulingana na duru kutoka HCR. Kwa mjibu wa vyanzo vyetu, ugonjwa wa malaria umeibuka ndani ya kambi ya Nyarugusu na katika nchi nzima ya Tanzania. Nchi hiyo imeimarisha vita dhidi ya ugonjwa huo katika maeneo ambayo yako hatarini yakiwemo makambi ya wakimbizi. HABARI SOS Médias Burundi

Kampeni ilianzia katika zone ya 12 na 13 ambako kulishuhudia visa vingi vya malaria na itaendelea katika maeneo mengine ya kambi ya Nyarugusu.

Kampeni hiyo inafanyika katika maeneo yanayoikaliwa na warundi kadhalika na wakongomani.
Hayo ni wakati vitanda vya hospitali vimezidiwa na idadi ya wagonjwa ndani ya kambi ya Nyarugusu. HCR na washirika wake wanataka kupunguza madhara.

” Wathiriwa zaidi ni watoto wa chini ya miaka mitano, akinamama wajawazito, pamoja pia watu wazima. Kuna waliokwisha fariki. Kwa hiyo tunatakiwa kuchukuwa hatua kwa wakati ili kukinga athari mbaya” alifahamisha afisa wa HCR.

Wakimbizi wanakaribisha kampeni hiyo. Wanatumia fursa hiyo kuomba HCR iwakabidhi vifaa vya usafi kama sabuni na vyombo vya kupikia ambapo kwa mjibu wao wamedumu navyo kwa miaka zaidi ya mitano.

Kambi ya Nyarugusu inaorodhesha wakimbizi zaidi ya laki moja na elfu 20 wakiwemo warundi elfu 49, huku wanaosalia wakiwa raia kutoka Kongo

Previous Nyarugusu (Tanzania): a campaign against malaria
Next North Kivu: renewal of fighting between the FARDC and the M23 in Rutshuru