Mgogoro mashariki mwa Kongo: EAC inapendelea viongozi wa kijamii kuliko kundi la M23 katika mazungumzo

Mgogoro mashariki mwa Kongo: EAC inapendelea viongozi wa kijamii kuliko kundi la M23 katika mazungumzo

Rais wa burundi kwa tikiti ya mwenyekiti wa EAC (Jumuiya ya afrika mashariki) ijumaa alimpokea rais mstaafu wa Kenya ili kujadili njia za kumaliza mgogoro unaoendelea mashariki mwa Kongo. Wanafahamisha kuwa awamu nyingine ya mazungumzo itafanyika Nairobi kuanzia tarehe 16 novemba. Kundi la M23 kundi la waasi la zamani la watutsi lilichokuwa tena silaha mwishoni mwa mwaka wa 2021ambalo linatuhumu Kinshasa kutoheshimu ahadi zake za kuwaingiza wapiganaji wake jeshini limebaguliwa. Viongozi wa kijadi na kijamii ndio wamechaguliwa. HABARI SOS Médias Burundi

Watu hao wawili walimaliza masaa mengi wakiwa pamoja siku ya alhamisi alasiri katika ofisi ya rais Neva ndani ya jiji kuu la biashara la Bujumbura. Baadaye walijieleza kwa wandishi wa habari kwa lugha ya kiswahili peke yake.

Rais wa Burundi ambaye hivi karibuni alichukuwa kiti cha uongozi wa mzunguko wa EAC alithibitisha kuwa makundi mengi ya silaha yaliweka silaha chini ili kujiunga na mazungumzo ya Nairobi. Alitoa mfano wa kundi la waasi la kivu ya kusini ( mashariki mwa DRC) ambapo nchi yake ina vikosi viwili kupitia jukwa la ushirikiano kati ya nchi hizo mbili na chini ya uongozi wa EAC.

” Tulishuhudia eneo la kivu ya kusini ambalo liko karibu yetu na tukagundua makundi mengi ya silaha yaliweka silaha chini na yanasema kuwa yako tayari kushiriki mazungumzo ya Nairobi. Kundi la Mai Mai liliweka silaha chini, Gumino lilitia silaha chini” , alisema.

Kwa mjibu wa Bwana Ndayishimiye, kundi la M23 halihusishwi na mazungumzo ya Nairobi, bali linahusishwa na mchakato wa Luanda ( Angola).

Ndani ya EAC, tunashughulishwa na makubaliano kati ya serikali ya Kongo na makundi ya ndani. Kundi la M23 linahusika na mchakato wa Luanda. Tuliona tuwaalike viongozi wa kijadi na kijamii katika mazungumzo ya Nairobi sababu makundi ya silaha yanatoa hoja kuwa yalichukuwa silaha ili kulinda jamii zao” alizidi kusema rais Neva.

Kulingana na mpatanishi Kenyatta, raia wa Kongo wanatakiwa kuangalia mfano wa Burundi.

” Ndugu zetu wa Kongo wanatakiwa kuelewa kuwa vita na silaha sio suluhu. Suhulisho litatoka katika mazungumzo kati ya wadau ” alibaini Uhuru Kenyatta.

Na alihakikisha ” Nina imani kuwa wandugu zetu wa Kongo watapata amani na maendeleo wakitizama mfano wa Burundi kuliko kuendelea na mauwaji na vilio” .

Fidèle Sebahizi mmoja kati ya wataalam wa maswala ya Kongo aliyefanya masomo ya Phd kwenye chuo cha Virginie anasema kuwa wadau wa mgogoro wa Kongo wanaobagua kundi la M23 katika mazungumzo wanajidanganya.

[….], Hakika serikali ya Kongo inatuhumu kundi la M23 makosa mengi. Kuliko kuituhumu Rwanda kusaidia kundi hilo, wangelihusisha katika mazungumzo sababu ni kundi peke lenye nguvu uwanjani. Serikali ya Kongo ingetakiwa kusikiliza kundi la M23 sababu kundi hilo linaundwa na raia wa Kongo. Viongozi wa Kongo wanatakiwa kusikiliza madai yao kuliko kuwabagua. Hata kama watawafukuza leo, watarudi kesho kama tulivyoshuhudia baada ya 2013 sababu ni raia wa Kongo. Hawana mahala ambapo wanaweza kwenda, hawana nchi nyingine mbali na Kongo “, alisema Sebahizi.

Previous Crisis in Eastern Congo: EAC prefers community leaders to M23 in dialogue
Next Burundi: unions concerned about the rise in the price of basic necessities